Posted by Esta Malibiche on JUNE 23,2017 IN NEWS
Na
Esta Malibiche,Majira
Iringa
KANISA la kiinjili la kilutheri
Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa limempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.John Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ya kuwatumikia
watanzania kwa uadilifu mkubwa,hivyo kuwataka watanzania kuendelea kumpa ushirikiano na kumuombea.
Akizungumza na vyombo vya Habari ofisini kwake,Katibu
mkuu wa KKKT dayosisi ya Iringa Nayman Chavala alisema, hatua anazochukua
Mh.Rais zinatakiwa kupongezwa kwa vitendo hasa za kuwabana wasio waadilifu
pamoja na kupambana na wizi wa mchanga wa dhahabu (MAKINIKIA) ni hatua ya
kupongezwa kwani suala hilo lilikuwa likiwanufaisha wachache huku Taifa
likibaki patupu .
" Sisi kama kanisa tumekuwa
tukimuombea kila wakati tena kwa kumtaja kwa jina na hatutachoka kuendelea
kumuombea maana kazi anayoifanya ni ngumu ambayo silaha kubwa ni maombi
"Alisema Chavala
Aidha akizungumzia maandalizi ya
kumwingiza kazini askofu mteule Mchungaji Blaston Gavile na msaidizi wake
Mchungaji Himidi Saga alisema yamekamilika na yanatarajia kufanyika siku ya
jumapili tarehe 25,6,2017,Kuanzia saa tatu asubuhi kwenye viwanja vya shule ya Msingi Gangilonga Manispaa ya IOringa.
Alisema
ibada hiyo itaongozwa na askofu mkuu wa KKKT Dkt Frederick Shoo pamoja na
askofu mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella na kuwa kabla ya idaba kutakuwa na
maandamano ya wachungaji na washarika yatakayoanzia usharika wa kanisa kuu hadi
Gangilonga.
"
Tunaomba wananchi wote na washarika kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo
la kihistoria pia tunategemea kuwa na viongozi mbali mbali wa serikali na
wageni mashuhuri kutoka ndani na nje ya Tanzania"Alisema Chavala na
kusisitiza kuwa
Aliongeza
kuwa Askofu Gavile amechukua nafasi ya aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Dkt
Mdegella ambaye alistaafu kwa heshima kubwa na kuacha heshima ya aina yake
ndani ya KKKT .
0 maoni:
Chapisha Maoni