Jumapili, 25 Juni 2017

MAELFU YA WANANCHI MKOANI IRINGA WAJITOKEZA KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI

Posted by Esta Malibiche on JUNE 25,2017 IN NEWS

Wananchi wa Mkoa wa Iringa wakiwa kwenye maandamano ya kumpongeza Mh.Rais wa Jmuhuri ya Muungano wa Tanazania Dkt.John Pombe Magufuli.PICHA NA ESTA MALIBICHE
 



Na Esta Malibiche
Iringa
WANANCHI Mkoani Iringa wamejitokeza kwa wingi kumpongeza Mha. Rais wa Jamuhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli hapo jana katika viwanja vya mwembe togwa Manispaa ya Iringa.
Awali pongezi hizo zilianza na maandamano makubwa kutoka katika viwanja vya Bustani ya Manispaa ya Iringa na kuelekea katika viwanja vya Mwembetogwa ,ambapo mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza alipokea Maandamano hayo,nakufuatiwa na salamu mbalimbali za pongezi kutoka wananchi wa mkoa wa Iringa,wakimpongeza Mh.Rais  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotolewa na wananchi,Viongozi wa dini,vyama vya saiasa,vyuo vikuu,Serikali na asasi zisizo za kiserikali.
Salamu hizo zilitolewa kutokana na utendaji kazi mzuri wa Mh. Rais na Serikali yake tote,huku wananchi wakimuombea Afya njema ili aweze kuendelea kuwatumikia na hivyo kuifanya Tanazania kuwa Mpya.
Hata hivyo mada kutoka vyuo vikuu vilivyopo Mkoani Iringa Zilitolewa ,Pamoja na vikundi mbalimbali vya sanaa vilitumbuiza kupamba pongezi hizo.
 


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza akizungumza ana mael;fu ya wananchi waliojitokeza kumpongeza Rais Magufuli katika viwanja vya Mwembetogwa  Manispaa ya Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamuhuri Davidi Willium akitoa salamu za wilaya ya kilolo, za kumpongeza  Rais Magufuli katika viwanja vya Mwembetogwa  Manispaa ya Iringa.

 Mkuu wa wilaya ya Kilolo Bi.Asia Abdallah akitoa salamu za wilaya ya kilolo, za kumpongeza  Rais Magufuli katika viwanja vya Mwembetogwa  Manispaa ya Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  akitoa salamu za wilaya ya kilolo, za kumpongeza  Rais Magufuli katika viwanja vya Mwembetogwa  Manispaa ya Iringa.

Katibu wa chama cha Mpainduzi ccn Mkoa wa Iringa,akitoa salamu za pongezi kwa Mh.Rais John Pombe Magufuli kwa niaba ya wanaccm Mkoa wa Iringa.

Mbunge wa viti malum Mkoa wa Iringa,kupitia chama cha Mapinduzi ccm Ritha Kabati akitoa salamu zaker za pongezi kwa Mh.Rais.
Katibu wa umoja wa Vijana CCM Iringa Mjini akitoa salam za pongezi kwa Mh.Rais




















0 maoni:

Chapisha Maoni