Posted by Esta Malibiche on April 21,2018 IN NEWS
MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewaomba wakazi wa Mkoa wa Iringa kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wa Jmuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli anaetarajia kuwa mgeni rasmi katika Maaadhimisho ya Sherehe ya Siku ya wafanyakazi Duniani,[Mei Mosi ambayo kitaifa yanafanyika Mkoani Iringa katika uwanja wa Samora,uliopo Manispaa ya Iringa.
Akizungumza na Vyombo vya Habari Ofisini kwake aliseama katika kuelekea kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Mei Mosi kitaifa matukio Mbalimbali yanaendelea zikiwemo ikiwemo semina,michezo na makongamano yatakayofanyika katika wilaya zote za Iringa.
“Kuelekea kilele cha maadhimisho hayo ya mei mosi mwaka 2018 kutakuwa na michezo mbalimbali itakayokuwa inachezwa katika viwanja mbalimbali hapa mkoani Iringa na michezo hiyo ni kama ifuatayo mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba,bonanza la michezo mbalimbali na michezo hii ilianza tarehe 17 /04 /2018 na itahitimishwa 30 /04 / 2018” alisema masenza
Akielezea juu ya maandalizi ya sherehe za mei mosi mkoani Iringa alisema kwa sehemu kubwa maandalizi yanakwenda vizuri na wamepata ratibu ya kuzunguka wilaya zote za mkoa wa Iringa kutoa elimu pamoja na kututana na wafanyakazi ili kujua changamoto zao.
“Tumejiridhisha kuwa kila kitu kinaenda kama tulivyopanga ndio maana leo tunahuru wa kusema kuwa mei mosi itafanyika kwa mafanikio makubwa mno” alisema
Hata hivyo Masenza aliwataka wafanyakazi kujitokeza kwa wingi kushiriki sherehe hizo na kuwa kupitia sherehe hizo watapata fursa ya kujua mikakati ya serikali dhidi ya wafanyakazi hapa nchini.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa TUCTA Taifa Dk.Yahaya Msigwa alisema wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa ya Mei Mosi kujiingizia kipato.
‘Tunategemea kwa kipindi hiki ambacho Mkoa unapokea ugeni wananachi hasa wale wenye nyumba za kulala wageni,mama ntilie na wafanyabiashara wadogowadogo na wakubwa’Alisema Msigwa
‘Wafanyakazi wanapopewa elimu tunapunguza matatizo kwa wafanyakazi hivyo ninawaomba waendelee kujitokeza katika makongsamano yanayoendelea ili wawaeze kujifunza na kupata majibu ya yale yanayowatatiza mahali pao pa kazi’Alisema Dk.Msigwa
Aidha aliwataka wananachi wa Mkoa wa Iringa kuitumia vizuri Mei Mosi katika biashara ili kutengeneza mahusiano mazuri
. |
0 maoni:
Chapisha Maoni