Alhamisi, 22 Juni 2017

RIDHIWANI KIKWETE:TUMEJIPANGA KUHAKIKISHA HALMASHAURI YA CHALINZE INAJIWEZESHA YENYEWE

Posted by Esta Malibiche on JUNE 23,2017 in NEWS



Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli akifungua  kiwanda kikubwa cha Matunda kilichopo Chalinze Mkoani Pwani.


Na Afisa Habari
  Ofisi ya Mbunge-Chalinze

Mbunge wa Chalinze kupitia chama cha Mapinduzi Ccm,Ridhiwani Kikwete,ameshiriki Ziara ya Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanazania Dr.John Magufuli katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
MH.Rais Magufuli akiwa wilayani humo,alifungua Kiwanda kikubwa cha  matunda cha Sayona kilichopo Mboga Wilayani Chalinze.
Mh.Rais  akiwa katika jimbo Chalinze, Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi Ccm  Ridhiwani Kikwete alimuhakikishia Mheshimiwa Rais juu kuwa ataendelea kumuunga mkono katika hatua mbalimbali anazochukua ikiwemo kupambana na Rushwa, Ufisadi na kuwahakikishiaWatanzania  wananufaika na rasilimali zilizopo Nchini .
Ridhiwani  alimweleza Mh.Rais  juu ya jitihada ambazo Wana chalinze wanazifanya ili kujikomboa katika Uchumi tegemezi ikiwa ni pamojana  jinsi Halmashauri ya Chalinze ilivyofanikiwa kukusanya fedha kwa kuvuka kiwango cha makusanyo.
" Mh. Rais Halmashauri yako hii ya Chalinze imefanikiwa kukusanya zaidi ya Asilimia 102 juu ya makadirio mbayo tulikuwa tumejipangia. Fedha hizi zitapelekwa katika miradi ya maendeleo ambayo inagusa wananchi wa chini kabisa ikiwemo kuimarisha huduma za afya, maendeleo ya jamii, mikopo kwa wakina mama na vijana pia miradi ya maji "Alisema Ridhiwani na kuongeza kuwa

"Mh. Raisi , tumejipanga  kuhakikisha kuwa halmashauri yetu inajiwezesha yenyewe,ambapo kiasi cha zaidi ya Milioni 200 zimetolewa kwa ajili ya kuwakopesha wananchi wenye kipato cha chini ili waweze kujishughulisha na shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato na hatimae kujikwamua kiuchumi""" Alisema Ridhiwani.
Aidha Mbunge huyo alimuomba  Rais kuitumia Chalinze kama sehemu ya ushuhuda wa hatua na jitihada anazochukua kukuza uchumi wa watu na maendeleo ya kweli yanayotazama uelekeo wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Ccmi na ahadi zake.
Mh.Rais kama kuna mtu ambaye ana shaka na utayari wako pamoja na uchapakazi wako juu ya sera ya viwanda basi Mwambie aje Chalinze ili  aje kuona jinsi mambo yanavyofanyika."
 MH.Rais alimshukuru Mbunge na akampongeza kwa kumfananisha na Baba yakealiyewahi kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete. ""Ridhiwani wewe ni Nyoka mtoto .Nimekuona na ninakupongeza kwa jinsi  unavyochapa kazi na kuhakikisha unawaletea wananchi wako maendeleo Hongera sana.hivyo basi ninapenda kuwaambia ndugu zangu wana Chalinse kuwa hakika nimemsikia Mbunge wenu na nimeridhika na utendaji wake,sisi sote ni mashahidi tumeona anavyofanya juhudi kutatua kero za wanaChalinze,hakika  Nyoka huzaa Nyoka".Alisema Mh.Rais.
 Aidha Mh.Rais aliikabidhi Halmashauri ya Chalinze majengo ambayo yalitumiwa na Mkandarasi pale Msata wakati wa Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia-Masata.
Hata hivyo baada ya kuzungumza na wananchi wa Chalize,Mh.Rais alielekea Bagamoyo ambako alifanya mambo mawili makubwa ikiwemo uzinduZi wa Barabara ya Bagamoyo Msata na Kiwanda cha kukausha Matunda kilichopo Mapinga, Bagamoyo.
Mbunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ccm,Ridhiwani kikwete akibkufungua adirishana mawazo na Mh.Rais wakati wakielekea katika ufunguzi  wa Kiwanda
  
Mbunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ccm,Ridhiwani Kikwete akipanda mti,mara baada ya
Mbunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ccm,Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi wa Jimbo lake la Chalinze   

Mbunge wa Jimbo la Chalinse kupitia Chama cha Mapinduzi Ccm Ridhiwani Kikwete,akiagana na Mh.Rais wa Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika Jimbo la Chalinze.

0 maoni:

Chapisha Maoni