Jumanne, 3 Aprili 2018

MASOGANGE AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 3

Posted by Esta Malibiche on April 3,2018 in NEWS.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kwa kosa la kutumia madawa ya kulevya aina ya  heroin.
Msanii huyo alikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Februari 15, 2017, akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.
Masogange alikuwa miongoni mwa watu maarufu waliotajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati akipambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya.

0 maoni:

Chapisha Maoni