• TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

Ester Malibiche

Kali ya habari

  • Nyumbani
View post on imgur.com

Ijumaa, 20 Aprili 2018

SERIKALI YAANZISHA MPANGO WA KUTOA MAFUNZO KWA VIJANAKUKIDHI MAHITAJI YA VIWANDA VYA NGUO

07:36    No comments





Posted by Esta Malibiche on April 2018 IN NEWS
Mhe. Charles J. Mwijage (Mb), Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, NFRA
Baadhi ya wakuu wa mikoa inoyozalisha Pamba kwa wingi wakifatilia mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Mgeni-Rasmi Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Mhe. Charles J. Mwijage (Mb), akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Naibu waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt Mary Mwanjelwa akijadiliana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Waziri wa kilimo, Mhe. Dkt Charles Tizebawakati akifatilia kwa makini mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.
Baadhi ya  wadau wa sekta ya pamba wakifatilia kwa makini mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018.

Na Mathias Canal, Dodoma

Serikali kwa kushirikiana na viwanda vya nguo na mavazi imeanzisha mpango maalum wa kutoa mafunzo ya ushonaji kwa vijana kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya viwanda vya nguo.

Upatikanaji wa ujuzi wa aina hiyo utapunguza gharama kwa wawekezaji na kuongeza ufanisi katika uzalishaji. Vilevile, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kupitia msaada wa Gatsby Africa, kimeendelea kutoa mafunzo ya Shahada ya Teknolojia ya Nguo (Textile Degree) ambapo, mwaka 2016/2017, Chuo kilitoa wahitimu 44 ikilinganishwa na wahitimu 13 kwa mwaka 2015/2016. Lengo ni kuhakikisha kuwa kuna wataalam wa kutosha wa fani ya ubunifu na uzalishaji mavazi nchini.

Hayo yamebainishwa na Mhe. Charles J. Mwijage (Mb), Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, wakati akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya pamba na mavazi katika halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hazina- Mjini Dodoma leo 20 Aprili, 2018
Alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazozalisha pamba kwa kiasi kikubwa barani Afrika, ikiwa na zaidi ya wakulima 500,000 wanaolima pamba katika eneo linalokadiriwa kufikia hekta 412,000 katika mikoa 13 nchini. Sekta ya nguo na mavazi ni moja ya sekta za Kipaumbele katika kusukuma gurudumu la maendeleo nchini na inahusisha mnyororo mrefu wa uongezaji thamani kuanzia kuchambua pamba (ginneries); kusokota nyuzi (spinning); kuseketa vitambaa (weaving); kufuma vitambaa (knitting),kuchapa na kutia rangi (processing) na kushona mavazi (garments).
Aliongezaa kuwa Sekta hii ni moja ya sekta muhimu katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuanzisha viwanda vinavyoajiri watu wengi kwa wakati mmoja. Sekta hii itawezesha kupunguza uingizaji wa nguo kutoka nje na kuongeza matumizi ya pamba inayolimwa nchini pamoja na malighafi nyingine zinazopatikana nchini kama vile magadi na gesi asilia.
Hata hivyo, Serikali imeendelea kuzishawishi taasisi za Umma kwa kuanzia majeshi na hospitali ili wanunue nguo na mavazi yanayozalishwa na viwanda vya ndani.  Lengo ni kuhakikisha kuwa utaratibu wa makusudi unawekwa kwa Taasisi za umma kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu hapa nchini. Kwa mfano uvaaji wa fulana aina ya Polo Shirt kwa wafanyakazi wote katika siku moja ya wiki, na pia wanafunzi wote shule za msingi na sekondari kuvaa sare hizo. Inakadiriwa kuwa kuna jumla ya wanafunzi milioni 15 na wafanyakazi wa sekta zote za umma wanafika 25,000.
Mhe Mwijage alisema kuwa Utengenezaji wa fulana moja ya polo unakadiriwa kutumia wastani wa gramu 300 za pamba, sketi moja inakadiriwa kutumia gramu 600 za pamba, kaptula moja inakadiriwa kutumia gramu 600 za pamba. Hivyo jumla ya gramu 900 za pamba zitahitajika kutengeneza sare kwa mwanafunzi mmoja awe wa kike au wa kiume.
Kama ikikadiriwa kila mwanafunzi atavaa wastani wa sare (sketi & shati au kaptula na shati) mbili tu kwa mwaka gramu 1800 (sawa na kilo 1.8) za pamba zitahitajika kwa mwanafunzi mmoja, hivyo wastani wa kilo 27,000,000 (sawa na tani 27,000) zitahitajika kwa mwaka. Endapo mahitaji yaliyokusudiwa yakipitishwa tunategemea kwamba viwanda vya ndani vitakuwa na uwezo wa kutumia asilimia 17 ya pamba yote inayozalishwa nchini kwa mwaka. Hii itahamasisha uzalishaji wa pamba, kuongeza ajira na kuongeza kipato.
“Serikali inakamilisha taratibu za kuidhinisha ‘’ Blue Print’’   ambayo imeainisha maeneo ya kufanyia maboresho ya Kisera na Kisheria ili kuhamasisha uwekezaji katika Sekta mbalimbali za uchumi ikiwemo sekta ya pamba nguo na mavazi” Alikaririwa Mhe Mwijage

Pia,aliwashukuru Wadau wa sekta ndogo ya pamba, nguo na Mavazi kwa kazi kubwa wanayofanya katika uzalishaji, biashara na wadau wengine kwa michango yao katika kuendeleza sekta hii. 

Mkutano huo umehusisha Wizari ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara wa Fedha na Mipango, Wizara ya Kilimo; Waheshimiwa Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge za Viwanda, Biashara na Mazingira; Bajeti; Kilimo, Mifugo na Maji; na Uwekezaji Mitaji ya Umma, Wakuu wa Mikoa; Makatibu Wakuu, Wawakilishi wa Sekta Binafsi, Maafisa wa Serikali na Taasisi za Serikali

Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye Facebook
Chapisho Jipya Taarifa za zamani Nyumbani

0 maoni:

Chapisha Maoni

Music

  • Popular
  • Tags
  • Blog Archives
  • HAMAD RASHID AAPISHWA AMUOMBA RAIS DK SHEIN KUTEUWA MAWAZIRI WATENDAJI WENYE UTAALAMU
    Ali Issa Maelezo, Zanzibar  Mwakilishi mteule wa Chama cha Alliance for Development Change (ADC) Hamad Ras...
  • Africa Carbon Forum 28 – 30 June, 2016
    ...
  • KILIMO BORA CHA ZAO LA MAEMBE
    Posted by Esta Malibiche on MARCH 6,2017 Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko k...
  • (kichwa hakijaongezwa)
    mbunge  wa Singida Kaskazin Bw Lazaro Nyalandu (kulia) akimpokea  waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba alipofanya...
  • MHE BITEKO AANZA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUKOMESHA UTORO MASHULENI, ACHANGIA MATOFALI 10,000 UJENZI WA MAABARA
    Posted by Esta Malibiche on April 3,2018 in NEWS Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto...
  • SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA KWANZA KOZI NA. 22 ZAFANA CHUO CHA MAGEREZA, TUKUYU MKOANI MBEYA
    Posted by Esta Malibi...
  • Rais Magufuli na Rais Lungu wakubaliana kufufua TAZARA na TAZAMA
    Posted by Esta Malibiche on Nov 28,2016 in NEWS     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Dkt. John Pombe J...
  • (kichwa hakijaongezwa)
  • DKT SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mw...
  • RC SHIGELLA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA VIWANDA MKOANI TANGA,AVITAKA KUONGEZA UZALISHAJI
    Posted by Esta Malibiche on JAN 31,2017 IN NEWS Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella akisaini kitabu cha wageni mara baada ...

Blog Archive

  • ►  2025 (1)
    • ►  Januari (1)
  • ▼  2018 (277)
    • ►  Agosti (1)
    • ►  Julai (11)
    • ►  Juni (36)
    • ►  Mei (30)
    • ▼  Aprili (62)
      • RAIS MAGUFULI AAHIDI KUIGEUZA IRINGA KUWA MKOA WA ...
      • PITIA VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YA LEO TZ NA ...
      • RAIS MAGUFULI AANZA ZIARA LEO MKOANI IRINGA,AFUN...
      • SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WA...
      • MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) UMEKUWA MSHIND...
      • RAIS MAGUFULI ANATARAJIA KUANZA ZIARA YAKE KESHO M...
      • PITIA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE ...
      • GGM YAVULIWA UBINGWA KOMBE LA MEI MOSI KITAIFA MKO...
      • UCHUKUZI YANYAKUA VIKOMBE SABA KATIKA MICHEZO YA R...
      • TIMU YA IKULU,UCHUKUZI ZAWANIA UBINGWA NETIBOLI KO...
      • RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO N...
      • MSAMAHA WA RAIS KWA WAFUNGWA KATIKA KUADHIMISHA MI...
      • RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA MAELFU YA WATANZANIA ...
      • MICHEZO YA MEI MOSI YAENDELEA KULINDIMA MKOANI IRI...
      • MUHUMBA,SCOLASTICA WAIBUKA MABINGWA WA BAISKELI M...
      • MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE APRIL 25, 2018
      • RAIS MAGUFULI AAGIZA KUSHUGHULIKIWA TATIZO KUBWA L...
      • LIPULI FC 1-1 SIMBA SC, ADAM SALAMBA AENDELEZA UBABE
      • SERIKALI YA CCM YANG'ARISHA IKUNGI KWA UMEME
      • BUNGE LAPITISHA BILLIONI 898 BAJETI YA WIZARA YA A...
      • UZALISHAJI WA CHAKULA NCHINI UMEIMARIKA-MAJALIWA
      • MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA UJENZI W...
      • TIMU ZA NETIBOLI,KAMBA ZA UCHUKUZI ZANG'ARA KOMBE ...
      • MKUU WA MKOA WA IRINGA AMINA MASENZA AWATAKA WANAN...
      • TUMBAKU,UCHUKUZI ZAONGOZA MICHUANO YA SOKA KOMBE ...
      • MADAKTARI BINGWA WABAINI WAGONJWA ZAIDI YA 460 WA ...
      • SERIKALI YAANZISHA MPANGO WA KUTOA MAFUNZO KWA VIJ...
      • PADRE BEATUS URASSA ATEULIWA KUWA ASKOFU WA JIMBO ...
      • MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE APRIL 20, 2018
      • TIMU YA WANAWAKE SEKTA YA UCHUKUZI YAIBUKA KIDEDE...
      • RAIS WA TUCTA AWATAKA WANANACHI MKOANI IRINGA KUIT...
      • TUMAINI NYAMHOKYA;WANANACHI IRINGA ITUMIENI MEI M...
      • PITIA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO APRIL 18,2018
      • MAVUNDE AMWAGA NEEMA KWA WAJISIRIAMALI DODOMA,AWAT...
      • Posted by Esta Malibiche ON April 16,2018 IN MICHE...
      • MTOTO MUDASILI AWALILIA WATANZANIA WANUSURU UHAI ...
      • MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE APRIL 12,2018
      • PITIA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE ...
      • CHAMA CHA MAPINDUZI CCM IRINGA MJINI CHAIKABIDHI H...
      • RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA KUMSIMIKA MHAS...
      • RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA KUMSIMIKA MHAS...
      • MBARAZA UVCCM DAR AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA VIJAN...
      • MAVUNDE AZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUHAKIKISHA ZIN...
      • MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE APRIL 7, 2018
      • DC IRINGA RICHARD KASESELA AWATAKA WAJASILIMALI KU...
      • MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE APRIL 6, 2018
      • MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI MJINI DODOMA LEO 5, A...
      • JAFO ASIMAMISHA UJENZI WA VIVUKO BARABARA YA NAMEL...
      • MAKAMU WA RAIS AHAMASISHA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO ...
      • RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MRADI WA KUZALISHA UMEME...
      • MWIGULU NCHEMBA KULIONGEZEA NGUVU JESHI LA POLISI
      • DOROTH MWAMPOMA AWATAKA WAZAZI KUWASOMESHA WATOTO
      • SERIKALI YAAHIDI KUBORESHA MICHEZO KATIKA TAASISI ...
      • YANGA YAJICHIMBIA MOROGORO KUWASUBIRI WAHABESHI JU...
      • MASOGANGE AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 3
      • MHE BITEKO AANZA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU L...
      • WAZIRI MKUU AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI...
      • PITIA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO APRIL 3,2018
      • RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA K...
      • PITIA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO TZ NA NJE ...
      • ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA IRINGA AWATAKA WAAMINI...
      • RAIS WA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA TARCI...
    • ►  Machi (45)
    • ►  Februari (59)
    • ►  Januari (33)
  • ►  2017 (602)
    • ►  Desemba (52)
    • ►  Novemba (59)
    • ►  Oktoba (59)
    • ►  Septemba (30)
    • ►  Agosti (43)
    • ►  Julai (29)
    • ►  Juni (80)
    • ►  Mei (15)
    • ►  Aprili (36)
    • ►  Machi (38)
    • ►  Februari (45)
    • ►  Januari (116)
  • ►  2016 (2522)
    • ►  Desemba (64)
    • ►  Novemba (185)
    • ►  Oktoba (207)
    • ►  Septemba (239)
    • ►  Agosti (303)
    • ►  Julai (313)
    • ►  Juni (358)
    • ►  Mei (262)
    • ►  Aprili (508)
    • ►  Machi (83)

 
  • Blogroll

  • About

Copyright © Ester Malibiche | Powered by Mkami Jr
- |