Posted by Esta Malibiche on JUNE 19,2017 IN NEWS
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika tukio hilo la
kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini,
Mh. Koka
Dk. Kigwangalla ampongeza Mbunge wa Kibaha Mjini, Mh. Koka kwa kuchangia vifaa tiba
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla amekabidhi jumla ya vifaa 831 vyenye thamani ya jumla ya
Shilingi milioni 400, kwa kituo cha Afya Mkoani Kibaha Mjini, vifaa
vilivyotolewa na Mbunge wa jimbo hilo, Mh. Silvestry Koka.
Awali
kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa
kukagua maeneo ya majengo ya Kituo hicho cha Afya huku akbaini mambo
mbalimbali aliyoagiza yafanyiwe kazi ili kituo hicho kiweze kuwa
Hospitali ya Wilaya pindi itakapokamilisha vigezo
Wakati
wa kukabidhi vifaa hivyo, Dk. Kigwangalla alipongeza juhudi za Mh. Koka
kwa kujali wananchi wake kwani hadi kuweza kupata vifaa hivyo aliweza
kutumia maarifa na ukaribu wake na wananchi wake hivyo kufika kwa vifaa
hivyo vitakuwa faraja kubwa kwa Wanakibaha na wananchi wote wa maeneo
jirani.
“Nampongeza
Mbunge Koka kwa kuwaletea vifaa hivi. Kwani ni vizuri na vitakuwa
msaada mkubwa kwa wananchi wa Kibaha na maeneo yake ya jirani.
Nakupongeza sana sana” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa tukio hilo la kukabidhi vifaa hivyo.
Aidha,
aliwataka wananchi wa Kibaha mjini waweze kuwa karibu na Mbunge wao na
wamwamini kwani anawajali ndio maana anawatumikia kwa kila njia ikiwemo
kuwaletea maendeleo kwa ujumla.
Kwa
upande wake, Mbunge wa Kibaha Mjini Mh. Silvestry Koka amemshukuru
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kwa kuweza kufika na kujionea Kituo hicho
sambamba na kukabidhi vifaa huku akimuomba kuendelea kufika mara kwa
mara kujionea mipango ya Afya jimboni humo.
“Leo
hiii najisikia faraja kwa vifaa hivi kuweza kufika hapa jimboni kwangu
kutoka nchini Marekani. Nawaomba vitumike kwa uangalifu mkubwa sana na
viweze kuwa msaada kwetu” alieleza Mh. Koka.
Awali
alieleza kuwa, kiasi cha shilingi milioni 32 fedha zilizotolewa na
Halmshauri ya mji wa Kibaha ziweza kusaidia usafirishaji wa vifaa hivyo
kutoka nchini Marekani huku yeye kama Mbunge akitumia gharama ya
shilingi milioni 12 kwa ajili ya kuwaleta wataalam kwa ajili ya ukaguzi
na kuvifunga vifaa hivyo.
Mbunge
huyo ameeleza kuwa, vifaa hivyo vitagawia katika zahanati na vituo
vyote vilivyopo mjini Kibaha na maeneo mengine yenye uhitaji.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza katika tukio hilo la
kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini,
Mh. Koka
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akikabidhia nyaraka zenye vifaa tiba akikabidhiwa na
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Mh. Koka
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akikabidhi nyaraka yenye idadi ya vitu hivyo vya vifaa tiba
kwa uongozi wa Kituo cha Afya Mkoani Kibaha Mjin wakati wa tukio hilo
la kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha
Mjini, Mh. Koka
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akishuhudia vitu hivyo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la
Kibaha Mjini, Mh. Koka
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha wakati wa
tukio hilo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla kisalimiana na na uongozi wa Mkoa na Wilaya ya Kibaha
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni kwa ofisi ya Wilaya ya Kibaha
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya Madiwani wa Jimbo la Kibaha Mjini
Baadhi ya vifaa tiba vilivyokabodhiwa leo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akifanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya kituo cha Afya
Mkoani
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akikagua eneo la mahabara katika kituo cha Afya Mkoani,
Kibaha Mjini
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akikagua eneo la Chumba cha Upasuaji katika kituo cha Afya
Mkoani, Kibaha Mjini
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa na mbunge wa jimbo hilo
Wakiangalia vifaa hivyo
Mbunge wa Kibaha Mjini Mh. Koka akielezea namna vifaa hivyo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi
Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na baadhi ya watendahi wa
Hospitali ya Mkoa, Kituo cha Afya Mkoani na Mganga Mkuu wa Mkoa
0 maoni:
Chapisha Maoni