Posted by Esta Malibiche on April 27,2018 IN MICHEZO
Mshambuliaji Ramadhani Shegodo wa Tumbaku akikokota mpira kwenye mchezo wa nusu fainali wa michuano ya Kombe la Mei Mosi dhidi ya Geita Gold Mine (GGM) uliofanyika leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa. Tumbaku wametinga fainali kwa magoli 4-1.
Nahodha wa timu ya Geita Gold Mine (GGM), Mohamed Salum (mwenye mpira) akimtoka mlinzi wa Tumbaku Hossein Mbongwa (9) katika mchezo wa nusu fainali wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyikka leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa. Tumbaku walishinda magoli 4-1.
Beki wa Uchukuzi Erick Mpunga (jezi ya bluu) akitoa hatari langoni mwake huku mshambuliaji Kurwa Makaranga wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akijaribu kutibua katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa. Tanesco wametinga fainali kwa magoli 2-1.
Kiungo wa Uchukuzi Suleiman Kaitaba (kushoto) akimpiga chenga Joseph Mzee wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Mei Mosi uliofanyika leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa. Tanesco waliibuka washindi kwa magoli 2-1.
Kipa Willy Barton (1) wa Uchukuzi akidaka
mpira uliyepigwa na Suleiman Ismail aliyeanguka kushoto) wa Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) katika mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Mei Mosi
uliofanyika leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa. Tanesco wameshinda kwa
magoli 2-1.
TIMU
inayoundwa na wachezaji chipukizi ya Tumbaku ya Morogoro leo iliwavua ubingwa
wa michuano ya Kombe la Mei Mosi timu ya Geita Gold Mine (GGM) na kutinga hatua
ya fainali baada ya kuwafunga magoli 4-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu
fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Tumbaku
ambayo haijapoteza mchezo tangu ilipoanza hatua ya makundi ikiwa kundi ‘A’ na
GGM ikiwa kundi ‘B’ ilianza kupata bao lake la kwanza kupitia kwa mshambuliaji
wake Kelvin Makamba aliyepiga shuti kali nje ya 18 katika dakika ya pili.
GGM
walisawazisha katika dakika ya 44 kwa kichwa kilichopigwa na Oswald Binamungu baada
ya kupata pasi ya Ferdinand Makaranga.
Tumbaku
waliongeza bao la pili katika dakika ya 51kupitia kwa mshambuliaji wake Issa Simbaliane
aliyepiga mpira wa faulu uliokwenda moja kwa moja golini, huku bao la tatu
lilipachikwa kimiani katika dakika ya 62 baada ya Emmanuel Mwakibinga
kuunganisha kwa kichwa kona iliyochongwa na Idd Likasi.
Kiungo
Idrisa Magongo alifunga kitabu cha magoli katika dakika ya 79 kwa kufunga bao
la nne.
Hatahivyo,
Katibu mkuu wa timu ya GGM, Wilhemin Bayanga pamoja na kukiri mchezo ulikuwa
mkali na mzuri lakini wameikatia rufaa timu nzima ya Tumbaku kwa madai
wamechezesha mamluki.
Katika
mchezo mwingine wa nusu fainali timu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
imeingia fainali baada ya kuifunga timu ngumu ya Uchukuzi kwa magoli 2-1.
Uchukuzi ndio walikuwa wa kwanza kupachika bao katika dakika ya 67 kupitia kwa
Omary Kitambo.
Tanesco
walisawazisha kwa njia ya penati iliyotolewa na mwamuzi Winfred Fyataga, katika
dakika ya 70 na Seleman Ismail baada ya kipa Willy Barton kumchezea madhambi Gossage Mtumwa. Bao la ushindi la Tanesco
lilifungwa na Fortunatus Mgimba katika dakika ya 76 baada ya kipa Barton
kuusukumiza mpira wa kona uliochongwa na mfungaji.
Kocha
Mkuu wa Tanesco, Fidelis Almas amekiri leo atakuwa na kibarua kipevu kutokana
na Tambuku kutokana na wachezaji wake kuwa chipukizi zaidi.
“Ninajua
mechi itakuwa kali lakini tumejiandaa kukabiliana na Tumbaku kwani tunawajua
kutokana na kuwaona mara kadhaa wakiwa wanacheza na tulikuwa kundi moja,”
alisema Almas.
Wakati huo huo,
timu ya Uchukuzi imeongeza kikombe baada ya kushinda Mzee Omari Said kuibuka
bingwa katika mchezo wa bao uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa Iringa.
Ushindi wa pili ulichukuliwa na Suleiman Chitanda wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) na Shaaba Kidang’ala wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) aliibuka
wa tatu.
MWISHO
0 maoni:
Chapisha Maoni