Posted by Esta Malibiche on April 27,2018 IN MICHEZO
Wachezaji wa timu ya kamba ya wanawake ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wakiongozwa na Neema Mbuja (wa kwanza mbele) wakicheza na RAS Iringa, katika mchezo wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mlandege mkoani Iringa, hata hivyo Tanesco walivutwa kwa mivuto 2-0. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
Washindi wa pili wa michuano ya Mei Mosi timu ya wanawake ya Uchukuzi wakimalizia mchezo wao kwa kuwavuta Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro jana kwa kuwavuta mivuto 2-0. Mchezo ulifanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mlandege. (Picha na Bahati Mollel wa TAA) .
Mchezaji
Warda Sapali (mwenye mpira) wa timu ya RAS Iringa) akimrushia mfungaji wao
Zitaamanzia Kididi (GA aliyenyoosha mkono juu) huku Mary Kajigiri (C ) wa
Uchukuzi akitafuta mbinu za kuupokonya mpira huo katika mchezo wa netiboli wa
michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha
Katoliki Iringa (RUCU), ambapo Uchukuzi walishinda kwa magoli 31-17. (Picha na
Bahati Mollel wa TAA).
: Mlinzi Subira Jumanne (WA) wa Uchukuzi akidaka vyema mpira uliorushwa na Zaituni Magiga (hayupo pichani) huku Ester Turuka (C ) wa RAS Iringa akitaka kutibua katika mchezo wa netiboli uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU), ambapo Uchukuzi walishinda magoli 31-17. (Picha na Bahati Mollel wa TAA
Mfungaji tegemeo wa timu ya Uchukuzi, Matalena Mhagama (mwenye mpira) akimrushia mfungaji mwenzake Bahati Herman (GS kulia) akimtoka mlinzi Zaujath Mdemu (GK) wa RAS Iringa katika mchezo wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki Iringa (RUCU), ambapo Uchukuzi waliibuka washindi kwa magoli 31-17. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
Mchezaji Mwadawa Hamis (aliyenyoosha kidole) wa Uchukuzi akiwaelekeza wenzake jinsi ya kuendelea kufanya vyema wakati wa mapumziko wa mchezo wa netiboli wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki Iringa (RUCU), ambapo Uchukuzi walishinda kwa magoli 31-17. (Picha na Bahati Mollel wa TAA).
TIMU
za Ofisi ya Rais Ikulu na Uchukuzi zitaamua bingwa wa mchezo wa netiboli wa
michuano ya Kombe la Mei Mosi inayofanyika mkoani Iringa, baada kushinda mechi
zao tatu kila mmoja na kujikusanyia pointi sita.
Hata
hivyo, Ikulu ambao ndio mabingwa watetezi wamewazidi Uchukuzi kwa kujikusanyia
magoli 159 na kufungwa 12, wakati Uchukuzi wamefunga 130 na kufungwa 33, ambapo
mchezo wao unaotabiriwa kuwa mkali utakaofanyika keshokutwa kwenye uwanja wa
Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU).
Katika
mchezo wa netiboli uliochezwa jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki
(RUCU), timu ya Uchukuzi iliwachapa RAS Iringa kwa magoli 31-17. Washindi
walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 14-7, ambapo wafungaji wake
Matalena Mhagama alifunga magoli 26 na Bahati Herman kafunga magoli matano.
Hadi
sasa Uchukuzi imeshatwaa vikombe vya ubingwa wa baiskeli kwa wanawake na
wanaume, huku kamba wanawake wametwaa ushindi wa pili. Bingwa wa kamba wanawake
ni RAS Iringa.
Katika
hatua nyingine timu ya Tumbaku ya Morogoro jana iliwafunga Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro kwa magoli 5-0 katika mchezo wa soka uliofanyika kwenye uwanja wa
Samora mkoani Iringa.
Washindi
ambao tayari wametinga hatua ya nusu fainali kutoka kundi ‘A’ walipata bao lao
la kwanza katika dakika ya 14 kupitria kwa Kelvin Makamba, huku Salum Idd
akifunga bao la pili katika dakika ya 16.
Mshambuliaji
Salum Idd aliongeza bao la tatu katika dakika ya 21, na Makamba alipachika bao
la nne katika dakika 45 na Ramadhani Silegondo alifunga hesabu kwa bao la tano
dakika ya 51.
Katika
mchezo wa kuvuta kamba wanaume uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi
Mlandege, timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) waliwavuta Ofisi ya
Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAO) kwa mvuto 1-0; nao Uchukuzi wanawake
waliwavuta NCAA kwa mivuto 2-0.
Michuano
hiyo itaendelea leo mchezo wa riadha wanawake kilometa nane na wanaume kilometa
10.
0 maoni:
Chapisha Maoni