Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Jumatatu, 26 Februari 2018

PITIA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO

Posted by Esta Malibiche ON Februari 27,2018 IN KITAIFA








MJUMBE WA BARAZA KUU TAIFA UVCCM GWANTWA MWAKIJUNGU AKABIDHI BATI 30 KATA YA KIJICHI

Posted by Esta Malibiche on Februari 26,2018 IN SIASA

 Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM,Mkoa wa -Dar es salaam Gwantwa Alex Mwakijungu amekabidhi bati 30 katika kata ya Kijichi kwa ajiri ya uezekaji wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Mission iliyopo Kijichi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi alisema kuwa lengo la kutoa mchango huo ni kutaka kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Aidha aliwashuruku wakazi wa Kijichi kwa niaba ya Umoja wa Vijana CCM Dar es salaam kwa imani kubwa walionyesha kwa Chama Cha Mapinduzi na Vijana kwa kumchagua Mtalawanji kuwa Diwani wa kata hiyo katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.


"Mtalawanje ni Kijana mwenzetu. Kumchagua kwenu nyinyi wananchi wa Kijichi kuwa Diwani wenu ni dhamana ya vijana wote wa UVCCM Dar kwani yeye anatuwakilisha sisi. Utendaji wake ndio mwangaza wa sisi vijana katika duru za uongozi kwani akifanikiwa yeye,sisi tutakuwa na jeuri ya kugombea nafasi nyingine za uwakilishi kwa kumtumia yeye kama mfano wa kuwa Vijana tunaweza. Na nina waahidi kuwa sisi viongozi wa jumuiya tutakuwa nae bega kwa bega kuhakikisha mipango ya maendeleo ya Kijichi inafanikiwa" Alisema

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kijichi Mh Eliassa Kassim Mtalawanje alimshukuru  Alex kwa mchango wa bati pia aliwaomba wadau wengine mbalimbali waweze kujitokeza na kutia nguvu katika shughuli za kimaendeleo mbalimbali ili kusaidia kuonesha njia kwa serikali katika kutatua changamoto za wananchi.





MAVUNDE AAGIZA WAAJIRI MWANZA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHINDWA KUJISAJILI MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI-WCF

Posted by Esta Malibiche on Februari 26,2018 IN NEWS

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde ameagiza Wakurugenzi wa Kampuni ya  Ujenzi ya *JASCO LTD,AIRCO na JB BELLMONT HOTEL* kufikishwa Mahakamani kwa kushindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF).

Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika mkoa wa Mwanza kukagua Viwango vya Kazi na kufuatilia utekelezaji wa Agizo la *Mh* *Waziri Jennister Mhagama* ambaye aliwataka waajiri wote nchini wawe wamejisajili kwenye mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi kabla au ifikapo tarehe *30.09.2017*

Katika Mkoa wa Mwanza jumla ya waajiri takribani 700 hawajajisajili katika mfuko wa Fidia wa Wafanyakazi ambapo zoezi la msako wa waajiri hao litaendelea kwa wiki nzima na kuwachukulia hatua stahiki wale waajiri wote wataokuwa hawatii matakwa ya sheria ya Fidia ya Wafanyakazi.

Kwa mujibu wa Kifungu cha  71(4) Mwajiri yoyote atakayeshindwa kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi atashitakiwa Mahakamani na akikutwa na hatia adhabu yake ni faini isiyozidi *TSh* *50,000,000* au kifungo cha *miaka mitano* au vyote kwa pamoja.

Aidha Mavunde amemuagiza Afisa Kazi Mfawidhi wa Mwanza kuwapa waajiri hao Amri tekelezi ya siku 30 kutekeleza matakwa ya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Na. 6/2004 kwa kuwapa Wafanyakazi wao mikataba,malipo ya mshahara kwa kima cha chini cha sekta husika na kuwasilisha michango ya wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.












MAVUNDE AANZA ZIARA MKOA WA MWANZA,ATEMBELEA OFISI YA CCM MKOA .

Posted by Esta Malibiche on Februari 26,2018 IN NEWS
Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu,na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,Anthony Mavunde akisalimiana na Katibu wa  CCM Mkoa wa MwanzaRaymond Mangwala mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Anthony Mavunde ambaye yupo mkoa wa Mwanza kwa ziara ya kikazi ya kukagua Viwango vya Kazi na Usajili wa waajiri kwa mfuko wa fidia wa wafanyakazi(WCF).

Mapema leo hii ametembelea ofisi za CCM MKOA wa Mwanza kwa ajili ya kusalimiana na viongozi kuelezea kazi ambayo amekuja kuifanya mkoani hapo na kanda ya ziwa.




 Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu,na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,Anthony Mavunde akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.





KILIMO, VIWANDA VYAINUA PATO LA MKOA WA IRINGA



Posted by Esta Malibiche on Februari 26,2018 in NEWS

Image result for MKUU WA MKOA WA IRINGA AMINA MASENZA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Amina Masenza akizungumza na Wandishi wa Habari[hawapo pichani]kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu.

MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amesema kuwa Sekta ya kilimo na viwanda inaendelea kwa kasi Mkoani hapa,huku ikichangia kuongezeka kwa pato la Mkoa kutoka Sh trilioni 2.3 mwaka 2010 hadi  kufikia Sh trilioni 5.10 mwaka 2016.

Akizungumza na wandishi wa Habariofisini kwake,  alisema; “pato la Mkoa huchangiwa kwa kiasi kikubwa na mashamba makubwa ya chai, misitu na tumbaku pamoja na viwanda vya  vyake.”

Alisema ongezeko hilo limenyanyua pia pato la mkazi kutoka Sh Milioni 1.3 mwaka 2010 hadi Sh Milioni 2.9 mwaka 2016.

Alisema sekta ya kilimo mkoani Iringa ni muhimili mkuu wa uchumi na inachangia katika usalama wa chakula na utoaji wa ajira.

“Sekta hii inachangia takribani asilimia 85 ya pato la mkoa wa mujibu wa wasifu wa kiuchumi na kijamii wa mkoa wa mwaka 2013,” alisema.

Alisema lengo la mkoa ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na chakula cha kutosha, kipato cha kaya kinaongezeka na kilimo kwa kusaidiana na viwanda vinaendelea kuwa muhimili mkuu wa uchumi.

Alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, mkoa ulikuwa na jumla ya viwanda 695 kati yake vikubwa vikiwa 24, vya kati 35, vidogo 149 na vidogo zaidi 1,995.

“Sekta hii ya viwanda inaajiri watu takribani 15,000 sawa na asilimia 1.6 ya wakazi wa mkoa wa Iringa kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012,” alisema.

Akizungumzia kampeni ya uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda mkoani humo kama sehemu ya utekelezaji wa azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda, alisema kila halmashauri inatakiwa kujenga viwanda visivyopungua 35 mwaka huu.

Katika kufanikisha azma hiyo alisema mkoa umeunda timu ya uratibu yenye wajumbe 18 wakiwemo wataalamu kutoka vyuo vikuu vya mkoani Iringa, sekretarieti ya mkoa pamoja na sekta binafsi.



MJUMBE WA HALMASHAURI KUU CCM TAIFA SALIM ASAS AIKABIDHI UWT KILOLO MILION 5 KWA AJILI YA UJENZI WA UKUMBI

Posted by Esta Malibiche on februari 26,2018 in SIASA

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa,ambae pia ni Mnec wa Mkoa wa wa IRINGA Salim Asas akimkabidhi Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilolo, kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa UWT wilayani humo.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ccm Taifa Saalim Asas,ambae pia ni Mnec wa Mkoa wa Iringa,akizungumza katika ofisi za ccm wilaya ya Kilolo .Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Kilolo akifuatiwa na Katibu wa ccm Wilaya ya Kilolo na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Uwt wilaya ya Kilolo
Katibu wa uwt wilaya ya Kilolo,akipeana mkono kuashiria kumshukuru Mjumbe wa Halmashauri kuu ccm Taifa Saalim Asas,kwa mchango wake alioutoa kufanikisha zoezi la ujenzi wa ukumbi  wa UWT linakamilika.

WAHAMIAJI HARAMU 83 WAKAMATWA IRINGA WAKIWA HOI

Posted by Esta Malibiche on Fbruari 26,2018

 Wahamiaji  haramu waliokamatwa Iringa

WAHAMIAJI haramu 83 wamekamatwa na idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Iringa jana huku baadhi yao wakiwa katika hali mbaya baada ya kukosa chakula siku tatu.

Akizungumza mara baada ya kuwafikisha katika kituo cha Polisi mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji  Mkoa wa Iringa, Hope Kawawa ,alisema wahamiaji hao walikamatwa katika maeneo ya kijiji cha Mbigili wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wakiwa katika roli aina ya Scania baada ya kupata taarifa kutoka raia wema.

Kawawa alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo walifanikiwa kulikamata roli hilo lenye namba  T903 AKH mali ya Gabriel Mwakyambiki mwenyeji wa Tukuyu ambapo dereva alifanikiwa kukimbia na kulitekeleza roli hilo kijiji cha Mbigili.

Alisema wahamiaji hao walikamatwa majira ya saa  kumi na moja juzi jioni na maafisa wa uhamiaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi hivyo wakiwa katika hali mbaya ambapo wengi wao walionekana wakiwa hawajapata chakula hali iliyolazimu kuwapatia kwanza huduma ya kwanza hadi hali zao zitakapotengemaa.

Alisema Kawawa alisema kuwa baada ya wiki iliyopita kuwakamata wahamiaji wanne waliendelea kufanya doria na kufanikiwa kuwakamata wahamiaji 83 juzi ambao watawafikisha mahakamani mara baada ya hali zao kuwa njema.

Aidha alitoa wito kwa wanaofanya biashara ya kuwasafirisha wahamiaji hao kuwa kwa sasa mkoa wa Iringa si mahala pa kupitisha wahamiaji bali wataendelea kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahamiaji wote watakaogundulika mkoani hapo na wako kazini kwa masaa ishirini nne.


“Naomba niwaambie madalali wanaosafirisha hawa wahamiaji mkoa wa Iringa sio mahala salama kabisa kuwapitisha hao watu kwani tuko makini masaa 24 na pindi tukiwabaini hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa kufanya biashara ya  kuwasafirisha wahamiaji hivyo wasitarajie watapita mkoa wa Iringa bila kuwakamata” alisema

Kawawa alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na idara ya uhamiaji kwa kutoa taarifa pindi wanapohisi baadhi ya watu sio raia wa Tanzania na watu wasiowajua kwenye vyombo vya usalama ili wachunguzwe na kuchukuliwa hatua madhubuti.
 
Kwa  upande  wake  mkuu wa mkoa  wa  Iringa Amina Masenza ambae  ni  mwenyekiti  wa kamati ya  ulinza  na usalama mkoa  wa  Iringa akizuingumza  baada ya kuwatembelea  wahamiaji  hao  ambao baadhi  yao wamelazwa katika Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa  Iringa alisema kuwa mkoa  wa  Iringa umejipanga  kiusalama  na  kuwa  si rahisi  kwa  wahamiaji  kuvuka  ndani ya  mkoa  huo .

wahamiaji haramu raia wa Ephiopia wanaswa Iringa wakisafirishwa kwenye Lori 


Wahamiaji hao wakiwa hoi

WAKULIMA WATAKIWA KUACHA KULIMA KILIMO KWA MAZOEA

Posted by Esta Malibiche on februari 26.2018 in News


Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (watatu kushoto) akishangaa gari la Benki la NMB lenye ATM ikiwa na Benki ndani yake huku Huduma za kibenki zikiendelea katika stendi ya mabasi yaendao mikoani mjini IRINGA baada ya kuzindua tawi jipya la NMB Ruaha Ijumaa wiki iliyopita. (Picha na Friday Simbaya)





IRINGA: 
Wakulima mkoani Iringa wametakiwa kuzitumia taasisi za kifedha mkoani humo kwa kuchukua mikopo nafuu ili kulima kilimo chenye tija na kukuza uchumi wao badala ya kulima kilimo cha mazoea hali inayopelekea kushuka kwa uchumi wao. 

Imeelezwa kuwa moja ya sababu inayochangia wakulima wengi kushindwa kulima kilimo cha kitaalamu ni ukosefu wa mitaji hali inayopelekea kuendelea kulima kilimo kwa mazoea 

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa iringa amina masenza hivi karibuni wakati akazindua tawi jipya la bank ya NMB Ruaha ambalo linatajwa kupunguza msongamano wa wateja huku akiwataka wananchi kuendelea kuzitumia taasisi hizo kwa kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla. 

Masenza alisema ili mkulima ajikwamue kiuchumi anapaswa kulima kilimo cha kisasa tofauti na ilivyozoeleka kwa wakulima wengi huku akizitaka taasisi za kifedha nchini kutoa kipaombele kwa wakulima. 

upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Biashara NMB Abdulmajid Nsekea aliwataka wanawake na vijana ambao wapo katika vikundi vya ujasiliamali kuchangamkia fursa ya mikopo inalotolwa na benki hiyo. 

Alisema uzinduzi wa tawi jipya la bank ya NMB Ruaha litakupunguza msongamano wa wateja katika benki ya Mkwawa, huku akiwataka wananchi kuendelea kuzitumia taasisi hizo kwa kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla. 

WATOTO 6 WAWASHIWA VIFAA VYA USIKIVU (COCHLEAR IMPLANT)

Posted by Esta Malibiche on februari 26,2018

0001
Mtaalam wa Huduma ya Usikivu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Mathayo Majogoro Alfred (katikati) akiunganisha kifaa cha usikivu cha nje na cha ndani ili mtoto Matilda Katobesi aweze kusikia kwa mara ya kwanza. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Koo na Masikio, Dkt. Edwin Liyombo akifuatilia na kushoto ni mama wa mtoto huyo, Angelina Cosmas.
0002
Mtoto Matilda kwa mara ya kwanza leo tarehe 24, Januari, 2018 akianza kutamka baadhi ya maneno baada ya kufundishwa na mtaalamu wa sauti kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili.
0003
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Koo na Masikio, Dkt. Edwin Liyombo wa Muhimbili akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwasha kwa mara ya kwanza vifaa vya usikivu kwa watoto waliofanyiwa upasuaji na kupandikizwa vifaa hivyo katika hospitaili hiyo. Kuanzia kushoto ni Mkuu wa Idara ya Macho, Dkt. Baruani, Katibu wa Umoja wa Watoto na Wazazi Wanaonufaika na Vifaa vya Usikivu nchini, Bupe Mwakalambile na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Wateja, Bwana Aminiel Aligaesha.
????????????????????????????????????
Wazazi wakisubiri kuashwa kwa mara ya kwanza kwa vifaa vya usikivu katika hospitali hiyo.
0005
Mtaalamu wa Sauti, Fayaz Jaffer akionyesha kifaa cha usikivu (Cochlear Implant) kwa waandishi wa habari ambacho kinapandikizwa kwa mtoto mwenye tatizo la kusikia. Kulia ni Paul Khalil kutoka Kampuni ya Medel. Kuanzia kushoto ni Dkt. Edwin Liyombo, Dkt. Baruani, Bi. Bupe Mwakalambile na  Bwana Aminiel Aligaesha wakiwa kwenye mkutano huo leo.
????????????????????????????????????
Wazazi wa watoto wenye matatizo ya kusikia wakiwa kweny mkutano huo leo.
PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

………………..

Dar es salaam                                                                                           
Watoto sita ambao wamewekewa vifaa vya usikivu Januari mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wameanza kusikia kwa mara ya kwanza baada ya kuwashiwa vifaa hivyo.
Kuwashwa kwa vifaa hivyo kumeleta furaha kwa wazazi kwani wameshuhudia watoto wao wakisikia sauti kwa mara ya kwanza na hivyo kuwajengea matumaini ya watoto hao kuanza maisha mapya.
Zoezi la kuwawashia vifaa hivyo (Switch On) limefanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  kwa kushirikiana na wataalaam kutoka Medel Austria ambao ndio wasambazaji wa vifaa hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari , Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Pua,  Koo na Masikio Dkt. Edwin Liyombo amesema watoto hao walifanyiwa upasuaji wa upandikizaji kifaa cha usikivu Januari mwaka huu ambapo zaidi ya asilimia 80 ya upasuaji huo ulifanywa na watalaam wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .
 ‘’Watoto hawa wataanza maisha mapya ya kusikia sauti mbalimbali katika mazingira yanayowazunguka baada ya kuunganisha vifaa hivi na kuviwasha’’. Amesema Dkt. Liyombo
Akifafanua amesema mbali na watoto hao sita lakini pia watoto wengine watano ambao walifanyiwa upasuaji huo mwaka jana  na  wengine sita  ambao walifanyiwa upasuaji huo nchini India nao wamekuja kufuatiliwa maendeleo yao ili kubaini changamoto zinazowakabili  na kupewa ushauri wa kitaalam. 
Akielezea ukubwa tatizo  Dkt. Liyombo amesema takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinaonesha kuwa katika watoto 1,000 wanaozaliwa,  inakadiriwa kuwa watoto watano wanazaliwa na tatizo kubwa la usikivu .
Pia amesema MNH ipo kwenye mchakato wa kuanzisha utaratibu wa kuwachunguza watoto wachanga ili kubaini mapema wenye matatizo yakutosikia.
Kwa upande wake Muwakilishi kutoka Medel Fayaz Jafar amesema upasuji huo umekua na mafanikio makubwa kwakua  katika awamu hiyo kumekua na mabadiliko  kwani asilimia kubwa  ya upasuaji umefanywa na watalaam wa MNH  na kwamba hatua hiyo ni ya kuridhisha.
Huduma ya Upandikizaji wa kifaa cha usikivu (Cochlear Implant) ilizinduliwa Juni 7 , 2017 na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu hivyo Tanzania imekuwa nchi ya pili kutoa huduma hiyo katika nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Kenya. Aidha Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo  kupitia Hospitali ya Umma ambayo ni Muhimbili yenye hadhi ya ubingwa wa hali ya juu.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI NACHINGWEA ASUBUHI YA LEO

Posted by Esta Malibiche on februari 26,2018 in News

PMO_0092
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili kwenye  uwanja wa ndege  wa Nachingwea kuanza ziara ya kazi mkoani Mtwara Februari 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SUGU NA MASONGA:-WAHUKUMIWA MIEZI 5 JELA KWA KOSA LA UCHOCHEZI

Posted by Esta Malibiche on februari 26,2018 in NEWS

index
Mhe Joseph Mbilinyi(SUGU), mbunge wa Mbeya Mjini na Ndg Emmanuel Masonga-Katibu wa kanda ya Nyasa Chadema WAMEHUKUMIWA KWENDA MIEZI 5 JELA kwa kosa la uchochezi.
Kwa madai kwamba ktk mkutano huo wa hadhara Mhe SUGU alisema ” Mhe Rais Magufuli hawezi kupendwa na watu kwa kumshoot risasi Lissu, kumtupa Jela miezi minne Lema, kumteka Ben saanane, kumteka Roma na kumzuia SUGU asiongee..!

MADINI YOTE NCHINI NI SHARTI YA WANUFAISHE WATANZANIA

Posted by Esta Malibiche on Februari 26,2018 in News


Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Aliyenyoosha mkono) akimuonyeshaNaibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko mitambo ya uchimbaji madini  alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji madini ya makaa ya mawe alipotembelea mgodi wa Edenville Tanzania Ltd uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Kulia) akimueleza Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko juu ya uchimbaji wa makaa ya mawe alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Rukwa

Serikali imesema kuwa sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza wazi kuwa Madini yote nchini ni Mali ya watanzania hivyo wanapaswa kutambua umuhimu wa rasilimali.

Wawekezaji na wachimbaji wote wa madini nchini wanapaswa kutambua kuwa wanalo jukumu muhimu la kurejesha kwa jamii asilimia chache ya kile wanachozalisha kwa kuunga mkono juhudi za serikali Back to the Community) katika kuboresha miundombinu, sekta ya elimu, afya N.K

Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko amesisitiza hayo Leo 23 Februari 2018 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe Mkoani Rukwa Magharibi mwa Tanzania.

Mradi huo unaosimamiwa na kampuni ya Edenville Tanzania Ltd kwa ubia na kampuni ya Edenville Energy of Uk na Upendo Group (Kampuni ya kizawa) ilianza shughuli za majaribio ya uchimbaji na uoshaji mwezi wa kumi mwaka Jana 2017 na mkaa wa kwanza kuuzwa kwa majaribio ni mwezi Novemba mwaka 2017.

"Nataka niwajulishe tu watanzania wenzangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliniteua kusimamia Wizara ya Madini nikimsaidia Waziri wetu Mhe Anjelina Kairuki ili kuboresha sekta hii ya Madini hatimaye kuwanufaisha watanzania kuliko ilivyokuwa awali ambapo Madini yalikuwa yanachimbwa nchini lakini faida inaenda nchi zingine" Alisema Mhe Biteko na Kuongeza kuwa

Wawekezaji hao wanapaswa kutoa ajira zisizo za utaalamu kwa wananchi wanaozunguka migodi yao sambamba na watanzania wote huku akiwaagiza kuwaajiri wataalamu wa Madini wa ndani ya nchi kwa kazi ambazo wanaweza kuzifanya sio kuajiri wageni.

Aidha, aliwasisitiza wananchi hao pindi wanapopata ajira zao katika migodi mbalimbali wanapaswa kuwa waaminifu ili kuwavutia wawekezaji hao jambo litakalopelekea wawekezaji kuwa na imani na watanzania na hatimaye kuongeza chachu ya ajira nyingi zaidi.

Sambamba na hayo amekemea baadhi ya wafanyakazi katika migodi mbalimbali ambao wameaminiwa na kupatiwa ajira lakini wanageuza muda wa kazi kuwa muda wa starehe kwa kunywa pombe na utoro kazini.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Rukwa kutembelea na kukagua uchimbaji wa Madini.

MWISHO.