Posted by Esta Malibiche on JUNE 17,2017 IN NEWS
N a Esta
Malibiche
Iringa
JAMII imetakiwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na
vitendo vya unyanyasaji ikiwemo ubakaji, ulawiti kwa watoto
wadogo ili waweze kufikishwa katika
vyombo vya sheria.
Kilio hicho
kimetolewa jana na watoto wa Mkoa wa Iringa katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto
wa Afrika yaliyofanyika katika kijiji cha Kising’a kata ya Kising’a Tarafa ya Isimani Mkoani
Iringa,iliyo hudhuriwa na viongozi wa serikali,dini, vyama vya siasa na asasi
zisizo za kiserikali.
Akisoma Risala ya watoto katika maadhimisho hayo, ,Elizabeth Mhaso ambae ni mwanafunzi wa
shule ya Msingi Ilambilole iliyopo katika Halamsahauri ya Iringa, alisema
kuwa kutokana na kauli mbiu ya mwaka
2017 inayosema ‘’Maendeleo endelevu 2013;Imarisha ulinzi na fursa sawa kwa
watoto’’ ujumbe huu unawataka wazazi,walezi,serikali na jamii kwa ujumla kuimarisha ulinzi na usalama kwa watoto
sambamab na kuwapatia watot wa kike na kiume
pamoja na watoto walemavu fursa sawa katika Nyanja za Elimu,kiutamaduni na
kiuchumi.
Mhaso
alisema swala la ulinzi na usalama kwa watoto linahitaji msukumo mkubwa katika
jaamii nzima kwasababu kumekuwa kukitokea matukio ya unyanyasaji,ulawiti,ubakaji,utekaji
na ukatili kwa watoto lakini jambo la kusikitisha
na kushangaza familia zimekuwa zikifanya mapatano ya kificho na kumalizana wao
kwa wao pasipo kuzifikisha katika vyombo vya sheria.,hivyo jitihada za makusudi
zinahitajika katika kuelimisha jamii ili kuwafichua wale wanaojihusisha na vitendo
hivyo.
‘’’Ndugu Mgeni
Rasmi,Tunaomba Taifa letu lijikite katika kuimarisha familia zetu ili ziweze
kuwajibika kikamilifu katika kuweka mikakati ya kutuendeleza watoto kwa
kutulinda na kutupatia fursa sawa katika Elimu bora pamoja na kutupatia haki ya kuishi katika mazingira salama,Afya
bora,Chakula,Malazi,Kulindwa,Kusilizwa na kushirikishwa.Pia juhudi za makusudi zifanyike ili kujenga
uelewa kwa familia zetu kutumia fursa sawa kwa watoto bila kujali jinsi ya
mtoto na hali ya maumbile ya mtoto’’’’’’Alisema Mahaso.
Alisema
Familia ambayo ni msingi wa maisha na yenye
jukumu la malezi,makuzi na ulinzi wa Mtoto imeonekana kulegalega katika kutoa
Fursa sawa kwa watoto kwani baadhi ya wazazi wamejengea tafsiri potofu za
kutokumwendeleza mtoto wa kike na kuona kwamba yeye ni wa kuolewa tu,hivyo
kufifisha ndoto za maendeleo ya watoto wa kike.
‘’’Ndugu
Mgeni Rasmi,sisi watoto tunasikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya
wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuona baadhi
ya watoto wenye ulemavu wakiachwa bila
kupelekwa shule na wengine kufichwa kabisa ndani wasionekane katika jamii,hivyo
kupoteza fursa mbalimbali ambazo watoto walemavu wangeweza kuzipata na kuwa na
mchango katika maendeleo ya Nchi.Pia kuna baadhi ya wazazi wamekuwa imani potofu ya kuwa mtoto wa kiume
anastahili kuchunga na kulinda mifugo ya familia,hivyo kufifisha ndoto za
maendeleo ya watoto wa kiume pia imeombwa kuongeza nguvu kupambana dhidi ya waoto unaofanyika
majumbani,Shuleni na katika jamii kwa ujumla’’’’Alisisitiza Mhaso.
Aidha katika
maadhimisho hayo,Mgeni Rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamuhuri
Davidi Willium aliyemuwakilisha mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza,akitoa
hotuba yake alisema kuwa pamoja na juhudi za serikali
kuandaa Sheria,Sera,Miongozo na mkakati mbalimbali ya kumjali mtoto,kumekuwepo na
changamoto zinakazo kwamisha utekelezaji
wa programu za kumwendeleza,kumjenga mtoto wa kike na kulinda haki zake.
Jamhuri
alisema changamoto hizo nipamoja na ukosefu wa rasilimali fedha,ushiriki mdogo
wa jamii katika kuatatua tatizo la uvunjaji wa haki za watoto,na uelewa mdogo
wa jamii kuhusu haki za watoto.Kwa hali hiyo,umuhimu wa swala la ushiriki wa
watoto katika kufanya maamuzi yanoayohusu maisha yao upewe kipaumbele ili sauti
zao ziweze kusikika na mchango wao uonekane katika kutekeleza haki zao.
‘’’’Sote ni
walezi wa familia ,niawaombe tuungane kwa pamoja kukemea vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia hususani ubakaji na ulawiti dhidi ya watoto ambao
umeendelea kujitokeza katika mkoa wetu.Kibaya zaidi unyanyasaji huu umekuwa
ukiwahusisha watu wazima na watoto
wadogo,hivyo daima tuhakikishe usalama wa watoto wetu unaimarika kikamilifu katika kuwalinda na kuwahakikishia
usalama wa maisha yao kwa kutoa ushahidi
ili waototo waweze kupata haki zao.
Alisema Madhara
ya vitendo vya ubakaji katika jamii ni pamoja
na wahanga wa vitendo hivi kupata athari za kisaikolojia kama kutokujiamini,kuwa
na wasisawasi, kutokuwa na furaha kutokana na matokeo ya vitendo hivyo,ugumba ,mimba
za utotoni na kuharibu mahusiano baina ya wanajamii.
‘’’’Vitendo
hivi viovu vinadidimiza sana jitihada za Mkoa wa Iringa za kupambana na
maambukizi ya virusi vya Ukimwi na Ugonjwa wa ukimwi.Tafadharini wanaume na
wanawake wote tuungane kwa pamoja tupaze sauti ili kukabiliana na changamoto
hii kwa manufaa ya Taifa zima.’’’’Alisema Jamuhuri.
Alisema
juhudi za kuanzisha mabaraza ya watoto katika Mkoa wa Iringa zinaendelea,ambapo
Halmashauri ya Iringa imeshaanza kwa kuunda mabaraza ya watoto katika kata 22
ambayo yanafanya kazi nzuri ya kutetea haki za watoto ukilinganisha na
Halmashauri zingine za Mkoa wa Iringa ambazo zimeunda mabaraza machache.Pia
aliwaagiza wakurugenzi wote washirikiane na wakuu wa wilaya amabo Halmashauri
zao hazijakamilisha uundwaji wa mabaraza
ya watoto katika ngazi zote kwa mujibu
wa serikali wahakikishe mabaraza hayo
yanaundwa haraka iwezekanavyo.
‘’’Kwa hali
ilivyo sasa,ushiriki wa watoto katika kufanya maamuzi ya masuala yanayohusu
maisha yao ni suala linalotiliwa makazo sana Nchini Tanzania hasa baada ya
kuridhia makataba wa haki za watoto mwaka 1991,baada ya hapo Serikali iliona
umuhimu wa ushiriki wa watoto katika kufanya maaamuzi
mbalimbalinkwa utaratibu rasmi na wenye muendelezo mzuri hasa baada ya tukio la
ushiriki wa watoto katika kikao maalum
kilichoandaliwa na umoja wa Mataifa cha mwaka 2002 na hivyo kupendekeza uwepo wa chombo mahususi cha
kitaifa cha uwakilishi wa kudumu wa watoto
chini ya usimamizi wa wizara ya maendeleo ya Jamii ,Jinsia na watoto’’’’Alisema
Jamuhuri.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali Mkaoni Iringa wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Kijiji cha Kising'a Halmashauri ya Iringa Mkaoni Iringa |
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali Mkaoni Iringa wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Kijiji cha Kising'a Halmashauri ya Iringa Mkaoni Iringa. |
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali Mkaoni Iringa wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Kijiji cha Kising'a Halmashauri ya Iringa Mkaoni Iringa |
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali Mkaoni Iringa wakiwa katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Kijiji cha Kising'a Halmashauri ya Iringa Mkaoni Iringa. |
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamuhuri David Willum akimkabidhi hati maalum mwakilishi wa Radio Maria Jimbo Katoliki la Iringa Thobias Augustino Myovela. |
Mgeni Rasmi na Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na vikundi vya sanaa. |
Mgeni Rasmi na Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na vikundi vya sanaa. |
Mgeni Rasmi na Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoa shule mbalimbali walioshiki katia maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika |
Mgeni Rasmi na Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja washindi waliopata tuzo ya Maalum. |
Mgeni Rasmi na Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja washindi waliopata tuzoMaalum. |
0 maoni:
Chapisha Maoni