Alhamisi, 19 Aprili 2018

TUMAINI NYAMHOKYA;WANANACHI IRINGA ITUMIENI MEI MOSI KUNUFAIKA KIUCHUMI


Posted by Esta Malibiche on April 19,2018 IN NEWS
RAIS wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa kutumia maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi mwaka huu ambayo yatafanyika mkoani Iringa  kuwa chachu ya kuongeza uchumi wao .
Akizungmza na vyombo vya habari Mkoani Iringa ujuio wa sherehe hizo mkoani hapa zitawasaidia wananchi wengi kujipatia kipato chao wenyewe,kuonesha biashara zao,pamoja na wadau mbalimbali ikiwawemo wenye mahoteli nk.
Nyamhokya alisema kuwa kwenye sherehe hizo wananchi wanatakiwa  kuonesha bidhaa zao wakati huu ambao serikali ikipambanua kuelekea kwenye uchumi wa kati wa viwanda.
 “Tumekuja hapa kuandaa maandalizi ya ujio wa viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Mgeni Rasmi ambae ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.

 Sisi kama viongozi tiunawaomba wananchi wachukulie kama fursa kwao .Pia tunawaomba sana wana Iringa kujitokeza kwa wingi kumpokea Mh.Rais.”alisema Nyamhokya
Naye  Paulo Sangeze ambaye ni mwenyekiti  Tuico taifa alisema kuwa malalamiko yaliyopo kwenye sekta ya viwanda kwa wafanyakazi yanaendelea kutatuliwa serikali huku akiwataka wafanyakazi wote kushiriki mei mosi kikamilifu.
Kwa upoande wake Stanslaus Mhongole ambaye ni mwenyekiti wa CWT mkoa wa Iringa amesema sherehe zilitakiwa kufanyika jijini Arusha lakini kutokana na kuwa na sababu zilizo nje ya uwezo imebidi wahamishe sherehe hizo mkoani Iringa huku akiwataka wananchi kutumia sherehe hizo kwakuibua fursa za kiuchumi.

0 maoni:

Chapisha Maoni