Posted by Esta Malibiche on JUNE 5,2017 IN NEWS
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,
Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa
mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na matenki ya
kuhifadhi maji katika Jimbo la Chalinze. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Chalinze, Mhandisi Christer
Mdomba, kulia ni Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest
Ndikilo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi
Evarest Ndikilo akizungumza wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya
mradi wa ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza maji safi kutoka
mto Wami pamoja na matenki ya kuhifadhi maji katika Jimbo la Chalinze.
Kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge,kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi
wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwangingo (Kulia) akitoa maelezo ya
utekelezaji wa mradi kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na
matenki ya kuhifadhi maji katika Jimbo la Chalinze.
Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwan
Kikwete (Kulia) akiteta Jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Majid
Mwanga Wakati wa hafla hiyo.
Moja ya tenki la maji linalojengwa katika chanzo cha maji cha mto Ruvu ikiwa ni sehemu ya mradi huo.
Mbunge wa Jimbo la
ChalinzeChalinze, Mhe. Ridhiwan Kikwete akimshukuru Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge kwa hatua nzuri iliyofikiwa katika
utekelezaji wa mradi huo.
Mafundi wakiendelea na maandalizi ya ujenzi wa matenki yakuhifadhi maji katika chanzo cha maji Ruvu.
(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)
……………………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Takriban wakazi 234,398 wa
Chalinze watanufaika na mradi wa upanuzi wa mtambo na ujenzi wa mfumo
wa kusafirisha na kusambaza maji safi pamoja na matenki ya kuhifadhi
unaolenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wake katika Jimbo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri
Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya kukagua maendeleo ya
mradi huo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge
amesema kuwa Serikali inaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo
na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi katika kutekeleza mradi huo.
“Dhamira ya Serikali ni
kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama ndio maana
tumeweka wataalamu wetu hapa kumsimamia mkandarasi ili afanye kazi kwa
ubora na kwa kasi kama ambavyo Waziri Mkuu aliagiza alipotembelea mradi
huu mwezi Machi mwaka huu”, alisisitiza Lwenge.
Akifafanua, Mhandisi Lwenge
amesema kuwa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo awamu ya
tatu ni ulazaji wa mabomba ya kusafirisha na ya kusambaza maji, ujenzi
wa matanki 19, na ujenzi wa mtambo wa kusafishia maji ambao unaendelea.
Kazi nyingine zinazoendelea
katika kutekeleza mradi huo ni ujenzi wa vituo 351 vya kuchotea maji
ambapo vituo 27 vimekamilika,vituo 226 vipo katika hatua mbalimbali na
vituo 98 havijaanza kujengwa.
Akizungumzia hatua
zinazochukuliwa na mkandarasi wa mradi huo, Mhandisi Lwenge amesema kuwa
ni kuongezeka kwa upatikanaji wa vifaa kwa wakati katika eneo la mradi,
kuongeza wafanyakazi na maeneo ya kazi na kuteua mwakilishi wa kampuni
anayeweza kutoa maamuzi kwa niaba ya kampuni inayotekeleza mradi.
Aidha, Waziri Lwenge amesema kuwa
Serikali itatoa ufumbuzi wa changamoto ya wananchi wa Jimbo hilo
kulipia malipo ya huduma (service charge) hata pale wanapokuwa
hawajapata huduma hiyo ili kuwe na utaratibu mzuri unaowezesha wananchi
kulipia huduma pale wanapotumia tu na si vinginevyo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo
hilo, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema yeye binafsi anaishukuru Serikali
ya Awamu ya Tano kwa namna inavyoshughulikia changamoto zinazowakabili
wananchi wa Jimbo hilo ikiwemo ya maji.
“Naridhika na hatua iliyofikiwa
katika utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya mradi huo ambao ukikamilika
utasidia kwa kiwango kikubwa kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji
katika jimbo hili hivyo wananchi wataweza kuongeza kasi katika shughuli
za maendeleo”, alisisitiza Ridhiwani.
Akifafanua amesema anaunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo .
Mnamo mwezi Machi mwaka huu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kutembelea mradi huo na
kukagua shughuli za ujenzi wa miundombinu ya mradi huo Awamu ya Tatu
na baada ya ziara aliagiza mkandarasi anayetekeleza mradi huo ambaye ni Overseas Infrastracture Alliance (OIA)Pv Ltd
kutoka India mwenye ubia na Kampuni ya Pratibha Industries nayo ya
India kukamilisha kazi hiyo ,mkandarasi wa mradi huo ameshalipwa
shilingi 38,716,375,627 ikiwa ni asilimia 42 ya gharama ya mradi.Uhaba wa maji safi na salama umelikumba jimbo la Chalinze kwa kipindi kirefu. Kwa sasa wanaopata huduma ya maji safi na salama ni 220,241, mradi ukikamilika, watakaopata huduma hiyo watafikia jumla ya 234,394.
0 maoni:
Chapisha Maoni