Posted by Esta Malibiche on JUNE 30,2017 IN MICHEZO,
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (kulia)akizungumza pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa
Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini
kwake Mjini Dodoma. wa pili kulia ni Mwenyeji na kiongozi wa Msafara
Bishop Oscar John.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (katikati) akimsikiliza Mheshimiwa William Ngeleja akizungumza
wakati Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED
STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (kulia)akimsikiliza Bishop Oscar John (aliesimama) akizungumza,
pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE
UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Chama cha Msalaba
Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha
(katikati) na Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo (kushoto)
uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa
Medali za Dhahabu katika Mashindano ya kimataifa ya Mazingira na Sayansi
yaliyofanyika hivi karibuni nchini Marekani. Kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa Shule ya Wavulana ya Feza Ndg. Ibrahim Rashid, anaefuata
ni Ndg. Rashid Kikwete, kulia ni Mhe. Hawa Ghasia, wa pili kulia ni Ndg.
Kassi Nkamia na watatu kulia ni Ndg. Abdallah Rubeya, waliotembelea leo
Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni
kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama
hicho Ndg. Mwadini Jecha (kushoto waliokaa) baada ya kikao
kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson (kulia) akimsikiliza Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu
Tanzania Ndg. Mwadini Jecha (katikati) pale ugeni kutoka Chama hicho
ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kushoto ni Mratibu wa
Mawasiliano Ndg. Anne kilimo.
0 maoni:
Chapisha Maoni