Posted by Esta Malibiche on April 3,2018 in NEWS
Shule ya Sekondari
Wenda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya
Mbeya Vijiji Mkoani Mbeya,eneo la Mbalizi,imewataka wazazi kuona umuhimu
wa Elimu kwa kuwasomesha watoto wao.
Kauli hiyo
imetolewa na Afisa Uhusiano wa Shule hiyo Doroth Mwampoma wakati akizungumza na
mtandao huu wa Habari [KALI YA HABARI BLOG]ofisini kwake,ulipotembelea shule hiyo jana kwa lengo la kufanya mahijiano maalum.
Doroth alisema kuwa shule
hiyo ina wanafunzi mchanganyiko ambao
wanatoka ndani ya Nchi na Nje,yenye malezi bora na inamjerngea mtoto uwezo wa kufanya vizuri katika masomo yake,na wanafunzi wote ni wa bweni.
'Toka Shule hii ilipoanza wanafunzi hawajawahi feli katika matokeo ya kidato cha pili,nne na sita.Hii ni kutokana na umahili wa walimu wetu katika ufundishaji.Tuna walimu wa kutosha kabisa,mazingira ya shule ni rafiki,vyumba vya madarasa vipo vya kutosha,na mazingira mazuri ya mkumfanya mwanafunzi aendelee kujifunza zaidi na zaidi'Alisema Doroth
Doroth alisema kuwa
maendeleo miongoni mwa jamii yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na kiwango
cha uwekezaji katika elimu, ni vema jamii iwekeze kutambua na kuona umhimu katika elimu kwa kuwasomesha watoto wao ili wawaeze
kujikwamua na umaskini uliopo na kupambana katika soko la ajira.
Ninawaomba wazazi wawalete watoto wao
katika shule ya sekondari Wenda,ada zetu ni nafuu na unalipa kidokidogo.Pia,Fomu za kujiunga na Shule hii zinapatika wenda sekondari na katika tofutti ya wenda
ambayo ni www.wenda High school.com
Aidha aliwataka wazazi na walezi kote nchini kuwa msatari wa
mbele na kuona umuhimu wa kuwekeza katika elimu.Nawaomba wawalete katika Shulea
ya Sekondari Wenda ili wawaeze kupata elimu iliyobora.
0 maoni:
Chapisha Maoni