Kwa Habari za kitaifa na kimataifa

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za michezo na burudani

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za afya

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za Kilimo

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za uchumi na biashara

Tembelea Kali ya habari

Kwa habari za elimu

Tembelea Kali ya habari

Ijumaa, 30 Juni 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 57 MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 30, 2017.

Posted by Esta Malibiche on JUNE 30,2017 IN SIASA

PIX 4 Mhe.Mwigulu
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.

PIX 1.1 Mhe.Ndugai
Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai  akiongoza    kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 2 Mhe.Jafo
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Mhe,Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 3 Mhe.Wambura
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.

PIX 5 Mhe.Kamwelwe
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge   katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 6 Mabula
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge    katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 7 Mhe.Ngonyani
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Eng,Edwin Ngonyani  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge  katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 8 Mhe.Simbachawene
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.George Simbachawene  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge  katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 9 Mhe.Cosato
Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe.Cosato Chumi akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 10 Mhe.Bashungwa
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk.Ashatu Kijaji akiteta jambo na Mbunge wa Karagwe Mhe.Innocent Bashungwa katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 11 Mhe.Shally
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Shally Raymond akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 12 Mhe.Mwanjelwa
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe.Dk Mary Mwanjelwa akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 13 Mhe.Mwantakaje
Mbunge wa Bububu Mhe.Mwantakaje Juma akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
PIX 14 Washindi wa medali za dhahabu
Washindi wa Medali za Dhahabu katika Mashindano ya Kimataifa ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika nchini Marekani Kutoka kushoto Ndg.Rashid Kikwete,Kassi Juma Nkamia na Abdallah Rubeya wakiwa bungeni kujifunza shughuli balimbali za  Bunge.
PIX 15 Mhe.Maghembe na Mbatia
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe akimsikiliza Mbunge wa Vunjo Mhe.Eng.James Mbatia  katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.

Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA UMOJA WA WANAMICHEZO WA MPIRA WA MIGUU KUTOKA FC GRACE UNITED STATES LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

Posted by Esta Malibiche on JUNE 30,2017 IN MICHEZO

unnamed
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kulia ni Mwenyeji na kiongozi wa Msafara Bishop Oscar John.
1
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Mheshimiwa William Ngeleja akizungumza wakati Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
3
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akimsikiliza Bishop Oscar John (aliesimama) akizungumza, pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
6
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (katikati) na Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo (kushoto) uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
3
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Medali za Dhahabu katika Mashindano ya kimataifa ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika hivi karibuni nchini Marekani. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Wavulana ya Feza Ndg. Ibrahim Rashid, anaefuata ni Ndg. Rashid Kikwete, kulia ni Mhe. Hawa Ghasia, wa pili kulia ni Ndg. Kassi Nkamia na watatu kulia ni Ndg. Abdallah Rubeya, waliotembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
4
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (kushoto waliokaa) baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
5
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimsikiliza Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania  Ndg. Mwadini Jecha (katikati) pale ugeni kutoka Chama  hicho ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kushoto ni Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo.


Viongozi wa Dini Wabebeshwa mzigo, Utunzaji wa Mazingira.

Posted by Esta Malibiche on JUNE 30.2017 
2
 Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo katoliki Musoma Mkoani Mara akiongea na Waandishi wa habari nje ya Mkutano huo kuelezea umuhimu wa mazingira.
unnamed
Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, akifungua kikao hicho, pembeni kulia ni Mratibu wa LVEMP Bw. Omari Myanza.
1
Baadhi ya Viongozi wa dini kutoka mkoa wa kagera wakiwa katika Warsha hiyo.
2
Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo katoliki Musoma Mkoani Mara akiongea na Waandishi wa habari nje ya Mkutano huo kuelezea umuhimu wa mazingira.
3
Sheik Hassan Kabeke, akiafafnua jambo kwa waandishi wa habari nje ya Warsha hiyo namna suala la mazingira linavyo tajwa katika Kuran tukufu.
4
Sheik Hassan Kabeke, akiafafnua jambo kwa waandishi wa habari nje ya Warsha hiyo namna suala la mazingira linavyo tajwa katika Kuran tukufu.
5
Mratibu wa LVEM Akitoa maelezo ya awali kabla yakuanza kwa Warsha hiyo ilikutanisha Viongozi wa Serikali na Dini katika baadhi ya Mikoa ya kanda ya ziwa (Picha zote na Ofisi ya mkuu wa Mkoa Mwanza).
…………………………
Na Atley Kuni- Mwanza.
Serikali mkoani hapa, imewapa jukumu kubwa viongozi wa dini kutoka baadhi ya  mikoa ya kanda ya ziwa kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega katika kulitunza ziwa Viktoria na Maliasili zake ili liweze kuwa tegemeo kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Akifungua Semina ya siku moja mkoani hapa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, na risala yake kusomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, Mongella amesema, viongozi wa dini wanalo jukumu kubwa kwani wao husimamia imani za watu. “Ninyi Viongozi wa dini dhima mliyonayo ndani ya jamii ni kubwa sana na chochote mtakacho waelekeza waumini wenu lazima waweze kukitekeleza, hivyo niwaombe sana viongozi wangu tulilinde ziwa viktoria kwa jitihada zetu zote’’ alisema Mongella.
Aidha Mongella amesema kuwa, kuwepo kwa Ziwa Victoria ni fursa ya uendelezaji ya kauli mbiu ya “Tanzania ya Viwanda” ambayo Serikali ya awamu ya Tano inasisitiza,  “Ziwa hili linasaidia upatikanaji wa rasilimali zinazotumika kwa matumizi ya nyumbani na viwandani, usafiri na usafirishaji na uzalishaji wa nishati ya umeme Hivyo basi hatuna budi kuhifadhi mazingira ya Ziwa na Bonde lake” amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Kwa upande wao, viongozi wa dini wakiongea wamesema, wao wanatambua na hata vitabu vya dini vinaelekeza juu ya mwanadamu anachopaswa kufanya katika kulinda mazingira ikiwepo ziwa Viktoria.
Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya amani ya madhehebu ya dini katika Mkoa wa Mwanza, Sheik Hassan Kabeke, amesema katika Uislam  na hususan ni katika mafundisho ya Mtume Muhama S.A.W,  inafafanua juu ya mito miwili yaani mto Nile na Furabu ambayo mtume aliipitia huku akisema kwamba, Mto Nile ambao unafungamanishwa na Ziwa Viktoria Mtume amesisitiza kuyatunza mazingira, “Katika kupanda miti kwenye uislamu mtu hupata thawabu, tunaimani kabisa kwamba kila mmoja wetu akitunza mazingira ni sehemu ya Ibada, amesema Kabeke.
Naye Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki la Musoma, kwa upande wake amesema kwa habari ya mazingira, tunaona ni jukumu la jamii nzima bila kujali itikadi zetu “ Kukutana kwetu hapa tunataka kuangalia nikwa namna gani tutaziangazia sababu za kiuchumi na kijamii, alisema Msonganzila na kuongeza kwamba kwa sasa wao katika Mkoa wa Mara wanayo kampeni kwenye eneo la Serengeti ambayo wanaendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa Utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya hali ya nchi.
Mradi wa Hifadhi ya Mazingira wa Ziwa Victoria (LVEMP II) utakamilika mwezi Disemba, 2017, aidha warsha hiyo ni kati ya warsha nne zilizoandaliwa na Mradi kwa madhumuni ya kukusanya maoni ya wadau ambayo yatawezesha kuandaa awamu ijayo ya Mradi inayotarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2018.
Kikao hicho kimewakutanisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Viongozi wa dini kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu na Mara.

JNIA TBIII Kuanza Kutumika Dec 2018-Mhe. Mbarawa

Posted by Esta Malibiche on JUNE 30,2017 IN NEWS

unnamed Prof. Ninatubu Lema, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa  (wa tatu kutoka kulia), leo wakati akianza ziara ya kutembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TBIII).
1Meneja wa Mradi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Ray Blumrick (kushoto) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye ujenzi wa jengo hilo, ambapo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbarawa (wa tatu kutoka kushoto) akimsikiliza kwa makini.
2Mhandisi Simba Charles (aliyenyoosha mkono) akionesha eneo la maegesho ya magari kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), leo alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
3
Bw. Ray Blumrick,  Meneja Mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) akimwelekeza namna paa lilivyo imara, Prof. Makame Mbarawa (Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano) aliyetazama juu katikati  wakati wa ziara yake kwenye jengo hilo leo.
4Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Prof Ninatubu Lema akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa pili kutoka kushoto) leo alipofanya ziara ya kutembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa TAA, Bw. Richard Malulu.

WAHALIFU WANNE WAUWAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI KIBITI

Posted by Esta MALIBICHE ON june 30,2017 in NEWS
unnamed
MKUU WA OPERESHENI ZA POLISI, NAIBU KAMISHNA DCP LIBERATUS SABAS, AKIONYESHA BUNDUKI AINA YA SMG ZILIZOPATIKANA JUZI USIKU WAKATI WA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI  BAINA YA WAHALIFU NA POLISI KATIKA KIJIJI CHA PAGAE WILAYANI KIBITI MKOANI PWANI. BUNDUKI 2 AINA YA SMG ZILIPATIKANA PAMOJA NA MAGAZINI 2 NA RISASI 17. PICHA NA HASSAN MNDEME-JESHI LA POLISI.
……………………..
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji  katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.
 
Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.
 
Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu  na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.
 
“Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji” Alisema Sabas.
 
Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.
 
Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
1 2

JUMUIYA YA WAZAZI Z’BAR YASISITIZA UADILIFU KWA WATENDAJI WAKE.

Posted by Esta Malibiche on JUNE 30,2017 IN SIASA
unnamed
Naibu Katibu Mkuu wa  Jumuiya ya Wazazi CCM Zanzibar, Nagma Giga akizungumza na Watendaji na viongozi wa jumuiya hiyo wa ngazi za Mikoa na Wilaya mara baada ya kuwakabidhi komputa.
1
Naibu Katibu Mkuu wa  Jumuiya ya Wazazi CCM Zanzibar, Nagma Giga akimkabidhi komputa Katibu wa Wazazi Mkoa wa Kaskazini Bi.Zaituni Bushiri Ussi.
2
Baadhi ya Komputa zilizokabidhiwa kwa Makatibu wa Mikoa na Wilaya jumuiya ya Wazazi za Zanzibar.
…………………….
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
JUMUIYA ya Wazazi ya CCM Zanzibar imewataka watendaji wake wa ngazi mbali mbali za jumuiya hiyo kuwa waadilifu wakati wa kuchuja majina ya wagombea wanaowania nafasi mbali mbali za uongozi kupitia uchaguzi unaoendelea ndani ya chama na jumuiya zake.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Bi.Nagma Giga wakati akikabidhi vitendea kazi ambavyo ni komputa na priter kwa Mikoa na Wilaya nane za jumuiya hiyo huko katika Afisi Kuu ya Wazazi Mpirani Kikwajuni Unguja.
Alisema watendaji wa ngazi za mikoa na wilaya za jumuiya hiyo ndio wasimamizi wakuu wa uchaguzi huo kwa ngazi mbali mbali za jumuiya hivyo wakati wa kuchuja wagombea ni lazima waweke kando urafiki na undugu na wawapitishe viongozi wenye sifa na uzalendo wa kukisaidia chama kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.
“Mafanikio tuliyonayo ndani ya jumuiya yrtu yanatokana na juhudi zenu za kiutendaji hivyo nakupongezeni sana na muendelee na kasi hiyo hiyo hadi tupate viongozi imara watakaotetea maslahi ya CCM mwaka 2020”,.alisema Giga.
 Aidha aliwasisitiza viongozi hao kuhakikisha wanatunza vizuri vifaa walivyopewa na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kurahisisha shughuli za kiutendaji za jumuiya.
Akitoa neno la shukrani Katibu wa Wazazi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bi.Zaituni Bushiri Ussi aliahidi kuwa vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya kuharakisha maendeleo ya taasisi katika harakati za kiutendaji.
Naibu Katibu Mkuu huyo ametoa Komputa nane zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa Mikoa na Wilaya zote za Jumuiya hiyo Zanzibar ili kukamilisha ahadi alizotoa katika ziara zake visiwani humo.
Komputa hizo zimetolewa kwa Mkoa Kaskazini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkoa wa Kusini Pemba, Wilaya ya Kaskazini “A”, Wilaya ya Dimani, Wilaya ya Amani na Wilaya ya Amani.

SPIKA WA BUNGE NDUGAI AKIFATILIA KWA UMAKINI MISWADA YA MALIASILI

Posted by Esta Malibiche on JUNE 30,2017 IN NEWS.

2
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Pamoja iliyokuwa ikijadili miswada miwili ya sheria  kuhusiana na usimamizi wa maliasili za Nchi.kikao hicho kilifanyika Mjini Dodoma jana Katika Ukumbi wa Msekwa.

unnamed
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Pamoja iliyokuwa ikijadili miswada miwili ya sheria  kuhusiana na usimamizi wa maliasili za Nchi.kikao hicho kilifanyika Mjini Dodoma jana Katika Ukumbi wa Msekwa.
1
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Pamoja iliyokuwa ikijadili miswada miwili ya sheria  kuhusiana na usimamizi wa maliasili za Nchi.kikao hicho kilifanyika Mjini Dodoma jana Katika Ukumbi wa Msekwa.

WAZIRI UMMY APOKEA TAARIFA YA WATOTO MAPACHA.

Poted by Esta Malibiche on JUNE 30,2017 IN NEWS

1
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakijadili kwa umakini na katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wakiongea na waandishi wa habari(Hawapo kwenye picha) juu ya taarifa ya kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi. Hasma Juma katika hospitali ya Temeke jijini Dar Es salaam.
2
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. BaKari Kambi akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari (Hawapo kwenye picha) wakatati wa uwasilishwaji wa taarifa ya tuhuma za kuibiwa kwa mtoto  mmoja wa Bi Hasma Juma uliofanyika mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
3
Waandishi wa habari wa vituo tofauti wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa taarifa ya tuhuma za kuibiwa mtoto mmoja wa Bi Hasma Juma uliowasilishwa leo na mwenyekiti wa kamati Dkt. Charles Majige ambae pia ni Daktari bingwa wa Magonjwa yakina mama , uliofanyika leo mapema katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akijibu maswali yaliyoulizwa na Waandishi wa Habari juu ya tuhuma za kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi.Hasma Juma katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam.


………………………..
NA WAMJW DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea taarifa kutoka kwa tume huru aliyoiunda ili kuchunguza malalamiko ya Bi. Asma Juma kuhusu kuibiwa mtoto mmoja kati ya mapacha wawili katika hospitali ya Rufaa ya Temeke Dar es salaam.
Akipokea taarifa  kutoka kwa Mwenyekiti wa tume hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama Dkt. Charles Majige  Waziri Ummy amesema kuwa Bi. Asma Juma(29) hakuwa na watoto mapacha kama ilivyodaiwa na mlalamikaji huyo kutokana na kipimo cha Utra sound kukosea katika uchukuaji picha ya mtoto akiwa tumboni.
“Nimepokea taarifa kutoka kwa tume huru niliyoiunda hivi karibuni na imethibitisha kuwa Bi. Asma Juma hakuwa na watoto mapacha ila uchukuaji mbaya wa picha ya mtoto aliyekuwa tumboni uliofanywa katika zahanati ya Huruma ukatoa matokeo hayo” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wanafamilia ya Bi. Asma wanatakiwa kumfariji ndugu yao na sio kumkumbushia jambo hili mara kwa mara kwani litamharibu kisaikolojia na kushindwa kutekeleza wajiu wake kwa mtoto kama mama mzazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Charles Majige Amesema kuwa Bi. Asma aliamini hivyo kwa sababu Hospitali ya temeke hawakumchukua vipimo vya picha bali walitumia taarifa ya vipimo vya awali .
Aidha Dkt. Majige Amesema kuwa tume hiyo imebaini kuwa Bi. Asma hakuibiwa mtoto na alikua hana mapacha kwa sababu uzito wake ulikua sio wa kubeba watoto wawili na katika chumba cha upasuaji kulikua na wataalamu 6 kutoka vitengo mbalimbali.
Kwa upande wake mwakilishi wa Familia ya Bi. Asma Juma Jordan Jaddah amesema kuwa anaishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kufatilia jambo hilo kwa ukaribu na kupata ukweli wa malalamiko yao na wameikubali taarifa hiyo .
“Tunaipongeza tume hiyo chini ya Wizara ya Afya na tunashukuru kwa msaada wao mwanzo mpaka mwisho na kutupatioa majibu ya kuridhisha nasi tutakuwa bega kwa bega katika kumfariji ndugu yetu kwa jambo hili lilitokea” alisema Bw. Jaddah.
Mbali na hayo Waziri Ummy amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa maagizo ya kila mtoto wa kike atakaepata ujauzito shuleni asirudi shuleni ila aendelee na masomo mengine ya ujuzi.

SERA YA MAENDELEO YA MICHEZO YA MWAKA 1995 YAFANYIWA MAREKEBISHO KUENDANA NA MAHITAJI YA SASA.

Posted by Esta MALIBICHE ON june 30,2017 IN MICHEZO
PIX 3 Mhe.Wambura
Na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo imesema kuwa inakamilisha mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Michezo ya mwaka 1995 ili kuhakikisha inaendana na mahitaji ya sasa katika maendeleo ya michezo nchini.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura wakati akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe.Cosato Chumi aliyetaka kujua mipango ya Serikali katika kufufua mchezo wa Riadha Bungeni Mjini Dodoma leo.
“Serikali kwa kushirikiana na wadau inatekeleza programu mbalimbali za kuendeleza  mchezo wa riadha nchini ikiwemo Kilimanjaro Marathon,Bagamoyo Marathon,Heart Marathon na Tulia Marathon ambayo hushirikisha wanariadha kutoka nje”,Aliongeza Mhe.Wambura.
Aidha pamoja na hayo Mhe.Wambura amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia  pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI imeendesha mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA  ambayo pamoja na mambo mengine yanalenga kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wetu katika mchezo wa riadha.
Akizungumzia suala la miongozo ya Kiserikali amesema kuwa Wizara yake inakamilisha taratibu za kuandaa miongozo ya kiserikali ili kuwezesha wadau wote kuendesha  shughuli  zao katika mazingira ya weledi na stadi bora za michezo.
Hata hivyo Naibu Waziri uyo amesema kuwa nchi yetu imeanza kufanya vizuri katika mashindano ya Riadha kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma kupitia kwa wanariadha wake kama Francis Naal,Samson Ramadhani,Gidamis Shahanga,Juma Ikangaa,Suleiman Nyambui na Filbert bayi na hivyo kuitangaza nchi yetu.
“Nchi yetu kwa sasa imeanza kupata mafanikio katika riadha kupitia wanariadha wetu kama Alphonce Simbu aliyeshinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya standard Chartered Mumbai Marathon,Cecilia Ginoka Panga aliyeshinda Beijing International Half Marathon na Giniki Gisamoda aliyeshinda Shanghai International Half Marathon,wote hawa wanaitangaza nchi yetu vizuri na kuifanya ifahamike na hivyo kuvutia watalii ”Alisisitiza Mhe.Wambura.

MAEGESHO YA KIVUKO LINDI KUKAMILIKA MWEZI NOVEMBA MWAKA HUU

Posted by Esta Malibiche on JUNE 30,2017 IN NEWS
unnamed
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS). Mkoa wa Lindi,Eng. Issack Mwanawima (mwenye koti la draft), akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa maegesho hayo, Mkoani humo, wakati Waziri huyo alipotembelea mradi huo hivi karibuni.
1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akiangalia ujenzi wa wa maegesho ya kivuko unaojengwa katika mkoa wa Lindi alipotembelea mradi huo hivi karibuni. Mradi huo utahusisha maegesho ya kivuko na ujenzi wa mita 150 za barabara ya lami upande wa Kitunda.
2
Tinga Tinga likiendelea na ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani lindi. Ujenzi wa maegesho hayo unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
3
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara (katikati), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), eneo la gati ya Lindi ambalo litatakiwa kuchimbwa ili kuongeza kina cha gati hilo, alipotembelea gati hiyo hivi karibuni.
4
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Eng. Juma Kijavara (katikati), akifafanua jambo kwa  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), wakati Waziri huyo alipotembea alipotembelea gati la Lindi kuona hatua mbalimbali za utekelezaji wa upanuzi wa gati hiyo hivi karibuni.
5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akienda kuangali sehemu ya kwanza ya upanuzi wa gati la Lindi ambalo kwa sasa linatakiwa kuongezewa kina ili meli kubwa ziweze kutia nanga.

…………………..
Serikali imesema ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani Lindi utakamilika mwezi Novemba mwaka huu ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa wakazi wa eneo la Kitunda Mkoani Lindi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi  wa maegesho hayo na kusema ujenzi huo umegharimu kiasi cha Tsh, bilioni 1.8 ambazo zitahusisha maegesho ya Kivuko na kujenga barabara ya kiwango cha lami mita 150 upande wa Kitunda Mkoani Lindi.
‘Tuliahidi na sasa tunatekeleza, nimefurahi kuona ujenzi unaendelea vizuri na ninawahakikishia mwezi Novemba tutakuja kuzindua kivuko’ alisema WazirI Profesa Mbarawa.
Aidha,Waziri Mbarawa amemtaka Mkandarasi anaejenga magesho hayo kuzingatia thamani ya fedha wakati wa ujenzi wake ili mradi huo uweze kudumu kwa muda mrefu.
‘hakikisha unajenga maegesho haya kwa kuzingatia viwango tulivyokubaliana, hatutaki kuona kasoro mara tu baada ya mwezi mmoja, hizi ni fedha za walipa kodi na tunategemea miundombinu hii ikae  muda mrefu’ alisisitiza Waziri Prof. MBARAWA.
Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads), mkoa wa Lindi, Eng. Issack Mwanawima amemuhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa watasimamia mradi kwa kuzingatia viwango katika ujenzi huo na kuhakikisha unakamilika kama mkataba unavyosema.
Katika hatua nyingine Waziri Profesa Mbarawa amekagua maendeleo ya ujenzi wa Gati la Lindi na kusema kuwa Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuongeza kina cha Gati hiyo mara baada ya kutokea changamoto ya upana wa Gati hiyo kuwa mdogo.
‘Baada ya kujenga sehemu iliyopo sasa tuligundua kuwa bandari inatakiwa kuongezwa kina hivyo tukalazimika kufanya usanifu upya ili tuongeze upana wa mita 60 mpaka 500kwa eneo lote vinginevyo meli zisingeweza kufunga nanga’ alisisita Waziri Prof Mbarawa.
Waziri Prof. MBARAWA aliongeza kuwa lengo la Serikali katika kufanya usanifu upya ni kuhakikisha Gati ya Lindi inakidhi mahitaji halisi na kuchochea uchumi wa mkoa huo.
Kwa upande Meneja Bandari ya Mtwara Eng. JUMA Kijavara amesema Mamlaka ya Bandari Nchini TPA imejipanga na iko katika hatua za mwisho za mazungumzo na Mkanadarasi ili aanze kazi hiyo.
Mradi wa upanuzi wa Gati la Lindi utahusisha miradi ya Gati hiyo, Bandari ya Lushungi pamoja na bandari ya Kilwa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano