Wana CCM Iringa mji walivyoupamba mji wa Iringa
Na Esta Malibiche
Iringa
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli amefungua barabara ya Iringa,Migori Fufu iliyojengwa kwa kiwango cha rami yenye umbali wa KM 189.
Akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Iringa jana wakati wa uzinduzi barabara uliofanyika katika kijiji cha Ndolela kata ya Kihorogota Tarafa ya Isimani Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa,Mheshimiwa Rais aliwashukuru wafadhiri ambao ni Benki ya Maendeleo ya Afrika na Serikali ya Japan kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu hivyo kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.
"Tumepewa barabara,hivyo tunatakiwa tuchangamkie fursa kwa kujishughulisha na Biashara,kufuga na kulima mazoa tofauti yanayostahimili ukame.Ninawaomba Barabara hii kuitunza na iwe mkombozi wetu kwa kujiingizia kipato na si vinginevyo"
Rais Magufuli alisema Serikali imeamua kuwa Iringa iwe sehemu ya Mkoa wa Utalii kutokana na mbuga kubwa ya wanyama iliyopo.
Tumeamua kuutengeneza uwanja wa Nduli kuwa wa rami ili ndege ziweze kutua ili wananchi wa Iringa waweze kunufaika kwa kutumia fursa zinazotokana na watalii.
Aliwataka wananchi kuijenga Nchi kwa kufanya kazi kwa bidiii kila mmoja katika nafasi yake ili pato la Nchi liendelee kuongezeka.Pia aliwasihi watanzania kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuondokana na ajali zinazoweza kuepukika.
Wakati huo huo amezitaka Halmashauri kuweka mikakati ya kuwapunguzia Wananchi ushuru katika Mazoa ili waweze kunufaika na Kilimo na hivyo kujikwamua kiuchumi.
Akisoma taarifa ya Mradi wa ujenzi wa barabara,mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng.Joseph Nyamhanga alisema kuwa kiasi cha Bil.207.4 zimegharimu ujenzi huo,ambapo Tz.imechangia 12.8 %,Benki ya Maendeleo ya Afrika 65.9% na Serikali ya Japan imechangia 21.3%.
Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dejene Demessie akitoa salam kutoka Benki hiyo alisema kuwa Benki inaipongeza Serikali ya awamu ya Tano chini ya Uongozi wake Rais Magufuli kwa kutekeleza miradi yake kwa wakati.
"Hii inaleta Matumaini makubwa kwa wananchi na wale wanaojitoa kusaidia ili waendelee kusaidia"
Demessie alisema Benki ya Maendeleo ya Afrika inaipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa hatua ya kukuza uchumi wa Nchi.
"Tunaamini barabara hii itaweza kuboresha maisha ya wananchi kiuchumi kwa kufanya biashara hivyo kujiingizia kipato.Pia Benki inatambua vipaumbele vilivyowekwa kuhakikisha Maendeleo ya uchumi yanaongezeka" Alisema
Nae Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na mawasiliano Makame Mbarawa alisema kuwa kukamilika kwa barabara hii kutarahidisha usafiri na usafirishaji katika mikoa ya Iringa na Dodoma pamoja na mikoa jirani.
"Mheshimiwa Rais Wizara yangu itahakikisha fedha zilizotengwa kwq ajili ya Miradi ya Barabara zinatumika ipasavyo huku tukiakikisha barabara inatunzwa" Alisema Waziri Mbarawa
Alisema Barabara hii ya Iringa_Migori_Fufu ni sehemu ya barabara ya Iringa_Dodoma yenye KM 260.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni