Posted by Esta Malibiche on JUNE 30,2017 IN KITAIFA
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2017 Ndg Amour Hamad Amour
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2017 Ndg
Amour Hamad Amour afurahishwa na kusifu mshikamano ulipo kati ya
viongozi na wananchi katika Wilaya ya Ikungi Jambo ambalo limepelekea
kutekeleza vyema miradi ya Mandeleo.
Mwenge wa Uhuru ukiwa umepata mapokezi makubwa ya wananchi
waliojitokeza kuulaki umekimbizwa umbali wa Kilomita 77.9 ambapo umezuru
Miradi yenye Jumla ya shilingi 2,417,184,466.72
Kati ya fedha hizo Wananchi wamechangia Shilingi
239,500,000/= ambapo Halmshauri ya wilaya ya Ikungi imechangia Shilingi
22,500,000/=, Serikali kuu imechangia 2,003,359,466.72 huku wahisani
wakiwa wamechangia shilingi 151,500,000/=
Akizungumzia Uwepo wa Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amewapongeza wakazi wa
Wilaya hiyo kwa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru uliowasili
Katika Wilaya hiyo Leo Alhamisi June 29, 2017 katika Kijiji cha Mkiwa,
Kata ya Mkiwa ukitokea katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Mhe Mtaturu amesema kuwa Jumla ya Miradi tisa imetembelewa
na Mwenge wa Uhuru ambayo ni miradi ya Sekta ya elimu, Afya, kilimo,
Maendeleo ya Jamii, Biashara, Viwanda na Utawala.
Miradi itakayozinduliwa ni pamoja na Programu ya Kilimo cha
Korosho, Madarasa ya Shule ya Sekondari Mkiwa pamoja na matundu 10 ya
vyoo vya shule hiyo.
Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg Amour
Hamad Amour ameweka Jiwe la msingi ujenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ikungi, Jiwe la msingi Zahanati ya Kijiji cha Ulyampiti sambamba na
kugawa vyandarua ili kujikinga na Malaria na kuweka Jiwe la msingi
kiwanda cha Mwananchi Cha kukamua Mafuta ya Alizeti sambamba na kufungua
klabu ya wapinga Rushwa katika shule ya Sekondari Ikungi.
Mhe Mtaturu amesema kuwa Wilaya ya Ikungi inaunga mkono
kauli mbiu ya mwaka huu 2017 ya Shiriki ukuzaji wa uchumi wa viwanda kwa
maendeleo ya nchi yetu.
Mkesha wa Mwenge wa Uhuru umefanyika katika viwanja vya
shule ya Msingi Puma, Kijiji cha Puma ambapo pia umetembelea vikundi vya
vijana na wanawake vya kiuchumi ambavyo vimewezeshwa na Halmashauri ya
Wilaya ya Ikungi kupitia mapato ya ndani, sambamba na Kuwapatia kadi za
Bima ya Afya waathirika wa Virusi Vya UKIMWI na UKIMWI.
Aidha, June 30, 2017 Mwenge wa Uhuru Utaelekea Manispaa ya Singida ambapo utakabidhiwa katika Kijiji cha Unyamikumbi.
Share:
0 maoni:
Chapisha Maoni