Posted by Esta Malibiche on April 3,2018 in MICHEZO
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na
Utawala wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bw. Makwaia Makani
akizungumza kwenye tafrija ya kuwaaga wachezaji wa Timu ya Michezo ya
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), timu ya Wizara ya Afya Zanzibar,
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) baada ya timu hizo kushiriki
tamasha la Michezo ya Pasaka 2018.
Baadhi ya wachezaji na wafanyakazi
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakimsikiliza Mkurugezi wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bw. Makani wakati akizungumza nao.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo
cha Utafiti- Zanzibar, Hamisi Rashidi Mohamed akizungumza kwenye
tafrija ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Wizara ya Afya Zanzibar na Timu
ya Michezo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na
Utawala katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bw. Makwaia Makani na
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Utafiti- Zanzibar, Hamisi Rashidi
Mohamed akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu hizo baada ya
kumalizika kwa tafrija hiyo.
………………
Serikali imesema itaendelea kuboresha michezo sehemu za kazi ili kuifanya iwe endelevu na kuwawezesha watumishi wengi kushiriki.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu-Kitengo cha Utafiti Zanzibar,
Hamisi Rashid Mohamed wakati alipokua akizungumza katika hafla ya
kufunga tamasha la michezo ya Pasaka 2018, iliyoshirikisha timu za
michezo kutoka Wizara ya afya Zanzibar, Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) , Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) pamoja na Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Amesema
michezo hiyo ni ya muda mrefu ilianzishwa mwaka 1972 na kwamba hakuna
budi kuindeleza na kuiboresha zaidi ili kuleta hamasa kwa wanamichezo wa
taasisi hizo kushiriki kwa wingi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala Bw. Makwaia Makani
ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru
amesema ushiriki wa michezo ni jambo zuri kwani inawaepusha vijana
kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa.
Amesisitiza
mipango iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kuhakikisha
michezo hiyo inaboreshwa na kutoa fursa kwa watumishi wengi kushiriki.
‘’Hospitali
ya Taifa Muhimbili inaipa kipaumbele michezo na nina ahidi kwamba
mapungufu yote yaliyopo tutayafanyia kazi kikamilifu na michezo hii
tutaendelea kuiboresha,’’ amesema Mkurugenzi Makani.
Tamasha
la michezo ya Pasaka lilianza Machi 30, 2018 na kumalizika Aprili 2 ,
2018 likihusisha mchezo wa mpira wa miguu ,pete pamoja na kuvuta kamba .
Tamasha hilo mwakani litafanyika Visiwani Zanzibar.
0 maoni:
Chapisha Maoni