Jumamosi, 9 Desemba 2017

MIAKA 56 YA UHURU WA TANZANIA BARA: BABU SEYA NA MWANAE 'OUT’

Posted by Esta Malibiche on DEC 9,2017 in NEWS


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli leo ametoa msamaha kwa wafungwa 8157 ambapo wafungwa 1828 wataachiwa huru leo na 6329 watapunguziwa muda wao wa kifungo,  Pia ametoa msamaha kwa wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa na kuziagiza idara husika kuwatoa leo au kesho


Rais Magufuli ametangaza kuwasamehe familia ya mwanamuziki Nguza Viking maarufu kama Babu Seya  pamoja na mwanaye Papii Kocha ambao walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha gerezani.

Akihutubia taifa katika sherehe za Uhuru mjini Dodoma, Rais Magufuli pia  ametangaza kusamehe wafungwa 8,157, na kuagiza wafungwa 1,828 kati yao watolewe magerezani mara moja na waliobaki wapunguziwe muda wa kukaa gerezani ili waje watolewe kwa mujibu wa vifungo vyao.

Pia ametangaza kuwasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa, na kuagiza watolewe gerezani leo au kesho.

Kuhusu waliohukumiwa kunyongwa, Rais Magufuli ametoa mifano kwa kusema “Yuko mtu aliyefungwa akiwa na miaka 18, na sasa hivi ana miaka sitini na kitu. Yumo mtu anaitwa Mganga Matonya, ana miaka 85 na ameishakaa gerezani miaka 44”

0 maoni:

Chapisha Maoni