posted by Esta Malibiche on JUNE 14,2017 IN MICHEZO
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), linawaalika wanafamilia wote wenye nia ya kuwania
uongozi katika shirikisho kujitokeza kuchukua fomu kuanzia Juni 16,
mwaka huu.
Tarehe hiyo ni ileile
iliyotangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili
Revocatus Kuuli alipozungumza na wanahabari Jumatatu wiki alipotangaza
ratiba nzima ya Uchaguzi Mkuu wa TFF uliopangwa kufanyika Agosti 12,
mwaka huu.
Kwa kuwa tovuti ya TFF: www.tff.or.tz
kwa sasa ipo kwenye marekebisho, zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi TFF zitatolewa kwenye ofisi za TFF
zilizopo Ilala, Dar es Salaam kuanzia asubuhi ya Juni 16, 2017 hadi saa
10 jioni siku ya Juni 20, mwaka huu.
Fedha za kulipia fomu hizo
zitalipiwa Benki ya CRDB kupitia namba ya akaunti 01J1019956700 ambako
mgombea atawajibika kuwasilisha stakabadhi ya malipo kutoka benki na
kupewa fomu ya nafasi husika.
Gharama za kuchukulia fomu ni.
1. Rais TSHS 500,000/=
2. Makamu wa Rais TSHS 300,000/=
3. Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/=
0 maoni:
Chapisha Maoni