Alhamisi, 21 Desemba 2017

MAVUNDE ATEMBELEA UJENZI WA DARAJA LA CHIHANGA-GAWAYE NA ZAHANATI YA ZEPISA,HOMBOLO MAKULU-DODOMA MJINI

Posted by Esta Malibiche on DEC 21,2017 IN NEWS

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM,Mh Anthony Peter Mavunde leo ametembelea ujenzi wa Daraja linalounganisha vijiji vya Chihanga na Gawaye kata ya Chihanga Jimbo la Dodoma Mjini na kupongeza kasi ya ujenzi inayofanywa na Mkandarasi katika kuhakikisha daraja hilo linakamilika mapema ili wananchi waondokane na adha kubwa ya kutokupitika eneo hilo kipindi cha masika.

Daraja hilo lenye thamani ya Tsh 49m linatarajiwa kukamilika mapema January 2018 na hivyo kuondoa kero ya muda mrefu ya kutopitika kwa eneo hilo.

Aidha Mh Mavunde pia ametembelea ujenzi wa Zahanati ya Zepisa akiongozana na Mkurugenzi wa Global Space East Africa Ltd Ndg Gaston M. Francis aliyeoongozana na Mhandisi Malcom kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Mbunge Mavunde katika kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo ambapo Mavunde ameahidi kuchangia matofali 1000 na saruji mifuko 100,Manispaa ya Dodoma 10m na Ndg Gaston M. Francis kwa niaba ya Kampuni ya Global Space East Africa Ltd ameahidi kuchangia mifuko 50 ya saruji na vifaa vya ndani vya Zahanati baada ya kukamilika.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Hombolo Ndg Jacob Lemanya kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa jitihada kubwa anazofanya za kuwasaidia katika ujenzi wa Zahanati kwa kutafuta wafadhili mbalimbali ili kufanikisha ujenzi huu wa zahanati na kuahidi kuunga mkono jitihada hizo kwa wao kujitolea katika shughuli mbalimbali za ukamilishwaji wa zahanati hiyo










0 maoni:

Chapisha Maoni