Posted by Esta Malibiche on Oct 31,2017 IN NEWS
MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Ritta Kabati akizungumza na kamati ya shule na wazazi hawapo pichani,kwenye kikao cha uchangiaji vifaa kwa ajili ya ukarabati wa shule ya Msingi Igeleke iliyopo Mnispaa ya Iringa,ambayo inakabiliwa na uchakavu wa majengo.PICHA NA ESTA MALIBICHE.
Na Esta Malibiche
IRINGA
MBUNGE wa Viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha Mapinduzi CCM Ritha kabati ameendelea na mpango wake wa kukarabati shule za Msingi kongwe zilizochakaa zilizopo Manispaa ya Iringa,ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira yanayostahili.
Akizungumza na wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Igeleke iliyoko kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa wakati akihamasisha uchangiaji wa vifaa vya ujenzi ili kukarabati majengo ya Shule hiyo yaliyochakaa,alisema ni aibu kwa shule kongwe kama hiyo kuwa miundo mbinu mibovu ambayo inawafanya wanafunzi kukaa kwa wasi wasi,hivyo aliwataka wazazi kuwekeza katika Elimu kwa kuchangia ili watoto waweze kusoma katika Mazingira rafiki na yanayostahili.
Ninawaomba Wazazi tuwarithishe watoto katikaElimu na siyo mali,mtoto akipata Elimu ataweza kujipangia nini cha kufanya na siyo mkurithisha mtoto mali.Mali bila Elimu ni sawa na bure.Elimu kwa mtoto ni muhimu sana kuliko kitu chochote,kwa kutambua hilo ninawaomba wa Elimu tuwekeze katika Elimu"Alisema Kabati.
Aidha Katika kikao hicho,wazazi walitoa mchango wa vifaa mbalimbali ikiwa nipamoja na Cement mifuko 33,Kokoto ndoo 17,Misumari kg13 na fedha kiasi cha Tsh.56950,vifa hivyo vilitolewa na wazazi ambapo mbunge alichangia mifuko 100 ya Saruji na pamoja na Singboard 100
''Sisi sote ni mashuhuda,watoto wetu wanasoma katika mazimgira magumu ambayo hayastahili,hali inayopelekea kutofanya vizuri katika masomo yao.Baada ya kuliona hilo,nikaweka mpango mkakati wa kuhakikiasha shule kongwe chakavu zinakarabatiwa kwa kushieikiana na wazazi pamoja na wadau wa Elimu""Alisema Kabati.
Kabati alisema shule hiyo licha ya kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani majengo yake hayaendani kabisa na hali halisi ya ufaulu wa wanafunzi hivyo kwa kushirikiana na wazazi ambao wamechangia vitu mbalimbali ukarabati wa shule hiyo utaanza jumamosi wiki hii.
“ Nimetembelea shule nyingi mkoani kwetu hasa za msingi kuweza kuangalia miundo mbinu na majengo yake kwa kweli hali inatisha na majengo mengi yamekuwa chakavu hivyo nitajitahidi kwa kushirikiana na wadau wa elimu kuweza kukarabati yaendane na hali ya sasa ya kuwa bora zaidi” alisema
Aliongeza kuwa shule ya Igeleke ni moja ya shule zinazofanya vizuri katika mitihani yake lakini imeharika hovyo na inahitaji msaada wa haraka kuikarabati kwa kuwa wanafunzi wanasoma katika mazingira magumu na kudumisha elimu ya wanafunzi hao waendelee kuongoza mkoani hapa.
Hadi sasa mbunge huyo amekwisha fanya ukarabati kwa shule za msingi za Azimio, Kihesa,Mtwivira na shule ya Kibwabwa ambazo alizitembelea na kubaini uchakavu mkubwa wa majengo na miundo mbinu mibaya na shule nyingine alizoahidi kuzifanyia ukarabati ni shule ya msingi Gangilonga.
Peter Kyando mmoja wa wazazi alimshukuru Mbunge huyo kwa niaba ya wazazi huku akiwataka wadau wa Elimu kujitoa kuchangia vifaa mbalimbali ili zoezi la ukarabati liweze kukamilika kwa wakati ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki.
Tunamshukuru Mbunge kwa kuona umuhimu wa Elimu,na kujitoa kukarababti majengo ya madarasa yaliyochakaa.Tuanaghitaji na wadau wengine waje,kwasababu bado vifaa vinahitajika ili kukamilisha.
MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Ritta Kabati akizungumza na kamati ya shule na wazazi hawapo pichani,kwenye kikao cha uchangiaji vifaa kwa ajili ya ukarabati wa shule ya Msingi Igeleke iliyopo Mnispaa ya Iringa,ambayo inakabiliwa na uchakavu wa majengo.PICHA NA ESTA MALIBICHE.