Postedby Esta Malibiche ob JUNE 27,2017 IN NEWS
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Januari Makamba akizungumza na wadau wa Mazingira Mkoani Iringa. |
Na Esta Malibiche
Iringa
SERIKALI imesikia kilio cha wabunge wa majimbo ya mkoa wa Iringa waliotaka wananchi wanaolima vinyungu katika mabonde yenye kuhifadhi unyevunyevu wasibuguziwe mpaka maamuzi ya pamoja yatakapofanyika.
Kwa nyakati tofauti katika bunge linaloendelea, wabunge wa mkoa wa Iringa waliungana na wabunge wa majimbo mengine nchini wakiitaka serikali isitishe mpango wa kuwaondoa wakulima katika maeneo hayo.
Wakiongozwa na Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi wabunge hao walitaka Serikali kusitisha zuio la kulima vinyungu mpaka tafsiri ya umbali wa mita 60 kutoka vyanzo vya maji itakapofafanuliwa ipasavyo.
Akizungumza na wadau wa Mazingira kutoa Halmashauri zote za mkoa wa Iringa katika kikao kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa IringaBi. Amina Masenza na Kilichofanyika jana MkoaniIringa,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Januari Makamba alisema kuwa zimejitokeza changamoto ya utekelezaji wa maelekezo ya kikosi kazi hicho kilichoundwa na Makamu wa Rais kwa lengo la kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu ambao vyanzo vyake vya maji vipo mkoani Iringa, Njombe na Mbeya.
Makamba alisema kuna bugudha zimejitokeza hasa kwa wakulima wa vinyungu wakati maelekezo hayo yakitekelezwa jambo lililolazimisha kifanyike kikao cha muafaka baina ya viongozi wenu na wataalamu wa wizara yangu.
Alitoa agizo kuwa kuanzia sasa mpaka watakapofikia maamuzi ya pamoja wananchi wanaolima katika maeneo hayo wasibughudhiwe lakini wasiruhusiwe kuingia maeneo mapya.Pia aliziagza halmashauri zote za mkoa wa Iringa zinatakiwa kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa maelekezo hayo, na ihakikishe miti yote isiyorafiki na vyanzo vya maji ikiwemo mikaratusi illiyopo katika vyanzo vya maji inakatwa.
‘’Katika kufikia maamuzi serikali itatembea mkoa mzima wa Iringa, kinyungu kwa kinyungu na bonde kwa bonde kabla ya kutoa maelekezo yatakayosaidia kwa nia njema kunusuru mazingira.’’Alisema Makamba
Kwa upande wao wabunge wa Mkoa wa Iringa, walitoa maoni yao baada ya tamko la Serikali kupitia waziri Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Mbune wa Jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa,alisema wananchi waliowengi wa mkoa wa Iringa wanategemea vinyungu ili kujikwamua kiuchumi,hivyo serikali imefanya busara kubwa kuhakikisha wakulima hawaadhiriki na pia Mazingira hayaathiiki kutokana na kilimo.
“Kilimo cha vinyungu kina tija kwa wananchi wengi wa jimbo la Kalenga na mkoa wa Iringa, kimebadili maisha ya watu wengi na kimewasaidia sana. Jambo la msingi tulime sambamba na kulinda mazingira yetu na vyanzo vya maji” alisema Mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa.
Naye Mbunge wa Mafinga Mjini Chumi alisema wakazi wa Iringa wanasifika kwa utunzaji wa mazingira, kinachotakiwa kufanywa ni kuelekezwa namna ya kutunza vyanzo vya maji bila kuathiri shughuli zao za uchumi.
Pamoja na Chumi na Mgimwa, wabunge wengine waliokuwepo wakati maelekezo hayo ya waziri yakitolewa ni Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto, Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa CCM, Rita Kabati na Mbunge wa Viti Maalum CCM Rose Tweve ,Nao waliosema kuwa tathimini ya kutosha inatakiwa kufanyika katika kilimo hicho.
0 maoni:
Chapisha Maoni