Ijumaa, 23 Juni 2017

TAARIFA YA JESHI LA POLISI , TAHADAHARI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL FITR

Posted by Esta Malibiche on JUNE 23,2017 IN NEWS

                                    23/06/2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El Fitri,  Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao.  Kipindi kama hiki cha sikukuu baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu na vitendo vingine ambavyo huhatarisha usalama wa watu na mali zao.  
Hata hivyo,   Jeshi la Polisi nchini,  limejipanga kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhakikisha kwamba  wananchi wanasherehekea Sikukuu katika hali ya amani  na utulivu.  
Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu. 
Vilevile,  Jeshi la Polisi linawatahadharisha watumiaji wa vyombo vya moto barabarani kuwa makini  na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani,  Jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kwa wale wote watakaovunja  sheria na kanuni za usalama barabarani kwa mabereva kutumia vilevi, bodaboda kubeba  mishikaki, kwenda mwendo kasi pamoja na kupiga honi hovyo.
Pia, tunawataka  wananchi wote kuwa wepesi katika  kutoa taarifa kwa kupitia  namba za simu za bure 111 au 112  pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara. 
         Tunawatakia watanzania wote Sikukuu njema ya Eid El Fitri.

    Imetolewa na:
Advera John   Bulimba -ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi

0 maoni:

Chapisha Maoni