Jumamosi, 14 Aprili 2018

MTOTO MUDASILI AWALILIA WATANZANIA WANUSURU UHAI WAKE

Posted by Esta Malibiche ON April 14,2018 IN NEWS

 Mtoto Mdasili Mwenye Umri wa Miaka Miwili anaesumbuliwa na Saratani ya Jicho.
Mama Mzazi wa Mudasili,BiHadija Said ambae ni mkazi wa kijiji cha Nampemba Wilayani NAchingwea Mkoani Lindi akimnyonyesha Mtoto wake Mudasili anaesumbuliwa na Saratani ya jicho.
Bi.Hadija Saidi Mkazi wa Kijiji cha Nampemba Wilayani Nachingwea Mkoa wa Lindi amewataka watanzania  kujitolea matibabu  ili waweze kunusuru Uhai wa Mtoto wake.
Ombi hilo amelitoa mapema leo hii wakati akizungumza na Mtando huu wa Habari  ulipomtembelea kijijini hapo mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi.
 Bi.Hadija alisema kuwa Mtoto MUDASILI amezaliwa Septemba 2016 katika kijiji cha Nampemba wilayani Nachingwea mkoani Lindi ambae anasumbuliwa na tatizo la uvimbe katika jicho la kushoto.
Akizungumzia namna tatizo la Ugonjwa wa mtoto wake lilivyoanza   alisema kuwa  

"Mwaka jana mtoto alianza kujiwasha jicho hili,hali ambayo ilinilazimu kwenda hospital huku jicho la mtoto likiwa jekundu mithiri ya damu''
Tulipewa dawa tukarejea nyumbani,hata hivyo hazikusaidia.

Kadiri siku zilivyosonga hali jicho la mtoto ilizidi kuwa mbaya,hali iliyopelekea jicho kutokea kwa nje kama unavyoona tukaenda Ndanda nako tukaambiwa tuende Nyangao.
Siku chache baadae tulipewa rufaa ya kwenda Muhimbili huko ambako tuliambiwa mtoto ana SARATANI ambayo imeenea mwiilini,hivyo turejee nyumbani hakuna tiba mbadala zaidi ya kupata dawa za kupunguza maumivu tu.
Alisema kuwa hali ilivyozidi kuwa mbaya baba wa mtoto alimkana kutokumtambua mtoto wake na kuondoa mahusianokabisa kwa mama yake.
Hali ya uvimbe imeingia hadi ndani ya koo,hali hii inamsababishia Mudasili kutoweza kula chakula kigumu na kuhitaji hakula laini na kunywa madawa ya kukata maumivu "PAIN KILLER" na dawa za kupambana na wadudu kwenye jeraha.
 KALI YA HABARI  blog inawaomba watanzia kukumtazama kila mmo aweze kuguswa  kumsaidia mtoto huyu anepata maumivu makali na mateso kutokana na ugonjwa unaomsumili aweze kupata matibabu na hivyo kupona kabisa.
Hii ni namba ya Bi HADIJA SAIDI Mama yake Mzazi 0654197916 (Namba hii imesajiliwa kwa jina la kiume ni vema ukipiga ujiridhishe)kwa ambao watapata nafasi ya kumtembelea mtoto huyu basi wawasiliane na Mzazi wake kwa namba hiyo hiyo ili kupata mwelekeo namna ya kufika Nyumbani kwake.




0 maoni:

Chapisha Maoni