Posted by Esta Malibiche on April 19,2018 in NEWS
Rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya akizungumza na vyombo vya Habari ,kushoto kwake ni Paulo Sangeze Mwenyekiti Tuico taifa. |
Na Esta Malibiche
Iringa.
Rais wa shirikisho
la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya amewataka wafanyakazi,wajiri,wananachi
hasa wakazi wa amkoa wa IRINGA wametakiwa
kushiriki katika matukio mbalimbali yakiwemo kongamano,Semina na Maonesho ili kufikia Kilele cha Mei Mosi 2018 kinachotarajiwa kufanyika Mkoani Iringa.
Akizungumza na vyombo vya Habari Mkoani hapa kuhusu maandalizi ya Mei Mosi kitaifa alisema kuwa katika kuelekea kilele kutakuwa
na matukio muhimu zikiwemo semina mbalimbali mahala pa kazi na sekta zisizo rasmi zikiwa
na maudhui ya kuelimisha sheria za kazi,Afya na Usalama kazini.
Nyamhokya alisema kuwa kabla ya kilele kutakuwa na
makongamano mawili ya kimkoa na moja la kitaifa,ambapo yanatarajiwa kufanyika
Wilayani Mufindi na Wilayani Kilolo huku yakiambatana na kongamano kubwa la
kitaifa litakalohusu TANZANIA YA VIWANDA,ambalo litafanyika katika ukumbi wa
kichangani Manispaa ya Iringa na litakalo washirikisha viongozi wa
kitaifa,wanazuoni,waajiri, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi kwa
ujumla.
''Maadhimisho ya Mei Mosi 2018,yamebeba ujumbe usemao’Kuunganishwa
kwa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kulenge kuboresha mafao ya mfanyakazi,na Mgeni
rasmi anatarajia kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John
Magufuli ‘alisema Nyamhokya na kuongeza kuwa
Michezo ya Mei Mosi ya fani mbalimbali
inaendelea katika viwanja vya samora ambayo ilianza toka tarehe 16,4,2018 mpaka 30,4,2018.
Aidha alisema kutakuwa na banda ya maonesho ya
huduma na bidhaa kutroka taasisi
mbalimbali za Serikali na binafsi,wajasiliamali wakubwa na wadogo kutoka ndani
ya Mkoa na nje, na yatafanyika katika
viwanja vya kichangani kuanza tarehe 25,4,2018 mpaka 28,4,2018.Pia kutakuwa na
burudani zikiwemo Muziki wa dansi,kizazi kipya, ngoma za asili,kwaya na tenzi.
0 maoni:
Chapisha Maoni