Posted by Esta Malibiche on JUNE 17,2017 IN NEWS
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla pamoja na Mke wake wakiwasili katika Hotel ya Hyatty
Kilimanjaro alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na
Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania) jioni ya Juni
16.2017 Jijini Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla ameshiriki futari maalum iliyoandaliwa na Benki ya Biashara
Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania) iliyokuwa maalum kwa ajili ya
wadau na wateja wa benki hiyo, tukio lililofanyika katika Hotel ya
Hyatty Regency, Kilimanjaro ijini Dar es Salaam jioni ya Juni 16.2017.
Dkt.
Hamisi Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo,
aliimiza ushirikiano, Umoja na upendo kwa watanzania wote hasa katika
kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kwa
upande wao CBA Tanzania walibainisha kuwa, tukio hilo ni sehemu ya
kuboresha uhusiano na wateja na wadau wao. Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo
Dk.Gift Shoko alisema: “Tunampongeza Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kwa
kufika na kujumuika nasi katika tukio hili maalum la Iftar. Pia
tunawashukuru sana wateja wetu nchini kote kwa kuendelea kuiamini benki
yetu katika kupata bidhaa na huduma za kibenki na ndio maana
tunashirikiana nao sana katika maeneo maalum ambayo yanatukutanisha ili
pia tuweze kujadiliana na kuboresha ushirika wetu kama tunavyokutana leo
kwenye futari hii”. Alisema Dk. Shoko.
Dk.
Shoko aliahidi kuwa Benki itaendelea kuboresha bidhaa na huduma zake
ili ziendelee kuwa na ubora wa hali ya juu kabisa ikiwa ni pamoja na
kubuni huduma mbalimbali za kuwarahishia maisha wateja wanapohitaji
kupata huduma za kibenki na kuboresha shughuli zao.“Benki ya CBA
Tanzania tunawatakia mfungo mwema wa Ramadhani lakini pia maandalizi
mema ya sikukuu hapo baadae!,” alieleza.
CBA
Tanzania ni sehemu ya CBA Group iliyopo katika nchi za Kenya, Uganda na
Tanzania, CBA Tanzania ina matawi kumi na moja yaliyosambaa sehemu
mbalimbali nchini.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Huduma Binafsi wa Benki ya
Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania), Bw. Julius Ngonyani
alipowasili katika Hotel ya Hyatty Regency, Kilimanjaro alipokuwa mgeni
rasmi katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo Tawi la
Tanzania (CBA Tanzania) jioni ya Juni 16.2017 Jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA Tanzania, Gift Shoko.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Iftar
iliyoandaliwa na Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA
Tanzania) iliyofanyika katika Hotel ya Hyatty Regency, Kilimanjaro jioni
ya Juni 16.2017 Jijini Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla pamoja na Mke wake wakipata huduma ya chakula alipokuwa
mgeni rasmi katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya Biashara
Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania) jioni ya Juni 16.2017 Jijini Dar
es Salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kamal Steel, Bw.
Gupta (kushoto) walipokutana katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na
Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania) iliyofanyika
katika Hotel ya Hyatty Regency, Kilimanjaro jioni ya Juni 16.2017 Jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA Tanzania, Gift
Shoko.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akiteta jambo na mmoja wa wadau wa Benki ya Biashara Afrika
(CBA) wakati wa hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo Tawi la
Tanzania (CBA Tanzania) iliyofanyika katika Hotel ya Hyatty Regency,
Kilimanjaro jioni ya Juni 16.2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya menejimenti ya
Benki ya CBA mara baada ya kumaliza hafla ya Iftar iliyoandaliwa na
Benki ya hiyo jioni ya Juni 16.2017Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa CBA Tanzania, Gift Shoko.
0 maoni:
Chapisha Maoni