Posted by Esta Malibiche on April 1,2018 IN NEWS
Na Esta Malibiche
Iringa
Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania,ambae pia ni Askofu Wa Jimbo Katoliki la Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amewataka waamini kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli na Serikali yake ili waweze kuliongoza Taifa kwa uzalendo wa kutenda haki kwa Raia wake.
Kauli hiyo ameitoa mapema leo hii wakati akitoa homilia yake katika adhimisho la Ibada ya Misa Takafitu ya Sikukuu ya Pasaka katika kanisa kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu Parokia ya Kihesa jimboni katoliki la Iringa.
Alisema kuwa Rais peke yake hawezi,hivyo ni jukumi la kila mkristo kumuombea yeye na Serikali yake ili iwe yenye Huruma Kwa watu wake.Watanzania tunapaswa kuliombea Taifa ili lisije kuingia katika machafuko yasiyostahili.
"Tukemee mambo yatakayotugawa kwasababu Sisi sote ni wamoja na watoto wa baba mmoja hivyo tunatakiwa tuitunze Amani hii tuliyonayo ambayo ni tuna toka kwa Mungu" Alisema Ngalalekumtwa na kuongeza kuwa
Aidha akizungumzia hali ya hewa Nchini alisema kuwa kutokana na Mvua kuchelewa kunyesha,pia maeneo mengine hazijafika kabisa,aliwataka waamini kukitumia vizuri chakula naweka akiba.
"Waamini wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania katika maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishajiwanahamasishwa na Mama Kanisa kuhakikisha kwamba, wanajitahidi kumjua Yesu Mfufuka, kuungana, kujitoa na kujituma zaidi kwa huduma inayomwilishwa zaidi katika upendo kwa Mungu na jirani, kielelezo makini cha imani tendaji na wala si kufanya mambo kwa mazoea.
Kama sehemu ya mchakato wa maadhimisho haya, familia ya Mungu nchini Tanzania inahamasishwa kufiriki na kuambata yale yaliyo juu, huku ikiongozwa na Roho Mtakatifu idumishe upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi, kwani haya ni matunda ya Roho Mtakatifu" Alisema Ngalalekumtwa.
Kama sehemu ya mchakato wa maadhimisho haya, familia ya Mungu nchini Tanzania inahamasishwa kufiriki na kuambata yale yaliyo juu, huku ikiongozwa na Roho Mtakatifu idumishe upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi, kwani haya ni matunda ya Roho Mtakatifu" Alisema Ngalalekumtwa.
Hata hivyo aliwataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema nchini Tanzania, kuyaisha maisha yao mintarafu Ufufuko wa Kristo Yesu kutoka kwa wafu kwa kutenda yaliyomema ya kumpendeza Mungu,Taifa na Jamii kwa ujumla ikiwa na kuachana na vitendo visivyofaa ambavyo vinaweza leta athari Nchini.
.
0 maoni:
Chapisha Maoni