Posted by Esta Mal;ibiche on JUNE 30,2017 IN NEWS
Mwakilishi
kutoka Mtandao wa Kodi Tanzania (TTJC), Grace Masalakulangwa
akiwasilisha ripoti ya utafiti ya One Billion Question iliyotafitiwa na
shirika la ISCEJIE katika Mkutano uliowakutanisha wadau wa Elimu na
Wenyeviti wa Chama cha Walimu ngazi ya mikoa ya Tanzania Bara
iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Alistidia Kamugisha akifungua mkutano na
kuwaelezea malengo ya mkutano huo wa siku mbili kwa wadau wa elimu na
Chama cha Walimu Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue
Pearl jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Cathleen Sekwao akitoa mada
kuhusu umuhimu wa ukusanyaji wa rasilimali za ndani na kuwekeza katika
kuboresha sekta ya elimu hususani kwa mtoto wa kike na maslahi ya walimu
katika mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania
(CWT/TTU).
Meneja
Mradi wa Elimu kutoka shirika la ActionAid Tanzania Ndugu Karoli
Kadeghe akiwasilisha changamoto zinazoikabili elimu msingi hapa nchini
ikiwa ni pamoja na upungufu wa vyumba vya madarasa, upungufu wa walimu
kwenye mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu pamoja baadhi ya viongozi
wa Chama cha Walimu ngazi ya mikoa ya Tanzania Bara iliyofanyika jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania wakichangia mada kwenye
mkutano uliowakutanisha ili kujadili kodi na ubora wa elimu hapa nchini
Tanzania kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar
Shirika
la ActionAid-Tanzania, Mtandao wa Elimu Tanzania, Shirika la Maendeleo
ya Elimu Singida-MEDO na Mtandao wa Asasi za Kiraia-KINGONET kwa pamoja
wanatekeleza mradi wa uhamasishaji utoaji elimu bora kupitia rasilmali
zetu wenyewe ( PROMOTING QUALITY EDUCATION THROUGH PROGRESSIVE DOMESTIC
RESOURCE MOBILIZATION) unaotekelezwa huko Kilwa na Singida Vijijini kwa
ngazi ya wilaya kwa kufanya kazi na kamati za shule na klabu za haki za
watoto shuleni. Kitaifa MRADI Huo unalenga kufanya utetezi wa
mabadiliko ya kisera na sheria hasa suala la ulipaji kodi, ukusanyaji
kodi kwa haki (tax Justice), uzibaji wa mianya ya uvujaji wa kodi ili
makusanyo yaongezeke na yagharimie huduma bora kwa wananchi wa Tanzania
hususani kuboresha utoaji wa Elimu bora Nchini.
Mratibu
wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bi. Cathleen Sekwao akifungua mkutano huo
aligusia pia kuhusu “utoaji wa huduma za jamii hapa nchini unakabiliwa
na ufinyu wa fedha, wote tu mashahidi kuwa hadi kufikia mwezi Machi,
2017 serikali ilikuwa imetoa asilimia 34 tu ya bajeti yote ya 2016/2017.
Jambo hili lina madhara makubwa katika utoaji wa huduma za jamii hasa
elimu msingi yenye ubora hasakwa mtoto wa kike”.
Aliongelea
pia serikali kushindwa kutoa asilimia mia moja ya fedha za kutekeleza
bajeti ya 2016/2017 tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza fedha
nyingi kupitia misamaha ya kodi.
Meneja
Mradi wa Elimu kutoka shirika la ActionAid Tanzania Ndugu Karoli
Kadeghe aliwasilisha changamoto zinazoikabili elimu msingi hapa nchini
ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa vyumba vya madarasa, Upungufu wa ofisi
za walimu, Upungufu wa vyoo vya wanafunzi,Uwiano usiokubalika kitaratibu
wa mwalimu na wanafunzi, Shule nyingine kukosa kabisa walimu wa kike.
Upungufu
wa nyumba za walimu, fedha za ruzuku zisizotosheleza, utegemezi wa
bajeti ya nchi za nje unaoathiri pia bajeti ya elimu na kusababisha
Serikali kushindwa kugharimia kiufanisi utoaji wa elimu, mgawanyo wa
ruzuku usiozingatia mahitaji halisi ya wenye uhitaji maalumu, jinsia na
mahitaji ya kijiografia na pia shule changa na zile ambazo ni kongwe,
Kuwa na mipango ya kibaguzi-Shule inayofanya vizuri ndiyo inapewa
fedha(payment for results- P4R) kutoka mpango wa BRN bila kujali mizania
ya usawa wa mazingira kati ya shule na shule, Kukosekana kwa mafunzo
kazini kwa walimu, Kutopandishwa madaraja walimu, Kutolipwa kwa wakati
stahiki za walimu wanaohamishwa/kustaafu mfano pesa ya usafiri.
Mratibu
wa Inter Faith Standing Committee Bi. Grace Masalakulangwa aliwasilisha
kuhusu Utafiti wa Ripoti ya “1 Billion Question” iliyojikita kubaini
upotevu wa kodi katika sekta ya madini au uziduaji katika wilaya za
Kilwa, Tarime na Geita. Utafiti huo umebaini serikali inapoteza
takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia
misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata
utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za
ukwepaji kodi.
Washiriki
mbalimbali wakichangia katika mkutano huo, walishauri serikali
kuboresha ukusanyaji wa kodi na utengaji wa bajeti katika sekta ya
maendeleo hususani sekta ya elimu. Baadhi ya washiriki walichangia pia
kukosekana kwa ufanisi na maendeleo yenye tija katika sekta ya Elimu
kutokana na usimamizi mbovu wa elimu, serikali kushindwa kuwekeza katika
elimu, kuwepo kwa wizara mbili zinazosimamia elimu na muda mwingine
kuingiliana kwa majukumu pamoja na kutozingatiwa katika maslahi ya
walimu.
0 maoni:
Chapisha Maoni