Ijumaa, 1 Desemba 2017

WAKAZI WA MTAA WA MJIMWEMA MAFINGA MJINI WAKO HATARINI KUKUMBWA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Posted by Esta Malibiche on DEC 1,2017 IN NEWS


 Na Esta Malibiche
Mafinga

WANANCHI wakazi wa kitongoji cha Mbigili mtaa wa mji mwemakata ya Boma  Halmashauri ya mji wa  Mfinga ,Mkoani Iringa wameitaka Seriakali  kunusuru Afya zao ambazo ziko hatarini kukumbwa na  magonjwa ya mlipuko yakiwemo kuhara,kupindupindu kutokana na dampo kubwa la taka lililopo katika makazi yao Mjini Mafinga.

Akizungumza leo na blog hii ya KALI YA HABARI huku akitokwa na machozi Moi Mgoda  ambaye ni mkazi wa eneo huilo alisema Afya zao ziko hatarini kutokana na Halmashauri kushindwa kutoa hizo taka kwa wakati,huku wakazi hao wakikabiliwa na harufu mbaya,kuzagaa kwa taka hadi katika makazi yao Pamoja na nzi.


‘’Moja ya kero tunayoipata hapa ni kuzagaa kwa taka hadi mlangoni kwetu,harufu mbaya na kuja kwa nzi katika makzi yetu.Tunashindwa kuhimili hali hii inayohatarisha Afya ya familia yangu Pamoja na familia za weakazi wa eneo hili,pia watoto wadogo wanacheza katika dampo hili’’Alisema Mgoda

Aliongeza kuwa Pamoja na familia zao kuathirika kiafya pia dampo hilo lipo katika vyanzo vya Maji,maji yanayotumiwa na  wakazi wa Halmashauri hiyo,hali inayoweza kuleta athari kwa wakazi wa mji wa Mafinga kukumbwa na  magonjwa kutokana na  matumizi ya maji.

‘’Asilimia kubwa ya wananachi wamji wa Mafinga wanatumia haya maji,tena wengine hata hawachemshi na dampo lipo katika vyanzo vya maji pia kipindi hiki mvua zinanyesha na kila aina ya taka zinatupwa hapa.Tunaomba dampo hili liondolewe katika makazi ya watu na itafutwe eneo amabalo halina makazi ya watu ili kunusuru Afya za watanzania’’’Alisema Mgoda

Kwa upande wake Beatrice Nestory nae alisema,kero hii ya kulundikana kwa taka kunatokana na Halmashauri hiyo kukosa Gari la kuzolea taka,hata hivyo gazri inatosomba toaka kutoka majumbani au katika mitaa ni toyo dogo ambalo halikidhi mahitaji ya wakazi waHalmashauri ya Mji wa Mafinga.

‘’Sisi tumekuwa na kazi ya kuwafukuza watoto ambao wamekuwa akija na kucheza katika dampo hili, na kuokota vitu mbalimbali,kwa kweli ni sehemu hatari sana si kwa watoto tu bali pia kwa sisi watuwazima afya zetu zipo hatarini’’Alisema Beatrice
Jitihada za kumtafuta  Diwani wa Kata hiyo Julius Pius  ili kujua ni hatua gani alizozichukua kuhakikisha ananusuru maisha ya wakazi wa eneo hilo,zilifanikiwa nae alisema kuwa alifikishaa tarifa kwa Halmashauri ya Mji wa Mafinga,kuondoa dampo hilo eneo la makazi ya watu lakini mpaka sasa hakuna mafanikio yeyote.

Julius aliitaka Halmashauri ya Mji wa Mafinga kuchukua hatuia za haraka za kulihamisha dambp hilo kwa kuwa wananchi wake wakiwemo watoto wadogo wapo hatarini kukumbwa na magonjwa.

Ndugu Mwandishi wa habari kwa upendo kabisa ninaiomba Halmashauri ichukue hatua kulihamisha dampo hilo,ukiangalia lipo mjini kabisa na lipo katikakatik ya makazi ya watu ni hatari sana.Pia lipo kwenye vyanzo vya maji , na wananchi wanalima vinyungu ambavyo mboga za majani tunazokula hapa Mafinga zinazalishwa hapo,hali hii nimbaya sana,si nzuri kwa na nimejaribu kulalamika sana bila mafanikio’’Alisea Diwani
Alisema  kwa  aliwaita watu wa afya
  ambao huwa  anapenda sana  kuwashirikisha katika mambo mbalimbali ingawa majibu yao hayaridhishi.

‘’Siku moja wananchi walikuwa wameipigia simu wakinitaarifu juuya kero wanayoipata kutokana na dampo hilo,kwa bahati nzuri nilipoongea na mtu wa afya na mtendaji wangu wa kata akiwepo alinijibu dampo hilo limewekwa kwa muda  lakini cha ajabu mpaka leo hii bado lipo na linaendelea kuwepo bila kuangalia athari wanazozipata wakazi wa eneo hilo ‘’Alisema Diwani huyo na kuongeza kuwa

Mimi ni kiongozi si mwanasiasa na shughuli zangu napenda ziende kama kiongozi mahali ninapotetea umma ninapenda kuona hatua zinachukuliwa haraka.Kilio change hakijasilikizwa na mwenywe umeshuhudia  atahari kubwa kwa watoto wa shule na wananchi amabao wanaingia kule kuchambua vitu.

Huwa ninaumia sana ninapopeleka kilio kwa Hamashauri ambayo ndiyo Serikali yenyewe lakini inashindwa kuchukua hatua,ni vema sauti yetu ikapaa zaidi katika nagzi za juu uli hatua za haraka ziweze kuchukuliwa kuzoa taka na kuliondoa dampo ili kunusuru uhai wa wananchi  amabao wapo katika mazingira hatarishi,ambapo hali hii ikiendelea maafa makubwa yanaweza kutokea ya mlipuko wa magonjwa ya kuhara na kipindupindu.Alisema Diwani Julius Pius



0 maoni:

Chapisha Maoni