Jumanne, 19 Desemba 2017

SELEMAN JAFO:KILA MKOA UHAKIKISHE UNASIMAMIA LISHE ILI KUPUNGUZA UDUMAVU

Posted by Esta Malibiche on DEC 20,2017 IN NEWS

image1.JPG
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo akizungumza na Wakuu wa Mikoa(hawapo pichani) kuhusu Mikataba ya Utendaji kazi na Usimamizi wa Shughuli za Lishe katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mikataba hiyo imesainiwa jana baina ya WN-OR-TAMISEMI na Wakuu wa Mikoa yote Nchini.  
image2.JPG
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo(katikati) alisainishana Mkataba  wa Utendaji kazi na Usimamizi wa Shughuli za Lishe na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Evarist Ndikilo(kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Chiku Galawa kw niaba ya Wakuu wa Mikoa yote Tanzania.
image3.JPG
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo(katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Evarist Ndikilo(kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Chiku Galawa wakionyesha Mkataba wa Utendaji kazi na Usimamizi wa Shughuli za Lishe mara baada ya kusaini makubaliano hayo.
image4.JPG
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo akimkabidhi Naibu   Waziri wa OR-Tamisemi Mhe. Josephat Kandege Mkataba wa Utendaji kwzi na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji katika Mikoa na Halmashauri zote Nchini.
image5.JPG
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo akimkabidhi Naibu   Waziri wa OR-Tamisemi Mhe. George Kandege Mkataba wa Utendaji kazi na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji katika Mikoa na Halmashauri zote Nchini.
image6.JPG
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo (katikati mbele) akiwa katika Picha ya pamoja na Manaibu Waziri Tamisemi pamoja Wakuu wa Mikoa baada ya kusaini Mkatana wa Utendaji Kazi na Usimamizi wa shughuli za Afya.
…………..
Nteghenjwa Hosseah,Tamisemi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo (Mb) amewaongoza wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara, kupitia na kusaini Mkataba wa Utendaji kazi na Usimamizi wa shughuli za Lishe kwa kila mkoa katika kikao kazi kilichofanyika mjini Dodoma.
Akiongea na Wakuu wa Mikoa katika ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma, Mhe. Jafo amesema maelekezo hayo awali, yalitolewa na Mhe. Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu, kuhusu tatizo la Lishe katika Mikoa na Kwa sasa Taifa limeamua kulishughulikia na Fedha imetengwa  katika bajeti ya mwaka  wa fedha 2017/2018.
“Tumesaini hii mikataba kwa lengo kubwa la kuhakikisha kwamba Wakuu wa Mikoa kama viongozi wa Wakuu wa Mikoa, wahakikishe halmashauri zao zinaenda kutekeleza mipango yao ya bajeti ambayo imetengwa katika halmashauri zao hususan ni suala la Lishe ambalo kwa sasa ni agenda kubwa na tutataka tuisimamie ili kuondoa Udumavu katika jamii zetu.
Mhe. Jafo amesema Wakuu wa Mikoa wanayo dhamana kubwa ya kusimamia miradi ya maendeleo kama ujenzi wa vituo vya afya na suala la lishe kwa ujumla, hivyo Watendaji watoe taarifa zao kwa Wakuu wa Wilaya kabla ya kuwasilishwa kwa Wakuu wa Mikoa kwa hatua stahiki.
“Wakurugenzi watoe taarifa kwa Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Wilaya nao wawasilishe kwa Wakuu wa Mikoa ili waone namna ya kuzisemea taarifa hizo katika suala zima la utekelezaji wa mipango ya Serikali”.
Aidha, amewataka Wakuu wa Mikoa kuwaelekeza na kuwasimamia Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya masuala ya lishe na ujenzi wa vituo vya afya 2011 ambavyo mpaka sasa vimeboreshwa na kujengwa ili kutoa huduma bora kwa jamii.   
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe S. Kebwe amesema, anaipongeza Serikali kwa kutoa takribani shilingi 11.6 Bilioni kwa ajili ya suala la lishe hasa katika kipengele cha udumavu.
Aidha, amesema suala zima la upatikanaji wa chakula mkoani Morogoro sio tatizo bali ni elimu ya ulaji chakula ndiyo inapaswa kutolewa ili kupunguza utapiamlo lakini pia kumekuwepo na tatizo la Maafisa Lishe katika halmashauri nchini kupangiwa kazi nyingine, kwa mfano kufanya kazi ya Idara tofauti kama vile kukusanya kodi.
Naye Stephen Motambi, Kaimu Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, amesema suala la Lishe limekuwa likifanyika katika Mikoa na Halmashauri zote katika kukabiliana na tatizo hili lakini kwa hivi sasa hali ya udumavu ni asilimia 34 hivyo mikoa inapaswa kuweka mikakati kuhusiana na kuondoa kabisa tatizo la lishe.

0 maoni:

Chapisha Maoni