Posted by Esta Malibiche on JUNE 25,2017 IN NEWS
Vijana wa Marafiki Charity wakipeana majukumu kabla ya kuanza jukumu la kufuturisha watoto hao wa CHAKUWAMA.
Ebby
mwenye jezi nyeusi akiwatambulisha baadhi ya vijana wenzake wa Marafiki
Charity kwa mmoja wa walezi wa kituo cha CHAKUWAMA wakati walipowasili
hapo jana Juni 24.2017 katika tukio hilo la kuwafuturisha watoto hao
wanaolelewa kituoni hapo.
Baadhi
ya wanaumoja wa Marafiki Charity wakiwa kwenye pozi tofauti, akiwemo
Devotha, Leah Mushi aliyembeba mtoto Malaika Ebby, Munira Hussen, Esther
Namuhisa,na Pendo
Omary Mkambara akijadiliana jambo na Naamala katika tukio hilo la kufuturisha
Wakibadilishana mawazo wakati wakisubiria muda
Omary Mkambara akiwajibika katika tukio hilo
Wakisaidia kushusha futari maalum
Watoto
hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya
kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Watoto
hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya
kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Watoto
hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya
kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Watoto
hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya
kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Shughuli ya futari ikiendelea
Watoto
hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiendelea kujumuika
pamoja katika furai hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Marafiki Charity wakiendelea kutoa huduma katika tukio hilo
zoezi la futari likiendelea
Marafiki Charity wakijumuika pamoja katika kupata futari hiyo
Omari Mkambara na Emmanuel Makundi (kulia) wakitoa neno la shukrani kwa kituo hicho
Omary Mkambara akitoa neno la shukrani
Dua maalum kwa ajili ya tukio hilo
Mmoja wa wasimamizi katika kituo hicho akiwatambulisha Marafiki Charity kwa Mama mwanzilishi wa kituo hicho
Marafiki Charity wakimsikiliza Mama Mwanzilishi wa kituo hicho wakati walipofika kumjulia hali
Wakiuliza maswali mbalimbali juu ya kituo hicho cha CHAKUWAMA
Mama Mwanzilishi wa kituo cha CHAKUWAMA akiwaombea dua Marafiki Charity
Baadhi
ya Marafiki Charity wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kumaliza tukio la kufuturisha watoto wa kituo cha kulea watoto Yatima
cha CHAKUWAMA, tukio hilo limefanyika jana Juni 24.2017.
Asasi ya MARAFIKI CHARITY TZ Wafuturisha watoto Yatima Dar
Asasi
isiyo ya Kiserikali ya Marafiki Charity Tanzania ‘Marafiki Charity’,
kwa umoja wao jioni ya jana Juni 24. 2017, wameweza kujumuika kwa
pamoja katika tukio maalum la kufuturisha katika kituo cha kulea watoto
Yatima cha CHAKUWAMA.
Marafiki
hao waliweza kuandaa futari hiyo maalum na kwenda kujuika pamoja na
watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho cha CHAKUWAMA, chenye makazi yake
Sinza-Mori (CHAKUWAMA). Aidha wakitoa shukrani kwa niaba ya Asasi hiyo
ya Marafiki Emmanuel Makundi na Omary Mkambara walieleza kuwa, moja ya
shughuli waliokuwa wamepanga ni kufanikisha tukio hilo la kujumuika
pamoja na watoto hao ikiwa ni njia moja wapo ya kutoa sadaka jamii yenye
uhitaji.
“Tumeweza
kujumuika hapa kwa pamoja tukiwa Marafiki. Hii ni moja ya kuonesha
upendo, undugu, uelewano na hutu wetu kwa wenzetu wa kituo hichi cha
CHAKUWAMA.” Alieleza Makundi.
Kwa
upande wake, Omari Mkambara alieleza kuwa, huo ni mwanzo kwani
wamefurahia uwepo wao hapo wa kupata kufuturu pamoja hivyo ikiemo dua
walioombewa ni faraja kwa umoja wao huo.
Marafiki
Charity ni muunganiko wa marafiki kutoka kada mbalimbali, waandishi wa
Habari, wanasheria, wahandisi, wajasiriamali, wahasibu na watu
mbalimbali ambapo wanashirikiana na kwa pamoja katika kusaidia jamii
ikiwemo kufanya kazi kwa pamoja za kujitolea, kusaidia wasiojiweza,
kubadilishana mawazo na kujumuika pamoja katika mustakabali wa kuijenga
Tanzania.
0 maoni:
Chapisha Maoni