Posted by Esta Malibiche on April 28,2018 IN NEWS
Na Esta Malibiche
Iringa
MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka wananchi wa Mkoa wa Iringa kujitokeza kwa wingi kumpokea Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzania Dkt.John Magufuli anaetarajia kuwasili mkoani Iringa kesho April 29, akitokea Mkoani Dodoma.
Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo hii ofisini kwake alisema kuwa Mh.Rais anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Iringa kuanzia tarehe 29/4/2018 hadi tarehe 5/4/2018,ambapo anatarajia kufungua na kuelekeza shughuli mbalimbali za Maendeleo Mkoani Iringa.
"Mapokezi ya Mhe.Rais yatafanyika kwenye kijiji cha Ndolea wilaya ya Iringa na baada ya mapokezi atasomewa taarifa ya Mkoa na kufungua barabara ya Iringa_Migoro _Fufu" Alisisitiza Masenza na kuongeza kuwa
Katika ziara yake Mkoani hapa, Mhe.Rais anatarajia kuwa Mgeni rasmi kwenye sherehe za Mei Mosi kitaifa Mkoani Iringa.Sherehe hizo pia zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mh.Makamu wa Rais,Mh.Waziri Mkuu,Mh.Spika,Mh.NaibuSpika, Waheshimiwa Mawaziri,Wabunge,wakuu wa Mikoa,viongozi mbalimbali wa kitaifa na Mabalozi.
Masenza alisema kuwa Mh.Rais ataweka jiwe la Msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo,atazindua kiwanda cha Silverland kilichopo Wilaya ya Mufindi pia atafungua barabara ya Iyovi_Iringa katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga.
"Kwakuwa Iringa kuanzia sasa tumepata wageni wengi wakiwemo wa kitaifa,naomba tuwahufumie vizuri hasa wamiliki wa Mahoteli,Watengenezaji wa vyakula.Tuonyeshe kwa vitendo dhana ya kuendeleza utalii wa ndani ya " Karibu kusini ili wageni hawa watamani tena kurudi Mkoani Iringa"Alisema Masenza.
0 maoni:
Chapisha Maoni