Jumanne, 6 Juni 2017

SILA JOHN MWANGU AWASHUKURU WATANZANIA KWA MICHANGO YAO,AMESAFIRISHWA LEO KWENDA MUHIMBILI KUPATA MATIBABU.

Posted by Esta Malibiche on JUNE 6,2017 IN KIJAMII

Hili ndilo gari la Wagonjwa lililombeba Sila John Mwangu kuelekea Hospital ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

 Zimepita  siku tatu toka mtandao huu wa Habari ulipomtembelea Sila John Mwagu nyumbani kwao baada ya kupata Taarifa kuwa anasumbuliwa na Fungus ya Ulimi,lakini alishindwa kwenda kutibiwa kutokana na kukosa fedha za matiababu,ndipo Mtandao huu wa Habari ulipogonga hodi nyumbani kwao eneo la Mwembetogwa Manispaa ya Iringa na kumkuta Sila pamoja na Mama yake Mazazi na  kuzungumza nao.
Mungu ni mwema baada ya taarifa kuwafikia watanzania kupitia mtandao huu wa habari,kwa kushirikina na Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela,Katibu wa Cahama cha Mapinduzi ccm Iringa Mjini,Magroup ya Whatsaap pamoja na  watanzania wote,hatimae leo Sila ameanza safari kutoka Iringa na kuelekea Muhimbili kwenda kutibiwa.
  Mtandao huu wa Habari unatoashukurni za dhati kwa   watanzania wote walioguswa kwa na  tatizo liliomkuta Sila na hatimae kutoa michango yao mara mlipopata taarifa ,Mungu awabariki sana na  waongezea mara dufu pale mlipopunguza na kumsaidia Sila kupata Matibabu hivyo kunusuru uhai wake.
Ndugu Mtanzania  Sila  bado anahitaji mchango wako  wa hali na mali ili aweweze kumudu gharama za matibabu yake,chakula,na gharama mbalimbali akiwa Hospitalini.
Tuendelee kumuombea aweze kupona haraka,pia bado anahitaji mchango wako wa hali na mali,kila mmoja atakavyoguswa.
Kama unachochote tafadhari mtumie Mama yake Mzazi  kwa namba hii...0768825554.
Mtandao huu wa Habri utaendelea kutoa taarifa kwa watanzania kama hapo awali kuhusu maendeleo ya Sila akiwa Hospitalini Muhimbili mapaka atakapotoka,hivyo basi endelea kufuatilia taarifa kupitia Blog yako hii ya KALI YA HABARI.

Sila John Mwangu akijaribu kuzungumza kwa Ishara   kupitia vyombo vya habari   akiwashukuru  Watanzania kwa  Michango yao ya hali na mali leo asubuhi  kabla ya kuanza safari kuelekea katika Hospital ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
Sila John Mwangu akijaribu kuzungumza na watanzania na kuwashukuru kwa Michango yao ya hali na mali leo asubuhi  kabla ya kuanza safari kuelekea katika Hospital ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
Sila John Mwangu akijaribu kuzungumza na watanzania na kuwashukuru kwa Michango yao ya hali na mali leo asubuhi  kabla ya kuanza safari kuelekea katika Hospital ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
Mama Mzazi wa Sila John Mwangu akizungumza leo asubuhi  kuwashukuru Watanzania kwa michango yao kabla ya kuanza safari kuelekea Muhimbili.Pia amewaomba Watanzania kuendelea kutoa michango yao ili Sila aweze kutibiwa na kurudi katika hgali yake ya kawaida.

Huyu ndiye sila John,anasumbuliwa na Ugonjwa wa Fungus ya Ulimi. Tuma chochote kwa namaba hii ya MAMA yake Mzazi ili kunusuru uhai wake.0768825554.

0 maoni:

Chapisha Maoni