Ijumaa, 6 Aprili 2018

DC IRINGA RICHARD KASESELA AWATAKA WAJASILIMALI KUTUMIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI.

Posted by Esta Malibiche on April 6,2018 IN SIASA

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitembelea mabanda ya Wajasiliamali katika Mafunzo na Maonedho ya Ujasiliamali yanayoendelea Manispaa ya Iringa katika eneo la Olofea yaliyoandaliwa na UVCCM Mkoa wa Iringa.


NA ESTA MALIBICHE
IRINGA
WAJASILIAMALI nchini watakiwa kutumia fursa za kibiashara ili kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa jana   na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakati wa Uzinduzi wa kongamano la Mafunzo na maonesho  ya  bidhaa za ujasiliamali kwa wananachi wa Mkoa wa Iringa.
Kasesela  alisema kuwa endapo wajasiliamali wakitumia fursa za kufanya biashara kwa bidhaa watakazokuwanazo kutawafanya kupata kipato ambacho kitawaondoa katika hali ya umaskini.
 “Kijana mwenye uwezo wa kubuni biashara inayouzika katika soko atakuwa na uhakika wa kupata fedha kutokana na biashara yake hivyo ni vyema kila mmoja atumie fursa ya kufanya biashara inayouzika”alisema Kasesera.
Pia alizitaka Halmashauri zitoe elimu kwa vijana(kuhusu asilimia zinazotolewa na Serikali kwenye mikopo) ili wawe na ufahamu utakaowafanya kufanya maamuzi ya kuomba mkopo kwa aji ya biashara.
Mwenyekitiki wa jumuiya ya umoja wa vijana chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa(UVCCM),Kenani Kihongosi alisema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa vijana wa mkoa wa Iringa kuwajengea uwezo wa kufanya biashara yenye soko ili kuwa na uhakika wa kupata kipato halali.

Kihongosi alisema kuwa elimu hii itawasaidia kujiajiri ili waweze kujipatia kipato, kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya Tanzania ya viwanda.
“Kijana ni lazima aelewe ni biashara gani anayoweza kubuni na kuangalia soko lake liko vipi ili atakapoanza biashara yake awe na uhakika wa kuuza sokoni”alisema Kihongosi.
Alisema kuwa watu wengi wamesoma lakini wamekuwa haitumii elimu yao kwa kujiajiri kwa kuwa elimu waliyonayo ni mtaji wa kwanza na mtaji wa pili ni fedha kwa ajili ya biashara.
Alisema kuwa kongamano wa wajasiamali lililoandaliwa naUVCCM mkoa wa Irinnga ambapo vijana zaidi ya 500 wameshiriki na kuonesha bidhaa zao wanazozalisha.
Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Iringa (CCM), Christopher Magala vijana ni wengi na nguvu kazi ya Taifa hivyo wakitumia nafasi yao vyema katika kuzalisha wataweza kujiingizia kipato wenyewe na nchi.
“Vijana waongeze ujuzi ili kuweza kuutumia katika kuzalisha mali ili kuweza kuendana na kasi ya serikali ya viwanda kwa kuzalisha bidhaa bora”alisema.
Kwa upande wake Afisa maendeleo manispaa ya Iringa, Marcelina Ngowi alisema mafunzo haya ni kuwawezesha vijana kupata elimu ya kuzalisha mali watakayoitumia kuzalisha mali yenye kiwango bora.
Alisema kuwa ili kuondokana na changamoto ya kutokuwa na kipato ni vyema wakatumia fursa hii ya kupata elimu na kuitumia katika kuzalisha bidhaa yenye ubora.
Mafunzo hayo yenye kauli mbiu ya 'IRINGA YETU NA UCHUMI WA VIWANDA'yanaendelea katika ukumbi wa Olofea Manispaa ya Iringa ambayo yanatarajiwa kufungwa rasmi kesho jumamosi na Naibu Waziri wa Vijana Anthony Mavunde.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo na Maonesho ya Ujasiliamali.Uzinduzi huo ulifanyika jana na yanayoendelea leo,ambapo kesho yanatarajiwa kufungwa rasmi na Naibu Waziri wa Vijana Anthony Mavunde.


Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Christopher Magala akizungumza,ambapo aliwataka Vijana waongeze ujuzi zaidi katika bidhaa zao wanazozalisha   ili kuweza kuendana na kasi ya serikali ya Tanzania ya viwanda kwa kuzalisha bidhaa bora
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Iringa Kenani Kihongosi akizungumza,aliwasihi vijana kujiajili ili kupunguza wimbi la vijana wasio na Ajira .Alisema kuwa watu wengi wamesoma lakini wamekuwa hawaitumii elimu yao kwa kujiajiri kwa kuwa elimu waliyonayo ni mtaji wa kwanza na mtaji wa pili ni fedha kwa ajili ya biashara.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiendelea kutembelea mabanda ya Wajasiliamali na kukagua bidhaa zinazozaliwashwa. Mafunzo hayo yanayoendelea Manispaa ya Iringa katika eneo la Olofea ambayo yameandaliwa na UVCCM Mkoa wa Iringa.



0 maoni:

Chapisha Maoni