Ijumaa, 2 Juni 2017

SILA JOHN MWAGU AWAOMBA WATANZANIA WAJITOKEZE KUNUSURU UHAI WAKE

 Posted by Esta Malibiche on JUNE2,2017  in KIJAMI


Huyu kijana anaitwa Sila john Mwagu. Anaishi eneo la Mwembetogwa Manispaa ya  Iringa,anasumbuliwa na Fungus ya Ulimi.Mwezi wa pili mwaka huu alipelekwa Hospital ya Rufaa Iringa kwa ajili ya matibabu,baadae alipewa rufaa kwenda  Muhimbiri kkwa ajili ya matibabu zaiadi.Kutokana na familia kutokuwa na pesa toka mwezi wa pili hadi leo hii Sila bado yupo nyumbani na hali yake inaendelea kuwa mbaya kama mnavyomuona. Zaidi ya Mill.2 zinahitajika ili aweze kutibiwa.Kama mnavyomuona kwenye picha yupo nyumbani kwao Mwembetogwa hapa Mnispaa ya Iringa.Mimi kama Mwandishi wa Habari na mmiliki wa mtandao huu wa Habari nikiwa sehemu ya jamii,nilipopata taarifa nilimtembelea nyumbani kwao kumjulia hali na kunzungumza na Mzazi wake.anahitaji msaada wako mtanzania ili Sila aweze kwenda kutibiwa na hatimae kuokoa uhai wake kabla wadudu hawajaanza kusambaa mwilini..Kwa chochote utakachoguswa mtumie mama yake Mzazi kwa namba 0768825554.


0 maoni:

Chapisha Maoni