Jumamosi, 7 Aprili 2018

MBARAZA UVCCM DAR AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA VIJANA KATA YA BUGURUNI..

Posted by Esta Malibiche on April 7,2018 IN SIASA

 Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM kupitia Mkoa wa Dar es salaam *Ndg. Gwantwa Alex Mwakijungu* leo hii ameshiriki ufunguzi wa semina elekezi kwa viongozi wa kata na matawi ya Kata ya Buguruni ambayo imeratibiwa na uongozi wa Kata hiyo chini ya Mwenyekiti wao *Ndg. Mwandike* kama njia ya kuelekezana namna mbalimbali za uendeshwaji wa shughuli za Jumuiya ya Vijana kulingana na matakwa na miongozo ya Chama na Jumuiya.

Katika risala iliyosomwa kwa mgeni rasmi na jumuiya hiyo ngazi ya Kata,viongozi wa kata hiyo wamewasilisha ombi la kuwezeshwa kuanzishiwa mradi wa steshionari ili kusaidia katika uendeshaji wa shughuli za Jumuiya ya Vijana. Jambo ambalo *Ndg.Gwantwa Alex M.* ameahidi kuwasaidia *kompyuta 2* (Desktops) kama mchango wake katika kufanikisha azma yao hiyo.

*Ndg. Mwakijungu* pamoja na mambo mengine aligusia yafuatayo kama wosia wake kwa vijana Kata ya Buguruni.

1. *JUU YA KUJIWEKA KARIBU NA SERIKALI...*

"Serikali inapofanya mambo makubwa ya Kimaendeleo nchini watu wa kwanza kuyajua,  kuyajuzungumzia na kuyatetea ni sisi Vijana wa CCM na sio kuzubaa kusubiri kuzisikia kwenye Taarifa za Habari nyakati Usiku. UVCCM tuweni Updated".

2. *JUU YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA..*

"Mbinu za Ushindi haziwezi kufanana kwa Mkoa wote,mbinu za Msongola lazima ziwe tofauti na za hapa Buguruni. Ni lazima basi Vijana tujiongeze tuwe na mbinu mbadala kuelekea Uchaguzi Serikali za Mitaa 2019"

3. *UVCCM NA MAENEO YANAYOTAWALIWA NA UPINZANI..*

"Vijana tuishio kwenye Mitaa, Kata na Majimbo yanayoongozwa na Vyama vya Upinzani ni lazima tujikomboe, Tuitafute Dola yetu kwani hakuna amani katika kuwa mpinzani wakati nguvu ya kushinda tunayo,nia ya dhati tunayo na sababu za kushinda tunazo tele..." aliongoze *Ndg. Mwakijungu.*

Katika semina hiyo Mbaraza UVCCM Dar es salaam aliongozana na viongozi wengine wa Jumuiya wakiwemo *Ndg. Thobias Omega* Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa kupitia Mkoa wa Njombe, *Ndg. Nyansio Dismass Gregory*, mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM kupitia Mkoa wa Rukwa na *Ndg. Muhamed Mringo*,Mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya ya Temeke.









0 maoni:

Chapisha Maoni