Jumamosi, 30 Desemba 2017

MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA RUKIA MUWANGO AWATAKA WANANCHI KUZITUMIA FEDHA ZA KOROSHO KWA UANGALIFU

Poated by Esta Malibiche on DEC 30. 2017 IN NEWS

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Mh.Rukia Muwango akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ruponda mapema leo hii katika zoezi la usafi wa Mazingira 
 MKUU wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Rukia Muwango amewataka wananchi kuwa makini na matumizi ya fedha za korosho ili ziweze kuwasaidia katika kuboresha maisha yao pamoja na kusomesha watoto.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo hii Katika kijiji cha Ruponda mara baada ya   zoezi la usafi  wa Mazingira lililofanyika katika kijiji hicho,  alipoungana na wananchi kusafisha Mazingira ikiwa ni  ni moja ya utekerezaji wa Agizo la Mh.Rais Dkt.John Magufuli kuwa kila Mwisho wa Mwezi iwe ni siku ya usafi wa Mazingira kote Nchini.

Akizungumza na wananchi hao Muwango alisema kuw, matumizi ya fedha hizo yalenge katika kuleta mabadiriko ndani ya familia na kuwaletea maendeleo na si vinginevyo.
"Hakikisheni fedha mnazozipata kutokana na korosho mnazitumia vizuri ikiwa nipamoja na kujiretea maendeleo kwa kujenga nyumba,kujenga vyoo bora,kuwapeleka watoto shule  huku mkiwa na akiba kwa ajili ya  k Maendeleo"" Alisema Muwango na kuongeza kuwa
"" Kila Mwananchi anatakiwa awe na uchungu na fedha za korosho kutokana na maumivu mnayoyapata  kutokana na zao hili,mnapoteza muda mwingi na fedha kununulia  dawa  za kupulizia,hivyo mnapaswa kuwa na uchungu   na fedha  mnazozipata m zitumieni kwa uangalifu na umakini mkubwa""Alisema Muwango.

Aidha aliwataka wazazi kuhakikisha wanawaandikisha watoto shule wale wote waliofikia umri wa kuanza masomo ya shule ya Msingi.Pia kwa wale waliofauhuru na kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 wahakikishe wanaenda shule,na mazazi atakaezembea hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
"Sitamvumilia Mzazi,Mlezi aunmtu yeyote yule atakaebainika kutompeleka mtoto shule,nitamchukulia hatua kali,hivyo ninawaomba tuwapekeke watoto shule mara tu zitakapofunguliwa.

Akizungumzia kuhusu kilimo aliwataka kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mazao ya muda mfupi,ili waweze kupata chakula cha kutosha hivyo kuondokana na adha ya njaa.Pia aliwasihi kukitumia vizuri  na kwa uangalifu chakula kilichopo ili waweze kuondokana na adha ya njaa.

"Nawaomba twende shambani kulima,tusikae vijiweni na majumbani wakati wa msimu huu wa kilimo, tuzitumie hizi mvua zinaoendelea kunyesha kwa kilimo,  tupande mbegu za  bira kwa kuzingatia  Elimu tuliyoipata kutoka kwa wataalamu wetu wa kilimo 
ili tuoate chakula cha kutosha na hatimae kuondokana na baa la njaa kwa wilaya yetu.

 Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Mh.Rukia Muwango akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ruponda mapema leo hii katika zoezi la usafi wa Mazingira 

 Wananchi wa kijiji cha Ruponda wilayani Nachingwea waliojitokeza kushihiriki katika  zoezi la usafi wa Mazingira leo hii wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyoRukia Muwango.  

0 maoni:

Chapisha Maoni