Jumapili, 17 Desemba 2017

MAVUNDE AYATAKA MAKAMPUNI KUFADHILI MCHEZO WA KARATE NCHINI

Posted by Esta Malibiche on DEC 17,2017  IN NEWS

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde ameyataka makampuni,viwanda na Taasisi mbalimbali nchini kusaidia kufadhili mchezo wa Karate nchini ambao umeanza kukua kwa kasi hivi sasa.

Mavunde ameyasema hayo wakati akifungua mashindano ya kitaifa ya Karate katika ukumbi wa Kilimani Dodoma yanayojumuisha Timu za Karate kutoka Mikoa mbalimbali nchini na baadhi ya timu waalikwa kutoka Kenya.

“Wafadhili wengi hivi sasa wameweka nguvi kubwa katika kusaidia michezo ya mpira  miguu,pete,wavu na kikapu,ni muda sasa muafaka sasa kuangalia aina mingine ya michezo kama huu wa karate ambao unaweza kutuletea sifa katika medani za kimataifa”Alisema Mavunde.

Aidha akimkaribisha Mgeni Rasmi,Kiongozi wa Karate nchini Bwana Kitte Mfilinge alimuomba Mh Mavunde kusaidia kuutangaza na kuukuza mchezo huu kwa kushirikiana na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili upate uzito stahili kama ilivyo michezo mingine.



















0 maoni:

Chapisha Maoni