Posted by Esta Malibiche on April 25,2018 IN MICHEZO
Wachezaji wa mchezo wa baiskeli wakiwa tayari kuanza mbio hizo za kilometa 20 kwa wanawake na wanaume katika mchezo michuano ya Kombe la Mei Mosi inayoendelea kwenye mkoa wa Iringa.
Bingwa wa mchezo wa baiskeli kwa wanaume, Chaptele Muhumba (aliyenyoosha mkono) wa Uchukuzi akiwa na wasindikizaji wake mara baada ya kumaliza mbio za kilometa 20 zilizoanzia eneo la Mizani Ndolela mkoani Iringa, ikiwa ni michezo wa kombe la Mei Mosi inayoendelea mkoani hapa. Mshindi alitumia dakika
Mlinzi Jacky Sanga (WD) wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akijitahidi kuzuia mpira uliorushwa na Fatuma Fusi (WA) wa Ikulu katika mchezo wa netiboli wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU) mkoani Iringa. Ikulu wameshinda kwa magoli 70-4.
Mfungaji Caltace Manampo (GA) wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akidaka mpira uliorushwa na Pendo Rungu (WA-njano) huku Restituta Karani (WD) na Lilian Sylidion (GD) wote wa Ikulu wakijaribu kutibua harakati za mfungaji huyo katika mchezo swa netiboli wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki Iringa (RUCU).
Winga Pendo Rungu (aliyeina na mpira) wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akitafuta njia ya kupasia mpira mfungaji wake Imelda Hengo (GS-njano) huku Chuki George (mwenye ribbon ya njano kichwani) wa Ikulu akijaribu kukwapua mpira huo katika mchezo wa netiboli wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU).
Bingwa wa wanawake wa mbio za baiskeli, Scolastica
Hasiri (mwenye kofia ngumu) akiwa na viongozi na wachezaji wa michezo
mbalimbali wa timu yake ya Uchukuzi baada ya kuibuka mshindi katika michuano ya
Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwa kushindanishwa kilometa 20. Scolastica
alitumia muda wa dakika 53:44
.
Wachezaji na viongozi wa michezo mbalimbali ya timu ya Uchukuzi wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi kwa upande wa wanaume, Chaptele Muhumba (aliyevaa kofia nyeusi katikati), baada ya kuibuka mshindi kwa kutumia dakika 32:18 katika michuano ya kombe la Mei Mosi inayoendelea mkoani Iringa.
Na
Esta Malibiche
Iringa
TIMU
ya Uchukuzi imetwaa ubingwa wa mchezo wa baiskeli wa kilometa 20 kwa wanawake
na wanaume baada ya wachezaji wake Chaptele Muhumba na Scolastica Hasiri
kuibuka washindi, katika michuano ya Kombe la Mei Mosi inayoendelea mkoani
Iringa.
Mbio
hizo zilizoanzia eneo la mizani Ndolela na kuishia FFU, ambapo Muhumba
alimaliza baada ya kutumia muda wa dakika 32:18; huku Scolastica akimaliza kwa
dakika 53:44.
Ushindi
wa pili kwa wanaume ulichukuliwa na Nehemia Jonnas wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) aliyemaliza kwa muda wa dakika 41:44 na mshindi wa tatu ni
Stanley Umbe wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa dakika 46:51.
Aliyeshika nafasi ya nne ni Roman Steven wa MUHAS aliyetumia saa 1:12.40 na wa
mwisho ni John Fataki wa Ikulu.
Kwa
upande wa wanawake mshindi wa pili Happy Mwanga wa Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) alitumia mida wa saa 1:23.33 na wa tatu ni Severina Mnyaga wa MUHAS alitumia
muda wa saa 1:38.00.
Katika
mchezo wa netiboli timu ya Ikulu iliwaadhibu Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) kwa kuwafunga magoli 70-4 katika mchezo uliofanyika jana kwenye
uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCU).
Washindi
walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 33-2. Mfungaji Fatuma Machenga wa
Ikulu ndio aliyefunga magoli yote 70, huku kwa upande wa Tanesco yamefungwa na
Imelda Hango.
Katika
mchezo wa soka nao ulifanyika jana kwenye uwanja wa Samora, mabingwa watetezi
timu ya Geita Gold Mine (GGM) wameendelea kugawana pointi na wapinzani wao
ambapo wamelazimishwa sare na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya bao 1-1.
GGM
ndio walikuwa wa kwanza kupachika bao katika dakika ya 27 lililofungwa na
Mohamed Salum, lakini TRA wakasawazisha kwa njia ya penalti kupitia kwa
Boniface Emmanuel katika dakika ya 52.
Wakati
huo huo, michuano hiyo ya Mei Mosi yenye kaulimbiu “Tanzania ya Viwanda Swadakta… kwa
ukuzaji wa ajira sambamba na uhamasishaji wa michezo kazini”,
inafunguliwa rasmi leo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza, ambapo
zaidi ya timu 12 zinashiriki katika michezo ya netiboli, soka, karata, bao,
draft, baiskeli na riadha.
0 maoni:
Chapisha Maoni