Posted by Esta Malibiche on April 25,2018 IN MICHEZO
Mfungaji Ester Turuka (GA-orange katikati) wa RAS Iringa akijaribu kuwania mpira na Cecy Kanza (WD) Tanesco katika mchezo wa michuano ya Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki Iringa (RUCU). RAS Iringa walishinda kwa magoli 27-14
Mlinzi Jacky Sanga (mwenye mpira) wa Tanesco akitafuta wa kumrushia katika mchezo wa michuano ya Kombe la Mei Mosi kwa mchezo wa netiboli dhidi ya RAS Iringa uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki Iringa (RUCU).
Beki George Mlelwa wa timu ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAO) akipiga mpira mbele ya Andrew Kunambi (mwenye jezi ya njano mbele) wa Uchukuzi katika mchezo wa michuano ya Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora, ambapo Uchukuzi walishinda kwa magoli 3-1.
Mchezaji Erick Mpunga wa Uchukuzi (kulia) akijaribu kuzuia mpira unaotaka kupigwa na Kassim Mdee wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAO) katika mchezo wa mpira wa miguu wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Daktari wa timu ya Uchukuzi, Hawa Senkoro (kushoto) akimchua misuli mchezaji wake Kassim Sabu aliyebanwa na misuli katika mchezo wa soka wa michuano ya Kombe la Mei Mosi dhidi ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAO) uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora, ambapo Uchukuzi walishinda kwa magoli 3-1.
Wachezaji wa timu ya wanawake ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kulia wakiongozwa na Neema Mbuja wakiwavuta wenzao wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) jana kwenye michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika uwanja wa Samora. Tanesco walishinda kwa mivuto 2-0.
Wachezaji wa michezo mbalimbali ya Klabu ya Uchukuzi wakishingilia mara baada ya mchezo wa soka wa michuano ya Kombe la Mei Mosi dhidi ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAO) kumalizika kwa ushindi wa magoli 3-1 kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Na
Esta Malibiche
Iringa
TIMU
za soka za Uchukuzi na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zilizopo kundi ‘A’
na ‘B’ zinakaribia kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mei Mosi baada
ya jana kushinda michezo ya iliyofanyika kwenye uwanja wa Samora, ambapo kila
mmoja zinaongoza kundi lake kwa kujikusanyia pointi sita.
Uchukuzi
inafuatiwa na mabingwa watetezi Geita Gold Mine (GGM) wenye pointi mbili, NAO
na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yenye pointi moja kila mmoja; wakati
Tanesco inafuatiwa na Tumbaku nayo inapointi sita lakini imezidiwa magoli ya
kufunga, huku RAS Iringa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa hawana
pointi.
Katika
mechi hizo za jana Uchukuzi waliwafunga Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu
(NAO) kwa magoli 3-1. Nao ndio walikuwa wa kwanza kupachika bao katika dakika
ya 45 kupitia kwa Peter Dihoko aliyeunganisha kona ya George Mlelwa.
Uchukuzi
walisawazisha katika dakika ya 60 kupitia wa Kado Nyoni, huku bao la pili
lilifungwa na Omary Kitambo dakika ya 63 na bao la tatu dakika ya 68
lililofungwa na Issack Ibrahim.
Nao
Tanesco waliwachapa RAS Iringa kwa magoli 4-0, ambapo matatu yaliyofungwa na
Kurwa Mangara katika dakika ya 19, 34 na 59 huku Salehe Bakari alifunga bao la
nne dakika ya 66.
Katika
mchezo wa netiboli timu ya RAS Iringa iliwafunga Tanesco kwa magoli 27-14.
Washindi walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 9-7. Nayo Ikulu walipewa
ushindi wa mezani wa magoki 40 na pointi mbili baada ya Malaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA) kushindwa kufika uwanjani Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU) kwa
kuwa na majeruhi wengi waliotokana na kuvuta kamba.
Katika
mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake timu ya Uchukuzi ilivutwa na RAS Iringa 1-0
baada ya mvuto wa awali kutoka sare;
huku kwa upande wa wanaume wa Uchukuzi waliwavuta Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi wa Hesabu (NAO) kwa mivuto 2-0.
Michezo
mingine ya kamba wanawake walivutwa na MUHAS mivuto 2-0; nayo NAO waliwavuta
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mvuto 1-0 kwa upande wa wanaume.
Michuano
hiyo inaendelea leo kwa upande wa netiboli timu ya Uchukuzi itacheza na RAS
Iringa uwanja wa RUCU; huku katika soka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
watgakuna na Tumbaku ya Morogoro, na GGM watacheza na Uchukuzi kwenye uwanja wa
Samora; wakati katika kamba RAS Iringa kuumana na Tanesco kwa wanawake.
0 maoni:
Chapisha Maoni