Jumatatu, 2 Aprili 2018

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KITUO CHA RADA, APOKEA NDEGE YA TATU YA BOMBADIER

Posted by Esta Malibiche on April 2,2018 IN KITAIFA



9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono na kushukuru  wakati akiingia katika ndege hiyo mpya ya Bombardier Q400 iliyowasili kutoka nchini Canada

1
Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere huku ikipewa heshma ya  kumwagiwa maji(water salute) mara baada ya kutua.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli watatu kutoka kulia, pamoja na viongozi mbalimbali wa dini, viongozi wa Serikali wakipiga makofi wakati wakiipokea Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
4
Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 ikiwa imeegeshwa  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, viongozi mbalimbali wa dini na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ndege Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere..
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono marubani wawili waliokuja na ndege hiyo mpya.
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi mfumo wa usimikaji wa Rada katika viwanja vinne vya ndege (Mwalimu Julius Nyerere-Dar es Salaam, Mwanza, KIA-Kilimanjaro na Songwe katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
1314
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mwanamuziki wa Bongo flavor Naseeb Abdul-Diamond platinum mara baada ya kuweka jiwe la msingi mfumo wa usimikaji wa Rada katika viwanja vinne vya ndege (Mwalimu Julius Nyerere-Dar es Salaam, Mwanza, KIA-Kilimanjaro na Songwe katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU











0 maoni:

Chapisha Maoni