Jumamosi, 21 Aprili 2018

LIPULI FC 1-1 SIMBA SC, ADAM SALAMBA AENDELEZA UBABE

Posted by Esta Malibiche on April 21,2018 IN MICHEZO

Mchezaji wa Lipuli Fc Adam Salamba akipokea hundi ya sh. millioni moja


Salamba akipokea king'amuzi cha Azam



Bench la Ufundi la Simba wakishuhudia Mpambano

Mashabiki wa Simba wakishangilia mpambano


Simba wakishambulia lango la Lipuli

Mashabiki wa Lipuli Fc wakishangilia bao lililofungwa na Adam Salamba


Timu ya Lipuli Fc imelazimishwa sare nyumbani na Simba Sc ya 1-1 katika Dimba la uwanja wa Samora mjini Iringa.

Simba walionekana kupooza kipindi cha kwanza ambapo walilazimishwa na mashambulizi ya Timu ya Lipuli kufika golini kwao.

Mchezaji bora wa Lipuli wa Mwezi machi Adam Salamba akadhihirisha ubora wake kwa kuweza kupachika bao dk ya 31 ya mchezo katika kipindi cha Kwanza cha mchezo na kufanya lipuli kuongoza kipindi cha kwanza hadi kinamalizika.

Kipindi cha Pili Simba walirudi katika hali tofauti na kuanza kushambulia kwa nguvu na kulazimisha mashuti kufika katika lango la Lipuli na hadi kufikia dk ya 66 Laudit Mavugo akaisawazishia Simba.

Dakika 90 zikamalizika na timu hizo zote mbili zikitoka sare ya kufungana bao 1-1  

0 maoni:

Chapisha Maoni