Posted by Esta Malibiche on JUNE 5,2017 IN NEWS
Na Esta Malibiche
Mufindi
WATANZANIA
wametakiwa kumuombea Mh.Rais wa Jamhuri
ya Muuungano wa Tnazania Dkt.John Pombe Magufuli kutokana na kazi kubwa anayoifanya kuwatumikia wananchi na kuhakikisha
lasilimali za Nchi zinawanufaisha watanzania wote.
Kauli hiyo imetolewa
jana na Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba wakati akizungumza wna
wananchi wa amkoa wa Iringa katika Halmashauri ya wilaya ya Mfindi kwenye
tamasha la uzinduzi sa nyimbo za Injili kwaya ya Mtakatifu Secilia parokia ya
Mafinga Jimbo Katoliki la Iringa.
Katika
uzinduzi huo waziri Mwigulu aliambatana na Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Iringa
Rose Tweve,Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi,Mkuu wa Wilaya ya Mufindi
Willium Jamuhuri,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga pamoja na Viongozi
wa vyma vya Siasa.Katika uzinduzi huo jumla ya Mill.24 zilichangwa,ambapo yeye
na familia yake walikabidhi kisai cha Tsh.5 Mill.
Katika Hotuba yake Waziri Mwigulu alisema
Mh.Rais anania nzuri kwa watanzania,hivyo hatuna budi kumuombea kila mmoja kwa
dini yake ili awewe kuendelea kuwatumika wananchi kwa kutatua changamoto
mbalimbali.
‘’Tuendendelee
kumuombea Rais wetu bila kukoma kwa kazi yake kubwa nayoifnya na kwa hatua anaozozifanya kuhakikisha rasilimali za Tanzania zinalindwa na hatimae kuwanufaisha watanzania wote bila
kubagua dini,kabila wa itikadi za siasa.’’Alisema Mwigulu.
Aidha Waziri
Mwigulu amewataka viongozi wa dini kuhakikisha wanatoa Elimuya ya kutosha kwa waumini wao kuhusu vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia,ubakaji kwa
watoto wadogo,ulawiti na mauaji ya vikongwe.
Alisema
viongozi wa dini wanayonafasi kubwa ya kuongea na waumini wao na wakasikilizwa
kutokana na kalama aliyowapatia Mwenyezi Mungu,kwa kuisaidia Serikali wanao uwezo mkubwa kukemea
ili vitendo hivyo na mtukio ya
kiuharifu yasiendelee kutokea hapa Nchini.
Tuendelee
kushirikiana na Serikali na wizara ya ndani kukemea vitendo viovu vinavyokiuka
madili ya kitanzania,hasa katika maeneo ambayo wananchi hawashiriki katika
imani.Pamoja na serikali kuweka nguvu kubwa kukemea lakini viongozi na wazaZi
mna jukumu kubwa la kuongea na waumni wenu pamoja na familia zenu.
Aliongeza
kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali wanaobainika na kufanya vitendo visivyofaa
katika jamii kama mauji ya watu wenye ulemavu,mauaji ya vikonge ,ubakaiji kwa watoto
wadogo na kuwalawiti.
‘’Kama watanazania
kupige vita dhidi ya vitendo hivo na sisi kama serikali tunaendelea kuchukua
hatua mbalimbali kwa yeyote anainika kuhusika na vitendo hivyo.Pia ninawaomba kusema
katika ngazi za familia,tuzungumze na watoto wetu dhidi ya athari zinazotokana
na Madawa ya kulevya pia tuendelee kuongeza katika ngazi za familia
ili tuweze kuwanusuru vijana wetu na Taifa kwa ujumla.
Akisoma
Risala ya kwaya kuu ya Mtakatifu Cesilia kwa Mgeni Rami.Mwalimu Mkuu wa kwaya
hiyo Pius Kalimsenga alisema kuwa toka kuanzishwa kwa kwaya hiyo mpaka
leo wamefanikiwa kurekodi DVD toleo la kwanza mwaka lenye jina ‘NATANGAZA
HADHARANI’ na toleo maalumu la Albamu ya nyimbo za pasaka iliyoratibiwa na
Baraza la maaskofu Tanzania (TEC) kwa kushirikiana na shirika la Utangazaji
Taifa (TBC) hivi karibuni, wamefanikiwa kufungua akaunti ya kwaya katika banki
ya wananchi Mufindi (MUCOBA).
wameongeza ari na imani kwa waumini
kupitia uimbaji wao, Kuongoza ibada mbalilmbali kwa nyimbo kila
tunapohitajika kufanya hivyo,wamefanya ziara mbalimbali ndani ya parokia na nje
ya Parokia kupitia michango ya waumini.
Kalimsenga alisema pamoja na mafanikio
hayo lakini wanakabiliwa na cganamoto mbalimbali ambazo zinapelekea kutosonga
mbele katika uinjilishaji, kama Ukosefu wa chombo cha usafiri kwa ajili ya
safari za uinjilishaji nje ya Parokia yetu,Mahudhurio hafifu ya waimbaji
kutokana na ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira,Wanakwaya kujiunga na kuacha
kwasababu ya kukimbia michango ya kutegemeza kwaya pamoja na Kukosa miradi
ambayo ingepunguza mzigo wa michango ambayo inasababisha wanakwaya kutodumu
katika uinjilishaji.
Ndugu Mgeni Rasmi,kwaya yetu ina malengo
yatakayoweza kutusaidai ili kuweza kujikwamua kutoka katika utegemezi ikiwa
pamoja na kupunguza michango inayochangishwa na waumini kwa ajili kutegemeza
kwaya zetu pale hasa pale kwaya zinapohitaji kusafiri kwenda kuinjilisha nje ya
parokia, ununuzi wa vyombo na kurekodi albamu mpya.. Baadhi ya malengo hayo ni
pamoja na Kuwa na usafiri wa basi ambalo litatuwezesha kusafiri maeneo mbalimbali
kwa ajili ya kufanya Uinjilishaji kama lisemavyo agizo la Bwana wetu Yesu “enendeni
ulimwenguni kote mkaihubiri Injili “ (Marko 16:15),Kuwa na miradi
midogomidogo ambayo itawawezesha wanakwaya kujikwamua kiuchumi ikiwa na
kuzalisha ajira kwa vijana ili kuendana kauri mbiu ya serikali yetu ya awamu ya
tano isemayo”Hapa kazi tu”.
‘’’Jumla ya mahitaji yetu kwa malengo yaliyotajwa hapo juu
yanakadiriwa kufikia shilingi za kitanzania Milioni Miamoja na kumi (110,000,000/=.Tunaamini
malengo haya yakitimia, kwaya itaweza kuondokana na utegemezi pamoja na michango
mikubwa kwa wanakwaya wenyewe’’Alisema Kalimsenga.
0 maoni:
Chapisha Maoni