Posted by Esta Malibiche on April 4,2018 in NEWS
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kushoto)
akikagua ujenzi wa Vivuko katika barabara ya Namelock-Loltepes-Sunya
yenye urefu wa Km 88 iliyopo katika Wilaya ya Kiteto.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kulia)
akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Vivuko katika barabara
Namelock-Sunya wakati wa ziara yake Wilayani Kiteto.
Huu ni muonekano wa baadhi ya
Kivuko kinachojengwa katika barabara ya Namelock – Loltepes – Sunya
ambavyo Waziri Jafo amesimamisha ujenzi wake kutokana na dosari
zilizojitokeza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kulia) akitoa
maelekezo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Namelock – Loltepes
– Sunya yenye urefu wa Km 88 wakati wa ziara yake Wilayani Kiteto.
…………………
Nteghenjwa Hosseah, Kiteto
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesimamisha
ujenzi wa vivuko vyote katika ujenzi wa barabara ya Namelock-Loltepes
Sunya yenye urefu wa Km 88.1 inayojengwa katika Wilaya ya Kiteto na
Mkandarasi Deniko Constraction Ltd.
Waziri Jafo ametoa agizo hilo
mapema jana wakati wa ziara yake Wilayani humo kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo na kubaini mapungufu makubwa katika ujenzi wa
vivuko zaidi ya kumi alivyovipitia ndipo alipoagiza kusitisha ujenzi huo
mara moja hadi hapo Wataalamu wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini
(TARURA) watakapofika kukagua barabara ma kuwasilisha ripoti.
Aidha kutokana na hali hiyo ya
aligiza Mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa barabara hiyo Deniko
Construction sambamba na Mhandisi Mshauri Luptain Consult Ltd, Mhandisi
Consulting Engineers pamoja na ACE Consultant kufika Ofisini kwake mara
moja kutoa maelezo ya kina ya mapungufu hayo yaliyojitokeza katika
ujennzi wa barabara hiyo.
“Ni mara ya tatu sasa nakuja
kukagua Barabara hii na kila mara nabaini changamoto tofauti sjui kuna
tatizo gani nahitaji kusikia zaidi kutoka kwa wataalamu wa pande zote
ili tutafute suluhisho kwa pamoja”Alisema Jafo.
Aliongeza kuwa hapo awali Barabara
hii iligawanywa kwa wakandarasi wajenzi wawili ambaye ni huyu Deniko
alikuwa anajenga upande mmoja wenye Km 44 na Km 44 zilizobakia alipewa
Maginga Construction ambaye alishindwa kabisa kazi hii ndipo nilipoagiza
taratibu zifuatwe ili kuvunja mkataba wa awali na kazi ile apewe
Mkandarasi mwingine.
“Kazi hiyo aliongezewa Deniko
Construction ambaye kwa sasa ndiye anayejengwa barabara hii yote yenye
Km 88. Hapo awali kazi yake ilionekana nzuri sana na ya kuridhisha
lakini baada ya mvua za msimu huu mapungufu makubwa yamebainika hasa
katika vivuko vyote vilivyojengwa haviendani na mahitaji ya barabara
hii” Alisema Jafo.
Naye Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya
ya Kiteto Elias Paul alisema kuwa tatizo lililobainika katika ujenzi wa
vivuko hivyo ni Vivuko hivyo haviendani na wingi wa maji ya maji
yanayopita na vipenyo vya vivuko ni vidogo hivyo havina uwezo wa
kuhimili maji na takataka zingine zinazotakiwa kupita hapo na ni rahis
sana kuziba na hata kivuko chote kubebwa na maji ndani ya kipindi
kifupi.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya
Nmelock – Loltepes – Sunya unatekelezwa na Serikali kupitia Fedha za
wafadhili kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Marekani
(USAID) chini ya mpango wa (FEED FOR FUTURE) unaotekelezwa katika Wilaya
Nne Nchini ambazo ni Kilombero, Mvomero, Kongwa na Kiteto.
Wilaya ya Kiteto kupitia kwa
Wakala wa Babarabara za Mijini na Vijiji (TARURA) inahudumia mtandao wa
barabara zenye jumla ya urefu wa Km 1,088.35 kati ya barabara hizo km
2.8 ni za Lami, Changarawe Km 132 na Udongo Km 955.
0 maoni:
Chapisha Maoni