Posted by Esta Malibiche ON JUNE23,2017 in NEWS
Na Tiganya Vincent
IGUNGA
Askofu
Henery Minani wa Makanisa la Pentecostal kutoka Uganda amesema uongozi
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli
utasaidia wananchi wengi kunufaika rasilimali walizopewa na Mungu.
Kiongozi
huyo alisema hayo jana wilayani Igunga wakati wa kongamano la Kwaya
kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo pamoja na uimbaji waliendesha
maombi mbalimbali ya kuombea nchi na viongozi wake.
Alisema
kuwa Mungu aliamua kuwapa wananchi wa Tanzania Rais Magufuli ili
awaongoze katika kuibadilisha nchi hii kutoka ilipokuwa na kuwa ya neema
kwa watu wote kwa kufaidi utajiri walipewa na Mungu.
Akifungua
kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alisema kuwa
kazi nzuri aliyoiana Rais katika vita ya uchumi inahitaji kuungwa mkono
na viongozi wa dini ili Mungu ampe nguvu katika mapambano ambayo
yanalenga kuwaleta maisha bora wananchi wengi kwa kunufaika na
rasilimali zao.
Alisema
kuwa Rais Magufuli akiachwa pekee bila msaada wa maombi na dua kutoka
kwa viongozi wa dini Shetani anaweza kupata nafasi na zoezi hilo likawa
gumu.
Bw.
Mwanri alisema kuwa yeye kama Mkuu Mkoa kwa niaba ya wananchi wa Tabora
wanaungana na Rais Magufuli katika vita hiyo na hawatamuacha apigane
pekee yake wako nyuma yake na wataendelea kumuombea kwa Mungu.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewaomba viongozi wa dini kuuombea
Mkoa wa Tabora ili mauji yanatokana na ushirikina, wivu wa kimapenzi,
ujambazi na kulipa visasi yakome.
Alisema kuwa mauaji hayo yamekuwa yakinyima usingizi na hivyo kwa nguvu ya maombi na ya dola mauaji hayo yatakoma.
Bw.
Mwanri alisema kuwa viongozi wa dini hawawezi kujitoa katika mapambano
dhidi ya mauji hao, kwani wakijitoa na kuiachia Serikali pekee yake damu
ya watu inayomwagika itakuja kuwalilia.
Kongamano
hilo la Kwaya ambalo linawashiriki kutoka Tanzania, Kenya na Uganda
limeandaliwa na Kanisa la FPTC na linalizika Jumapili hii.
0 maoni:
Chapisha Maoni