Jumamosi, 23 Desemba 2017

*MAVUNDE KUENDESHA OPARESHENI MAALUM YA KUKAGUA WAAJIRI AMBAO HAWAJATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MHAGAMA LA KUJIUNGA NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) NCHINI*

Posted by Esta Malibiche on DEC 23,2017 IN NEWS


 NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde ameendelea kukazia maagizo ya Mh Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Jennister Mhagama aliyoyatoa kuwataka waajiri wote wawe wamejisajili katika mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kwa kubainisha kwamba kwasasa inaendelea operesheni maalum ya kuhakikisha maagizo hayo ya waajiri kujisajili katika mfuko wa fidia yanatekelezwa kwa mujibu wa sheria.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifungua Baraza la kwanza la Wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi(WCF)katika makao makuu ya ofisi za WCF Jijini Dar es salaam kwa kuwataka waajiri wote nchini kutekeleza sharti la kisheria la kujiunga na mfuko wa huo wa fidia ili kuilinda nguvu kazi ya Tanzania kutokana na madhara/magonjwa yatokanayo na kazi na kuahidi kwamba atalisimamia agizo la Waziri kwa kuendesha operesheni ya ukaguzi nchi nzima kubaini waajiri ambao bado hawajatekeleza takwa hilo la kisheria ambao kwa mujibu wa maelezo ya Mh Naibu Waziri Mavunde watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa WCF Ndg Masha Mshomba amebainisha kwamba Mwajiri yoyote atakayekutwa  hajajisajili katika Mfuko atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwamo faini isiyozidi *Tsh 50m* au kifungo cha *miaka 5* Jela kwa Mkuu wa Taasisi husika au vyote kwa pamoja kama ilivyoainishwa katika kifungu cha *71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi No. 20 ya Mwaka 2008*







0 maoni:

Chapisha Maoni