Alhamisi, 28 Desemba 2017

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA ZAHANATI MIBURE

Posted by Esta Malibiche on DEC 29,2017 IN KITAIFA


PMO_3575 airport
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea, kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, Desemba 28, 2017.
PMO_3641 mibure
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwananchi wa kijiji cha Mibure, Mzee Menrad Kilian, baada ya kukagua ujenzi wa zahanati kijijini hapo, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Desemba 28, 2017.
PMO_3661 mibure
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mibure, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho Desemba 28, 2017. Waziri Mkuu yupo jimboni kwake kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.
PMO_3699 namakuku
Mkurugenzi Mtendaji wa KALIF Construction, Ally Mohamed Libaba akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) wakati wakijaribu kuvuta maji kutoka kwenye pampu ya mradi wa maji wa kijiji cha Namakuku, Desemba 28, 2017. Wa kwanza kulia ni msimamizi wa mradi huo, Bw. Fadhil Ally Libaba.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
………….
*Aagiza zahanati ikiisha ipelekewe kifaa ca kutunzia watoto njiti
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameanza ziara fupi ya siku tatu, kukagua
miradi ya maendeleo jimboni kwake katika wilaya ya Ruangwa mkoani
Lindi.
Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, amekagua
miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na kuzungumza na wananchi kaika
vijiji vya Mibure, Namakuku, Chienjere, Namahema A na Namahema B.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mibure leo mchana (Alhamisi,
Desemba 28, 2017) mara baada ya kukagua zahanati ya kijiji hicho,
Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na ujenzi unavyoendelea na akamwagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa ahakikishe zahanati hiyo
ikikamilika inapata kifaa cha kuwatunzia watoto njiti kwa sababu
kijiji hicho kiko mbali na Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa.
“Nilileta makontena yenye vifaa vya hospitali, na humo ndani mlikuwa
na vifaa vya kuwatunza watoto njiti (watoto wanaozaliwa kabla ya muda
kutimia). Hakikisha hawa wanapata kifaa hicho kwa sababu hawana gari
la kubeba wagonjwa, na pia wako mbali na hospitali ya wilaya na pia
kituo cha afya cha jirani kiko mbali pia,” alisisitiza.
Akizingumzia kuhusu upatikanaji wa umeme kijiji hapo, Waziri Mkuu
alisema: “Mibure ipo kwenye mipango ya kupata umeme ambao unatoka
Nagurukuru, -Nghimbwa-Chienjere-Namakuku-Mibure.”
Aliwataka vijana wa kata hiyo, wachangamkie fursa kwa muanda mitaji ya
kuwa na gereji za kuchomelea vyuma, saluni na viwanda vidogo vya
usindikaji.
Mapema, akisoma taarifa ya ujenzi wa zahanati ya Mibure mbele ya
Waziri Mkuu, Mwenyeiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Chilemba alisema
mradi huo umekwishagharimu sh. milioni 52, ambapo kazi zilizokamiliak
ni jengo la zahanati, kichomea taka na choo chenye matundu matatu.
Alisema wanakabiliwa na changamoto ya kupanda holela kwa gharama za
vifaa vya ujenzi, kupokea michango kidogo kutoka kwa wananchi, ukosefu
wa nyumba ya mganga na wauguzi na kiasi cha fedha cha sh. milioni 8.26
za kununulia samani.
Bw. Chilemba alisema kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutasaidia
wakazi wa vijiji jirani vya Njawale, Namakuku, na vijiji jirani vya
wilaya ya Nachingwea ambavyo vinapakana na wilaya ya Ruangwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, DESEMBA 28, 2017

0 maoni:

Chapisha Maoni