Jumanne, 17 Aprili 2018

MAVUNDE AMWAGA NEEMA KWA WAJISIRIAMALI DODOMA,AWATAKA WACHANGAMKIE FURSA

Posted by Esta Malibiche on  April 16 IN NEWS

Mbunge wa Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapimduzi CCM Anthony Mavunde akizungumza na wajasiliamali  leo hii Mjini Dodoma.


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Peter Mavunde ameahidi kuwapatia vikundi vya wajasiriamali mafunzo ya UJASIRIAMALI na kuviwezesha vikundi katika kata zote 41 zilizopo Jimbo la Dodoma Mjini.

Mavunde ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Cavillam wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Ujasiriamali yaliyowashirikisha zaidi ya wajasiriamali 2000 kutoka viunga mbalimbali vya Manispaa ya Dodoma,ambapo mafunzo hayo sasa yataanza kutolewa kwa kila kata  ili kuhakikisha idadi kubwa zaidi ya wajasiriamali inafikiwa na kupata mafunzo haya yenye lengo la kumuandaa mjasiriamali wa Dodoma kupata ujuzi wa utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.

Aidha Mavunde amewataka wajasiriamali hao kutumia fursa za ujio wa shughuli za Serikali Mjini Dodoma kama sehemu ya kukuza uchumi wao na kujiletea maendeleo binafsi.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo hayo,Mkurugenzi wa Taasisi ya *MJASIRIAMALI KWANZA* Dr Mujungu amamshukuru Mbunge Mavunde kwa udhamini wa mafunzo hayo na pia kumpongeza kwa kugawa mashine ndogo ndogo zenye thamani ya **Tsh 55,000,000 **kwa Vikundi vya Wajasiriamali katika kata 31 za Manispaa ya Dodoma.








0 maoni:

Chapisha Maoni